Jump to content

Kampeni/Timu ya Bidhaa ya Shirika/Usajili/Muhtasari wa V1

From Meta, a Wikimedia project coordination wiki
This page is a translated version of the page Campaigns/Foundation Product Team/Registration/V1 Summary and the translation is 94% complete.

Timu ya Kampeni imeunda na kutoa toleo jipya la zana ya usajili wa tukio, linaloitwa V1. Katika ukurasa huu, tutaelezea mipango na maono ya toleo hili.

V1 ni nini?

V1 ya zana ya usajili wa tukio iliwezeshwa kwenye Meta-Wiki, pamoja na baadhi ya wiki za majaribio, mnamo Novemba 2022. Toleo hili la zana ya usajili wa tukio linatokana na toleo la V0 la zana. Lengo ni kuboresha V0 kwa kutumia vipengele na maboresho mapya, ili waandaaji waweze kuwa na zana ambayo inaweza kutumika katika matukio yao ya kampeni (na aina nyingine za matukio). Kipengele cha V1 hakina "kila kitu." Kwa hakika, tunapanga kutoa vipengele na maboresho zaidi baada ya V1. Hata hivyo, V1 ni imara zaidi, ina vipengele vingi, na ni muhimu kuliko V0, ikiwa na vipengele vingi vipya. Unaweza kupata maelezo zaidi kuhusu maboresho haya katika sehemu ya "Vipengele Muhimu" hapa chini.

Tarehe ya uzinduzi

  • Tarehe 3 Novemba 2022: Tulitoa toleo la awali la V1 (lenye idadi ndogo ya vipengele) kwenye testwiki na test2wiki.
  • Novemba 30, 2022: Tulitoa toleo jipya la zana ya usajili wa tukio kwenye Meta-wiki.

Kwa masasisho ya hivi punde, tafadhali tembelea ukurasa wa toleo.

Vipengele muhimu

Tumetoa hapa chini orodha ya uboreshaji wa vipengele vya msingi katika V1. Maboresho haya ya vipengele yalichaguliwa baada ya kupokea maoni kutoka kwa wanaojaribu V0 na kushauriana na timu za ndani za Wikimedia Foundation.

Vipengele vilivyopewa kipaumbele kwa toleo la kwanza (mwishoni mwa Novemba 2022):

  • Usaidizi kwa mwandaaji wa tukio kubainisha saa za eneo husika
  • Usajili wa kibinafsi: chaguo la washiriki kujiandikisha na kuonyesha tu jina lao la mtumiaji lililosajiliwa kwa waandaaji wa hafla hiyo
  • Barua pepe za uthibitishaji kiotomatiki baada ya washiriki kujiandikisha

Baada ya V1: Vipengele ambavyo tunaweza kuwa tunafanyia kazi baada ya toleo la kwanza:

  • Kuunganishwa na Dashibodi ya Mipango na Matukio
  • Uwezo wa mratibu kutuma barua pepe kwa washiriki (iwapo anwani ya barua pepe imehusishwa na akaunti zao)
    • Kumbuka kuwa kuna kazi ya sasa ya waandaaji kutuma barua pepe kwa washiriki kupitia kipengele cha 'Tuma barua pepe kwa mtumiaji huyu' kwenye ukurasa wao wa mtumiaji. Hata hivyo, kwa kipengele hiki, mratibu ataweza kutuma ujumbe kwa mmoja, baadhi, au washiriki wote mara moja.
  • Msaada wa kijiografia
  • Uwezo wa waandaaji wengi kuhusishwa na tukio

Zana-mfano

Ikiwa ungependa kupata hisia ya jinsi nyenzo hii itakavyonaweza kufanya kazi, tunakualika uangalie mifano hii. Tafadhali fahamu kuwa hizi sio bidhaa zinazofanya kazi moja kwa moja. Ilikuwa mifano iliyoundwa na mbunifu wa timu yetu ili kutoa wazo la awali la zana, lakini matokeo ya mwisho labda yataonekana na kuhisi tofauti kidogo.