The Wikipedia Library/Newsletter/August-September2017/sw

From Meta, a Wikimedia project coordination wiki
Jump to navigation Jump to search
This page is a translated version of the page The Wikipedia Library/Newsletter/August-September2017 and the translation is 89% complete.

Outdated translations are marked like this.
Other languages:
English • ‎Kiswahili • ‎Yorùbá • ‎français • ‎العربية • ‎中文 • ‎한국어
Wikipedia Library owl.svg Maktaba Ya Wikipedia
Bookshelf.jpg
Books & Bytes
Issue 24, August–September 2017

Jisajili ili kupata taarifa za kila mwezi

Katika ukurasa huu tunakupa dondoo mbalimbali zinazopatikana katika mkutano mkuu wa shirika la Wikimedia Foundation uitwao WIKIMANIA ambao hufanyika kila mwaka.Dondoo hizo ni pamoja na majadiliano, taarifa mbalimbali zinazohusu maemdeleo ya ulimwengu kiujumla na taarifa mbalimbali zinazohusu vitu vya kijamii vinavyohusiana na maktaba na elimu ya kidijitali.

Kundi la Watumiaji

Kundi la Watumiaji wa Wikipedia ni kundi la watumiaji wa Wikipedia wanaojihusisha na kuwaunganisha Watumiaji wa kawaida wa Wikipedia na watu wa maktaba ya Wikipedia na hivyo kuwa kama sehemu ya kukutanisha pande hizi mbili.Tangu kuanzishwa kwake, waanzilishi wa kundi hili wamekuwa wakifanya kazi kwa bidii kubwa kuhakikisha malengo ya kundi yanatimia. Miezi miwili iliyopita waanzilishi hawa wamekuwa katika hali ya kutingwa sana kutokana na kuwa na vikao viwili vya waazilishi na vikao vya wazi vya pande hizi mbili yaani watu wa maktaba ya Wikipedia na watumiaji wa Wikipedia wa kawaida. Vikao vya wazi viliruka moja kwa moja hewani kwa kutumia mtandao wa Hangouts On Air, rekodi na dondoo za vikao hivyo zinapatikana kwenye kiungo hiki. Katika kikao cha waanzilishi wa kundi hili, mchakato wa kubadilisha jina la kundi lililopo sasa uliibuka na kuafikiwa na wengi, pia hata katika vikao vya wazi suala hili liliafikiwa na wengi. Katika vikao vyote hivi,suala la kamati tendaji ya kundi hili liliibuka ambapo makubaliano yalikuwa kwamba kila mtu anaweza kujipendekeza mwenyewe kuwa katika kamati hiyo.Suala la kufufua mchakato wa Wikipedia Loves Libraries pia ulijadiliwa ili kusaidia watumiaji wapya wa Wikipedia kupata msaada kwa haraka zaidi, hivyo ukurasa huo upo katika matayarisho ya kutengenezwa katika ukurasa mkuu wa shughuli za Wikipedia uitwao Meta.Ukurasa wa draft homepage umepunguzwa kwa kiasi kikubwa huku ukiwa na taarifa fupi na za kueleweka kwa urahisizaidi na huku ukiwa na viungo vya vyanzo husika.Kifuatacho:Wito wa kupiga kura juu ya Jina la kundi, nembo ya kundi na watu binafsi kujipendekeza wenyewe kuwa katika kamati tendaji ya kundi hili.

Duniani

Matawi mengi duniani yanaendelea kuibuka na kuleta hamasa kubwa katika kuwasaidia wahariri wa Wikipedia wenye uhitaji haswa.Njia mbalimbali zimekuwa zikitumika ili kunufaisha na kuyapa nguvu makundi ya wahariri wasiotumia Kiigereza.Kuna uhitaji mkubwa wa kushirikishana vitu muhimu kutoka katika kitengo cha taarifa kwa kutumia lugha mbalimbali, na mwezi uliopita polepole tumeweza kuongeza idadi ya tafsiri za Books & Bytes na sasa tunawafikia wote ambao wana penda kufikiwa na sauti ya Books & Byteskwa lugha yao wenyewe.

Zawadi kwa Mratibu Bora

Mratibu Bora ni mchakato wa kutoa zawadi ya kuwatambua waratibu watakaoibuka kidedea katika kuratibu vizuri kazi za maktaba ya Wikipedia katika jamii zao kwa kila robo mwaka. Na mshindi ni...

Mtumiaji:Csisc, Tunisia
Hongera kwa Mtumiaji:Csisc kutoka Tunisia kwa kushinda nafasi ya mratibu bora kwa robo mwaka ya (Julai-Septemba)!!! Alisherehekewa robo hii ya mwaka kutokana na moyo wa kujituma katika kutoa makala ndefu zihusuzo Tunisia kwa kutumia marejeo ya kutosha na makala zenye ubora.Kwa maneno yake mwenyewe anasema kuwa “Hata hivyo tumekumbana na upungufu wa marejeo ya mitandaoni yanayohusu makala kutoka Tunisia na upungufu huu wa marejeo ya mitandaoni yanayohusu makala kutoka Tunisia umesababisha kudhoofika kwa ubora wa makala za Wikipedia zinazohusu mambo haya muhimu”.

