Jump to content

Matukio ya Kampeni

From Meta, a Wikimedia project coordination wiki
This page is a translated version of the page CampaignEvents and the translation is 89% complete.
Outdated translations are marked like this.

Kiendelezi cha Tukio la Kampeni ni zana madhubuti iliyoundwa ili kuboresha usimamizi na mwonekano/ugunduzi wa matukio ndani ya Wikimedia. Kiendelezi hiki kinatmbulisha mkusanyiko wa vipengele vinavyolenga kufanya mpangilio na ushiriki wa tukio kuwa rahisi na bora.

Kiendelezi cha CampaignEvent kinakuja na vipengele muhimu kadhaa:

Zana ya Usajili wa Tukio

Zana ya Usajili wa Tukio huruhusu waandaaji wa kampeni kudhibiti usajili wa tukio moja kwa moja kwenye wiki. Zana hii hurahisisha mchakato wa kufuatilia waliohudhuria, kudhibiti maelezo ya usajili, kutuma barua pepe kwa washiriki waliosajiliwa, mwingiliano na dashibodi ya Mipango na Matukio na mengine mengi.

Orodha ya Matukio

Orodha ya Matukio ni ukurasa maalum unaoonyesha orodha ya kimataifa, otomatiki ya matukio kwenye miradi ya wiki. Kipengele hiki hurahisisha matukio kugundulika kwa kuweka matukio kati ya wiki kwenye kalenda moja kuwaruhusu watumiaji kupata na kujiunga na matukio yanayowavutia. Waandaaji hawahitaji kufanya kazi yoyote ya ziada ili tukio lao lionekane kwenye Orodha ya Matukio. Ili mradi watumie Usajili wa Matukio, tukio lao litaonekana kwa watumiaji duniani kote. Orodha ya Matukio pia inajumuisha vichujio, ili watumiaji waweze kutafuta kwa urahisi aina mahususi za matukio.

Maboresho Yajayo

Kiendelezi cha CampaignEvent kimeundwa kwa kuzingatia unyumbufu, kikiruhusu kuunganishwa kwa zana za ziada ili kusaidia waandaaji na washiriki wa kampeni. Zana moja kama hiyo inayoundwa kwa sasa ni Orodha za Mialiko. Zana hii itasaidia waandaaji kwa kupendekeza washiriki watarajiwa ambao wanaweza kupendezwa na matukio yao yajayo, kuboresha zaidi ushiriki na mahudhurio.