Shirika la Wikimedia Foundation/Sheria/Uteuzi wa Kamati
Kamati za kujitolea ni sehemu kubwa ya kile kinachofanya jumuiya ya Wikimedia, kuwa jumuiya. Watu wanaojitolea katika jumuiya yetu wanafanya kazi mbalimbali, kuanzia kuhariri maudhui, hadi kuandaa matukio, mpaka kusaidia jumuiya kupitia majukumu ya uongozi. Majukumu haya ya uongozi yamekuzunguka pande zote - wakabidhi, washauri, wasimamizi, na wajumbe wa kamati za kujitolea.
Kila mwaka, kamati kadhaa za harakati hutafuta watu wa kujitolea, kwa kawaida kuanzia Oktoba hadi Desemba.
Soma zaidi kuhusu kamati hizo kwenye kurasa zao za Meta-wiki:
Maombi ya kamati hizo yatafunguliwa tarehe 30 Oktoba 2025. Maombi ya Kamati ya Ushirikiano, Wachunguzi Maalum na Kamati ya Mapitio ya Kesi yatafungwa tarehe 11 Desemba 2025. Saa kadhaa za mazungumzo zitapatikana ili kujadili fursa hizi:
- 5 Novemba 14:00 – 15:00 UTC (muda wa ndani) (jiandikishe)
- 26 Novemba 03:00 – 04:00 UTC (muda wa ndani) (jiandikishe)
Tuma barua pepe cst@wikimedia.org na maswali yoyote ambayo unaweza kuwa nayo au chapisha kwa ukurasa wa majadiliano. Toa mwaliko huu kwa watumiaji wengine ambao unadhani wanaweza kuwa wanastahili na kupenda. Asante!
Kuwasilisha maombi yako
Maombi ya AffCom ni ya umma, unaweza kujaza ombi lako kwa kutumia kiolezo kilichopo hapa.Baada ya kutuma ombi lako, tafadhali tuma barua pepe kwa Timu ya Usaidizi ya Kamati kupitia cst@wikimedia.org kuthibitisha uwasilishaji wako wa maombi. Utapokea maagizo kuhusu hatua zinazofuata utakazohitaji kuchukua, ikijumuisha uthibitishaji wa utambulisho wako. Maombi ya AffCom yatasaliawazi kwa maoni kuanzia wakati wa uwasilishaji wa mtu binafsi hadi tarehe 31 Desemba 2025.
Kama ungependa kuomba kwa Tume ya Wachunguzi Maalum au Kamati ya Mapitio ya Kesi tafadhali tuma maombi kwa kutumia fomu hii. Maombi ya Wachunguzi Maalum na Kamati ya Mapitio ya Kesi hayatachapishwa kwenye Meta-Wiki.
Please note that an account sign up is required in order to submit the form and receive a response about your application. You will be asked for your full name (you can enter your username) and your email address. You can also apply via email (see below).
Wanachama wa kamati zote tatu wanatakiwa kutia sahihi Mkataba wa usiri kwa taarifa zisizo za umma na lazima wawe tayari kutii sera zinazofaa za Shirika la Wikimedia Foundation (kama vile ufikiaji wa sera ya habari zisizo za umma na sera ya faragha ya Shirika na sera ya faragha ya Shirika). Nafasi hizi zinahitaji kiwango cha juu cha busara na uaminifu. Washiriki lazima pia wawe na umri wa zaidi ya miaka 18.
Njia mbadala ya maombi kwa Tume ya Wachunguzi Maalum na Kamati ya Mapitio ya Kesi
Kama fomu hii haifanyi kazi kwako au hutaki kuwasilisha taarifa zako kwa kutumia fomu, tafadhali tuma taarifa zifuatazo kwa barua pepe husika.
OC - ca@wikimedia.org
CRC - legal@wikimedia.org
- Jina lako la mtumiaji na kiungo cha ukurasa wa mtumiaji
- Miradi yako ya msingi
- Lugha unazozungumza/kuandika na kiwango cha ufasaha (tafadhali hakikisha kuwa umejumuisha Kiingereza)
- Uzoefu wowote ulio nao wa kushiriki kwenye kamati, iwe kwa harakati au nje ya harakati.
- Mawazo yako kuhusu ujuzi, uzoefu, au mtazamo gani unaweza kuleta kwa kamati ikiwa utateuliwa.
- Taarifa nyingine yoyote unayofikiri ni muhimu
- Uthibitisho na kujitolea kwako kwa muda na juhudi zinazohitajika kwa kazi ya kamati husika.
- Tume ya Wachunguzi Maalum pekee: Uzoefu wowote ulionao kwa zana za Checkuser au Oversight