Ugumu katika kutatua matatizo umepelekea kuundwa kwa tawi la Tunisia la TWL (Tunisia TWL la Tawa), hili ni tawi la kwanza na la aina yake na la kipekee.Tawi hili litakuwa likitoa marejeo yasiyokuwa mtandaoni na marejeo ya nchini humo kwa wachangiaji wa Wikipedia wa Tunisia kwa kupitia idara ya (Wikipedian-in-Residence) ya nchini humo katika maktaba za Medinas nchini Tunisia, na kuvipakia/kuviweka mitandaoni vitabu vya zamani katika tovuti za jamii na ili vitumike kama vyanzo vya makala katika Wikipedia.Unaweza kusoma zaidi hapa

Wikimania Wakati wa Ndege Wafananao

Kipindi cha "Ndege wafananao" katika mkutano wa Wikimania ilikuwa ni nafasi ya viongozi wanaojihusisha na mambo ya maktaba ya Wikipedia kukutana na kufanya ubia na wachapishaji, kuandaa matamasha katika taasisi mbalimbali na kutembelea mashirika mbalimbali au makundi mbalimbali ya kikanda.Hizi hapa baadhi ya dondoo:

 • New York: Inaunganisha nguvu na mashirika yaliyo ndani ya Wikipedia (chapter) ili kuhudhuria mikutano na kujadili jinsi ya kushiriki katika Shughuli za Wikipedia.Ilishirikiana na wanamaktaba wenyeji katika 1lib1ref.Ushirikiano wa mtu na mtu unakuza ufanisi.
 • Wanamaktaba kutoka Queensland wameongeza zaidi ya nukuu 1000 wakati wa 1lib1ref.
 • Art+Feminism inakaribia kufanya adhimisho lake la kumbukumbu ya miaka mi 5 tangu kuanzishwa kwake.
 • Mexico City: Mradi wa vitabu vya zamani ni pamoja na kuvifanya kuwa katika hali ya kidijitali na kuvisambaza kwa kupitia Wikisource
 • Wikimedia DC: ni Kamusi inayoandika wasifu wa Wanawake.
 • Ukurasa wa mtandao wa twitter umefufuliwa kwaajili ya kubadilishana taarifa/ matangazo/ kushirikishana na kuwaalika wafuasi wapya
 • ORCID Wikipedian-in-Residence na WikiCite wametengeneza kifaa kiitwacho (Zotero) kwaajili ya kufanyia utafiti na kuusambaza huku kikirahisisha muundo wa taarifa katika Wikidata .Pia wameongeza mara mbili mfumo wa kuwatambua wahariri na wachangiaji uitwao (ORCID IDs) na wanawaalika wengine kuongeza ORCID IDs za watafiti wao.
 • Chuo cha York kitakuwa ni moja ya washiriki katika tamasha la kuhariri muziki huko nchinhi Canada lililopangwa kufanyika mwezi Octoba.Mradi wa ARL ujao utalenga zaidi jamii wenyeji katika Wikidata.
 • Tawi la maktaba ya Wikipedia liitwalo 'Farsi limefanya mikutano ya nje katika vyuo vya ndani ya nchi na limefanikiwa kumpa vyanzo kila mhariri anayehitaji.
 • Muundo mpya wa Wikipedia ya Kifaransa ({{bibliographie}}) ambayo inakuwezesha kuingiza taarifa kwenye Wikidata ili kuingiza nukuu nzima.
 • OCLC Wikipedia + na miradi ya maktaba imwesaidia kuinua hadhi ya “wanamaktaba wanaojishughulisha na Wikipedia”; mwishoni mwa mafunzo ya mtandaoni yanategemewa kuvuta vitu vya kimaktaba vya wazi zaidi ya 500 na kuwavuta watu (watu takribani 706 kwa mujibu takwimu za mwezi Julai)
 • Maktaba za Bodleian zinafanya mradi mfumo wa tovuti kwaajili ya vitabu huku zikipendekeza kuifanya Wikidata kama kituo cha mafunzo
 • Wikicite imetengeneza mfumo wa uwakilishi wa Vitabu vinavyotumiwa katika Wikidata kama sehemu ya kuweka wazi taarifa za Wikipedia na hifadhi za maktaba
 • Chuo kikuu cha West Virginia kimefanya mradi wa kuendesha mafunzo kwa wanafunzi yanayohusu kuandika programu za vigezo vya kustaafu kwa kupitia Wikipedia
 • Kipindi cha Mafunzo kwaajili ya wanamaktaba nchini London kinalenga kuwawezesha watumiaji kuielewa vizuri Wikipedia.
 • Northeastern inafanya kazi na Wanafunzi kwenye mazoezi mbalimbali ya nyumbani kwa wanafunzi na Wanafunzi wanaona kuwa Wikipedia ina msaada mkubwa katika vipaji vyao.
 • Laurentian wametengeneza kifaa kinachoweza kuvuta taarifa wakati wa kurekodi wasanii katika orodha yao kutoka kwenye Wikidata.
 • Kuna uhitaji wa kutafuta namna ya kujihusisha na Miradi ya Wikipedia.
  • Machiavellian approach: Tafuta kujua watu wanajali nini na wanaeleza nini jinsi suala hili linavyoweza kufanikiwa kupitia kile unachotaka kukifanya.
 • Namna gani inaweza kutumika kuzuia kushindwa?
  • Kuwa muwazi kuhusu falsafa isemayo Jiamini.
  • Fundisha watu wanaoweza kuwafundisha wengine.
 • Tatizo la wanamaktaba ni kwamba michango yao huchukuliwa kama kitu cha kupuuzwa.
 • Kundi la Wanamaktaba wa Wikipedia ni kama sehemu ya kushirikishana na kuomba msaada zaidi.

