Fundraising 2012/Translation/Isaac appeal/sw
Banner[edit]
- Tafadhali soma:
Mwito wa kibinafsi kutoka kwa
Mhariri wa Wikipedia Isaac Kosgei
Appeal[edit]
Kutoka kwa mhariri wa Wikipedia Isaac Kosgei[edit]
Maarifa ni ya kila mtu, hata wale bila mtandao wa intaneti. Siku hizi, mashule mengi Kenya yana tarakilishi. Lakini mengi bado hayana intaneti, sana sana mle vijijini katika nchi yangu.
Kama mhanga wa Wikipedia, mchango wangu mkuu ni usamabzaji wa toleo la Wikipedia lisilohitaji intaneti. Toleo hili ni la maandishi pekee.
Kusafiri kwa basi na teksi, huku tukiwa tumejiami kwa diski-ROM, diski-USB, kompyuta ya mkononi na projector, mie na rafiki zangu hutembelea mashule Kenya kote.
Sisi husakinisha Wikipedia katika makompyuta ya shule na kuwaelimisha walimu ambavyo mradi unavyoendeshwa. Kisha tunaipa shule mzima mifano tukitumia projector na kupeana hotuba ya umuhimu wa wikipedia
Walimu wanasema ya kwamba mradi huu umebadili maisha ya maelfu ya wanafunzi na unaleta mapinduzi katika elimu nchini kenya. Wanafunzi huwa wenye furaha na hutushukuru kwa vitendo hivi.
Kutokana na wikipedia - na safari kadha refu katika mabasi yaliyojawa na vumbi - kizazi kizima cha wanafunzi sasa kina kamusi elezo kubwa zaidi duniani. Ninavyoona, hili ndilo jambo bora zaidi kutendeka.
Unapochangia kwa Wikipedia, unabadilisha dunia. Kutoka kwa mvunguni mwa moyo wangu, asante.
Isaac Kosgei
Mwanafunzi wa Biashara na mhanga wa Wikipedia