Chaguzi za Wikimedia Foundation/2022/Maswali yaulizwayo mara kwa mara

From Meta, a Wikimedia project coordination wiki
This page is a translated version of the page Wikimedia Foundation elections/2022/FAQ and the translation is 87% complete.
Outdated translations are marked like this.

Ukurasa huu unalenga kujibu maswali ya mara kwa mara kuhusu uchaguzi wa Baraza la Wadhamini. Sehemu hizo zinajumuisha maswali ya jumla kuhusu Baraza la Wadhamini na Chaguzi za Baraza la Wadhamini.

Ikiwa una swali ambalo huoni likijibiwa kwenye ukurasa huu, tafadhali ongeza swali lako kwenye ukurasa wa majadiliano. Timu ya wawezeshaji wanaounga mkono uchaguzi wa Bodi itaangalia mara kwa mara ukurasa wa majadiliano. Tafadhali kumbuka kuwa baadhi ya maswali yanaweza kutumwa kwenda kwa Kamati ya Uchaguzi kwa majibu. Wawezeshaji watafanya kila linalowezekana kusema nyakati tarajiwa za majibu kutolewa.

Ikiwa swali hili ni la dharura au linahitaji faragha, unaweza kuwasiliana na mwezeshaji moja kwa moja.

Maswali ya jumla kuhusu Bodi

Bodi ya Wadhamini ni nini?

Bodi ya Wadhamini ya Shirika la Wikimedia Foundation inasimamia shughuli za Shirika la Wikimedia. Baraza la Wadhamini linaundwa na wadhamini wa jumuiya na washirika na wadhamini walioteuliwa. Kila mdhamini anahudumu kwa muda wa miaka mitatu. Jumuiya ya Wikimedia inaweza kushiriki katika kuchagua wadhamini wa jumuiya.

Wadhamini wa Bodi ni akina nani?

Wadhamini ni watu kutoka ulimwenguni kote walio na uzoefu mpana. Fuatilia zaidi kuhusu nani yuko kwenye Bodi ya Wadhamini ya Shirika la Wikimedia Foundation.

Ni Wadhamini wangapi watateuliwa katika uchaguzi huu?

Wadhamini wawili watachaguliwa katika uchaguzi huu.

Je, ni sifa zipi za kugombea nafasi ya udhamini?

Hakuna vigezo zaidi ya ustadi wa kujua lugha ya Kiingereza. Baraza la Wadhamini huchapisha ujuzi na vigezo vinavyohitajika kila mwaka wa uchaguzi. Haya si mahitaji bali ni kusaidia jamii kuelewa vyema kile wadhamini wanahitaji ili kuwa Bodi inayofanya kazi vyema. Bodi imeshiriki ujuzi na uzoefu unaohitajika kuwa nao kwa watahiniwa wa mwaka 2022.

Maswali kuhusu Uchaguzi

Je, kuna vigezo vya kustahili kupiga kura?

Ndio vipo. Kamati ya Uchaguzi ndiyo huamua ustahiki wa kupiga kura. Miongozo ya kustahiki imeorodheshwa kwenye ukurasa wa Upigaji Kura wa Jumuiya.

Ninaweza kupiga kura mara ngapi?

Kanuni ni: mtumiaji mmoja, kura moja. Ili kukidhi ustahiki wa kupiga kura kwa mhariri, michango yako itahesabiwa kwenye wiki zote, ikiwa ni wiki yako ya nyumbani au nyingine yoyote.

Ukiamua kubadilisha kura yako, unaweza kufanya hivyo. Hii inaweza kuwa kwa sababu umebadilisha mawazo yako au ikiwa umefanya makosa. Piga kura tena na kura yako ya awali itakatwa.

Wadhamini waliochaguliwa watateuliwa lini?

Uteuzi wa mwisho unatarajiwa kufanyika katika kikao cha Baraza la Wadhamini la Oktoba.

Kamati ya Uchaguzi ni nini na kwa nini wanaamua njia ya upigaji kura?

Kamati ya Uchaguzi inasimamia uchaguzi wa jumuiya kwa Bodi ya Wadhamini ya Shirika la Wikimedia. Kamati ya Uchaguzi na watangulizi wake wamekuwepo tangu 2004. Kamati ya Uchaguzi ina watu wa kujitolea kutoka kwenye jumuiya.

Kamati ya Uchaguzi iliamua mfumo gani wa upigaji kura?

Kamati ya Uchaguzi ilichagua mbinu ya Kura Moja Inayoweza Kuhamishwa. Mfumo huu wa upigaji kura unawaruhusu wapiga kura kupanga wagombea badala ya kumpigia kura mgombea mmoja tu. Jaribu mfano huu wa kupendeza aina ya chakula. Je, unaweza kupanga vipi upendeleo wa vyakula unavyovipenda? Labda kama hivi:

  1. Chokoleti
  2. Vitafunwa
  3. Keki

Badala ya kupigia kura chokoleti pekee, unaweza kupanga aina zako za chakula kwa mpangilio wa upendeleo. Iwapo watu wengi watapigia kura chakula kingine, kura yako inaweza kuhamishiwa kwenda kwenye aina nyingine ya chakula. Kwa Kura Moja Inayoweza Kuhamishwa, mapendeleo yako yatazingatiwa hata kama wagombea ambao ni chaguo lako bora hawajachaguliwa.

Napenda utawala! Je, ninawezaje kushiriki zaidi katika Chaguzi za Bodi?

Hilo ni swali zuri! Kadiri wanajamii wengi wanavyoshiriki katika uchaguzi, ndivyo mchakato unavyokuwa bora zaidi. Wanajamii wanaweza kuwa mgombea au wakajiunga na Kamati ya Uchaguzi. Ikiwa hilo si pendeleo lako, njia nyingine nzuri ya kushiriki ni kwa kushiriki kama mjitoleaji wa Uchaguzi.

Wajitoleaji wa Uchaguzi huwa viunganishi kati ya Kamati ya Uchaguzi, timu ya uwezeshaji inayounga mkono uchaguzi wa Bodi, na jumuiya kwa upana wake. Huwawezesha wanajamii kushiriki katika uchaguzi na kuchangia katika kuunda harakati.