Uchaguzi wa Shirika la Wikimedia Foundation/2025/Tangazo/Tangazo la Uchaguzi
Uchaguzi wa Bodi ya Wadhamini ya Wikimedia Foundation mwaka 2025 na Wito wa Maswali
Wapendwa wote,
Mwaka huu, Muda wa Wadhamini 2 (wawili) waliochaguliwa na jumuiya na Washirika kwenye Bodi ya Wadhamini ya Shirika la Wikimedia Foundation utakamilika [1]. Bodi inakaribisha harakati nzima kushiriki katika mchakato wa uteuzi wa mwaka huu na kupiga kura kujaza viti hivyo.
Kamati ya Uchaguzi inasimamia mchakato huu kwa msaada kutoka kwa wafanyakazi wa Shirika [2]. Kamati ya Utawala inayoundwa na wadhamini ambao si wagombea katika mchakato wa uteuzi wa wadhamini waliochaguliwa na jumuiya na washirika wa mwaka 2025 (Raju Narisetti, Shani Evenstein Sigalov, Lorenzo Losa, Kathy Collins, Victoria Doronina na Esra’a Al Shafei) [3], ina jukumu la kutoa usimamizi wa Bodi ya wadhamini kwa ajili ya kuweka taarifa kwa Bodi ya wadhamini. Maelezo zaidi kuhusu majukumu ya Kamati ya Uchaguzi, Bodi, na wafanyakazi yako hapa [4].
Hapa kuna tarehe kuu zilizopangwa:
- Mei 22 – Juni 5: Tangazo (mawasiliano hayo) na mwito wa kipindi cha maswali
- Juni 17 – Julai 1, 2025: Wito wa wagombea
- Julai 2025: Ikihitajika, washirika hupigia kura wagombea waliopo kwenye orodha fupi ikiwa 10 au zaidi wataomba [5]
- Agosti 2025: Kipindi cha kampeni
- Agosti – Septemba 2025: Kipindi cha wiki mbili cha kupiga kura kwa jumuiya
- Oktoba – Novemba 2025: Ukaguzi wa usuli wa watahiniwa waliochaguliwa
- Mkutano wa Bodi mnamo Decemba 2025: Wadhamini wapya wamekaa kwenye kiti
Jifunze zaidi kuhusu uchaguzi wa 2025 - ikiwa ni pamoja na ratiba ya kina ya matukio, mchakato wa kugombea, sheria za kampeni na vigezo vya kustahiki kwa mpiga kura - kwenye ukurasa huu wa Meta-wiki [kiungo].
Wito wa Maswali
Katika kila mchakato wa uchaguzi, jumuiya ina fursa ya kuwasilisha maswali kwa wagombea wa Bodi ya Wadhamini kujibu. Kamati ya Uchaguzi huchagua maswali kutoka kwenye orodha iliyoandaliwa na jumuiya ili wagombea wajibu. Wagombea lazima wajibu maswali yote yanayohitajika katika maombi ili kustahiki; vinginevyo maombi yao yatakataliwa. Mwaka huu, Kamati ya Uchaguzi itachagua maswali 5 kwa wagombea kujibu. Maswali yaliyochaguliwa yanaweza kuwa mchanganyiko wa yale yaliyowasilishwa kutoka kwa jumuiya, ikiwa yanafanana au yanahusiana. [kiungo]
Watu wa kujitolea katika uchaguzi
Njia nyingine ya kuhusika katika mchakato wa uchaguzi wa mwaka 2025 ni kuwa Mtu wa Kujitolea katika Uchaguzi. Watu wa Kujitolea katika Uchaguzi ni daraja kati ya Kamati ya Uchaguzi na jumuiya zao. Wanasaidia kuhakikisha jumuiya inawakilishwa na kuwahamasisha kupiga kura. Jifunze zaidi kuhusu mpango na jinsi ya kujiunga kwenye ukurasa huu wa Meta-wiki [kiungo].
Asante!
[1] https://meta.wikimedia.org/wiki/Wikimedia_Foundation_elections/2022/Results
[2] https://foundation.wikimedia.org/wiki/Committee:Elections_Committee_Charter
[3] https://foundation.wikimedia.org/wiki/Resolution:Committee_Membership,_December_2024
[4] https://meta.wikimedia.org/wiki/Wikimedia_Foundation_elections_committee/Roles
[5] https://meta.wikimedia.org/wiki/Wikimedia_Foundation_elections/2025/FAQ
[6] https://meta.wikimedia.org/wiki/Wikimedia_Foundation_elections/2025/Questions_for_candidates
Salamu sana,
Victoria Doronina
Uhusiano wa Bodi na Kamati ya Uchaguzi
Kamati ya Utawala