Uangalizi: Wiki Loves Archives

Dondoo kutoka blogi ya Wikimedia Blog post na Benoit Rochon, kutoka Wikimedia Canada

Vituo mbalimbali vya makumbusho vinakumbwa na ufinyu wa bajeti na lazima vifanye maamuzi magumu ya kuchagua makusanyo fulani ili kuzuia uharibifu.Zaidi ya miaka kadhaa iliyopita, Wikimedia Canada imekuwa ikijihusisha na kutengeneza Wikipedia katika lugha za waaboriginal.Suala hili ndilo lililopelekea maktaba na kumbukumbu za Quebec (BAnQ) kuwataka watu wa Montreal kutunza kumbukumbu za picha kwa kuandaa tamasha la kwanza lililoitwa first scan-a-thon

Kwa shughuli hii na kwa shughuli za scan-a-thons zijazo, Wikimedia Canada na WikiClub ya Montreal nchini Canada ilipata kifaa spesheli kwaajili ya kuchunguzia vivuli vya mikanda ya picha kwa ubora mkubwa. Baada ya mafunzo mafupi kutoka kwa mtaalamu wa makumbusho, watu waliokuwa wanajitolea katika tamasha hilo walianza kuweka vivuli hivyo vya picha katika vishikizi vya mikanda ya picha wakati wengine wakivifanya kuwa katika hali ya kidijitali. Wakati huohuo, wengine walihakikisha kuwa hakukuwa na vumbi, kwamba picha zinaonekana vizuri na kuhakikisha vigezo vingine vya ubora vinazingatiwa. Baada ya hapo timu ya watu hao wa kujitolea walipewa picha katika USB na wakapakia katika Wikimedia Commons na kwa baadhi ya picha walitolea maelezo mafupi kuhusiana na picha husika. Wengine walitafsiri maelezo hayo mafupi ya kwenye picha kwenda katika lugha mbalimbali, na kama makala fulani ya Wikipedia itatumia picha hizi, wahusika wataboresha makala.

Kwahiyo mwisho wa siku, zaidi ya picha 500 na nyaraka mbalimbali kuanzia mnamo kama miaka ya 1700 hivi, ziliwekwa katika mfumo wa kidijitali na kupakiwa katika Wikimedia Commons. Makumbusho haya yatakuwa na faida ya moja kwa moja kwa kuwa na hati miliki isiyokuwa na masharti ndani ya Commons, BAnQ wanaweza kuchukua na kutumia hizo picha za zamani ambazo bado hazijawa katika mfumo wa kidijitali bado pamoja na maelezo ya picha katika orodha yao wenyewe. Baada ya bajeti kutolewa kwenye Commons, watu wa kujitolea kutoka kote duniani waliboresha picha kidijitali kwa kuondoa makunyanzi, vumbi na machozi.

Jaribio hili kiujumla lilikuwa ni lenye mafanikio, washiriki wote na BAnQ walifurahishwa na matokeo.Picha zote zilizoskaniwa na kupakiwa zinaweza kupatikana katika Wikimedia Commons.

Bytes kwa kifupi

Jamii kwa ujumla

Muhimu

Inafaa kusoma (au Kuangalia)


Thanks for reading! To receive a monthly talk page update about new issues of Books & Bytes, please add your name to the subscriber's list. For email delivery of the newsletters, please subscribe here. To suggest items for the next issue, please contact the editor, The Interior (talk · contribs) at en:Wikipedia:The Wikipedia Library/Newsletter/Suggestions.