Jump to content

Wikimedia Foundation elections/2021/2021-08-02/Delay of the 2021 Board of Trustees election/sw

From Meta, a Wikimedia project coordination wiki
Outdated translations are marked like this.

Tunapenda kuwatangazia leo kuhusiana na Uchaguzi wa Bodi ya Wadhamini wa Wikimedia Foundation 2021.Uchaguzi huu ulipangwa kufunguliwa mnamo tar 4 ya mwezi Agosti. Kutokana na sababu mbalimbali za kiufundi zinazohusiana na usalama wa njia iliyopangwa kutumika katika upigaji kura, uchaguzi ni lazima uchelewe kwa muda wa wiki mbili. Hii inamaanisha tunapanga kufungua zoezi la uchaguzi ifikapo tar 18 Agosti 2021, ambapo itakuwa ni siku moja baada ya Mkutano wa Wikimania kuhitimishwa kwa mwaka huu 2021

Kwa taarifa zaidi kuhusiana sababu za kiusalama, unaweza kuona zaidi kwenye Hii tiketi ya Phabricator

Tunaomba radhi sana kwa kucheleweshwa kwa zoezi hili na ni matumaini yetu kuwa tutarejea kufanya zoezi hili mnamo Agosti 18.Tunaendeleza mazungumzo na Kamati ya Uchaguzi na wagombea ili kuratibu hatua zinazofuata.Tutawapa taarifa zaidi kwenye ukurasa wa majadiliano na kundi la Telegram kadri tutakavyojua zaidi.