Mwongozo wa Kimataifa wa Mwenendo na Maadili/Kamati ya Uratibu/Uchaguzi/2024/Tangazo- Upigaji kura umefunguliwa
Appearance
Piga kura sasa ili kuchagua wanachama wa U4C ya awamu ya kwanza
- Unaweza kupata ujumbe huu ukiwa umetafsiriwa katika lugha za ziada kwenye Meta-wiki. Please help translate to your language
Wapendwa,
Ninawaandikieni ili kuwajulisha kuwa kipindi cha kupiga kura kwaajili ya kuchagua Kamati ya Kuratibu Mwongozo wa Kimataifa wa Mwenendo na Maadili (U4C) kimefunguliwa sasa hadi Mei 9, 2024. Soma maelezo kuhusu ukurasa wa kupiga kura kwenye Meta-wiki ili kupata maelezo zaidi kuhusu upigaji kura na ustahiki wa mpiga kura.
Kamati ya Kuratibu Mwongozo wa Kimataifa wa Mwenendo na Maadili(U4C) ni kikundi cha kimataifa kilichojitolea kutoa utekelezaji sawa na thabiti wa UCoC. Wanajamii walialikwa kutuma maombi yao kwa U4C. Kwa maelezo zaidi na majukumu ya U4C, tafadhali pitia Mkataba wa U4C.
Tafadhali washirikishe wanajumuiya wenzako ujumbe huu ili nao waweze kushiriki.
Kwa niaba ya timu ya mradi wa UCoC,