Jump to content

Mpango wa Mwaka wa Shirika la Wikimedia Foundation/2025-2026/Maendeleo yaliyofanywa kwenye mpango wa mwaka jana

From Meta, a Wikimedia project coordination wiki
This page is a translated version of the page Wikimedia Foundation Annual Plan/2025-2026/Progress made on last year's plan and the translation is 100% complete.

Shirika hutuma taarifa kila baada ya wiki mbili kuhusu maendeleo dhidi ya mpango wetu wa kila mwaka. Unaweza pia kusoma muhtasari wa miezi sita wa maendeleo kuhusu kilichofanyika dhidi ya mpango wa mwaka jana.

Dondoo ni pamoja na:

Miundombinu

Msaada kwa Wajitoleaji

Lengo hili jipya linajumuisha malengo ya mwaka jana ya "Usalama na Ujumuisho" na "Usawa wa Maarifa."

Ufanisi

  • Kufikia shabaha ya kuwa na mapato kwa njia tofauti kupitia ukuaji katika vyanzo vingi ikiwa ni pamoja na2024 kampeni ya “Big English”.
  • Kuongeza ufanisi wa gharama kwa kukamilisha kuhama kutoka ofisi ya Shirika ya San Francisco hadi kwenye nafasi mpya, ndogo zaidi ya usimamizi, na hivyo kupelekea kuokoa gharama ya kodi ya zaidi ya 80%.
  • Kukuza Biashara ya Wikimedia, kutoka kwa mkataba unaoendelea na wateja wetu wakubwa hadi kuongeza idadi ya wateja wapya (1, 2, 3). Kuwasaidia wateja hawa na vile vile kuongeza ukuaji wa wateja zaidi, tumeongeza vipengele vipya kadhaa kwenye API yetu, ikiwa ni pamoja na marejeo yaliyochanganuliwa, maudhui yaliyopangwa seti za data, na kiwango cha ufikiaji huria kilichoimarishwa.