Uchaguzi wa Shirika la Wikimedia Foundation/2025/Wagombea/Lane Rasberry
Lane Rasberry (bluerasberry)
bluerasberry (talk • meta edits • global user summary • CA • AE)
| Candidate details |
| |
|---|---|---|
| Candidate video statement | ||
| Jumla ya hesabu ya maneno kwa maombi yote (yanayohitajika + maswali ya hiari) ni maneno 2500. | ||
| Je, umesoma mahitaji ya chini ya mgombea na kuthibitisha kuwa unakidhi sifa za chini kabisa na sifa zinazohitajika kwa mgombea? | Yes | |
| Je, umesoma miongozo ya mgombea na kukubali kutii miongozo? | Yes | |
| Maswali yanayohitajika | ||
| ||
| Kwa nini unagombea Bodi ya Wadhamini ya Shirika la Wikimedia Foundation? Ungechangia nini? Je, ungependa kujifunza zaidi kuhusu nini? | Wikipedia ndiyo jukwaa pekee la mtandao ambapo jumuiya ya watumiaji husimamia thamani, maadili, bajeti na kila kitu. Huu ni uchaguzi muhimu zaidi kwenye Mtandao, na kura yako ina athari kiulimwengu na yenye kubadilisha historia! Kama mdhamini, nitaendelea kuambia vyombo vya habari na ulimwengu kwamba Shirika la Wikimedia Foundation hulinda, hufunza, na kuunga mkono wapigakura kama wewe ili kutawala na kudhibiti Wikipedia.
Haya ndiyo maoni yangu:
| |
| Tafadhali eleza uzoefu wako na Wikimedia (kama vile michango kwa miradi ya Wikimedia, uanachama katika mashirika au washirika wa Wikimedia, shughuli kama mratibu wa harakati za Wikimedia, au kushiriki na shirika mshirika la Wikimedia). | Nina ushiriki wa juu zaidi wa Wikimedia.
Wahariri wengi wa Wikipedia kamwe hawajiungi na vikundi na hiyo ni sawa, lakini kwangu, napenda vikundi. Nimekuwa hai kwa miaka 10 na zaidi katika Wikimedia New York City, Cascadia Wikimedians, na Wikimedia Bangladesh. Nimeandaa miaka 100 ya mikutano ya Wikimedia NYC, nimeandaa mikutano ikijumuisha Queering Wikipedia na WikiConference North America, na ni mwanzilishi mwenza na bado nipo hai katika Wikimedia LGBT+ na Wikimedia Medicine Uzoefu wangu ni kwamba tunafanya maendeleo haraka wakati vikundi vinapotamani kushirikiana. Nina Hariri 50k kwa Wikipedia, 10k kwa Commons, na 100k kwa Wikidata. Nimetoa mamia ya Mazungumzo na mahojiano ya Wikipedia kwa vyombo vya habari na mikutano. Mimi ni mhariri wa gazeti la Wikipedia la Kiingereza, Signpost. | |
| Kwa mtazamo wako, Shirika la Wikimedia Foundation linapaswa kutoa kipaumbele kwa kitu gani katika miaka 3-5 ijayo, na kwa nini unaona haya kama vipaumbele muhimu zaidi? | Kipaumbele muhimu zaidi ni kuweza kuandaa mazungumzo muhimu kati ya jumuiya ya mtandaoni na Shirika la Wikimedia Foundation kuhusu mada ngumu. Kwa matatizo tunayokabiliana nayo, suluhu ni kwamba Shirika la Wikimedia Foundation na jumuiya ya watumiaji wa Wikimedia wanahitaji mazungumzo bora na kuaminiana kati yao.
Tunakabiliwa na changamoto za kutisha ambazo zinatishia uwepo wa Wikipedia. Kwa mfano, serikali ya Marekani inawatesa wahariri na kutishia kuondoa hadhi ya kisheria ya Wikipedia. Tuna vitisho vikali kutoka kwa serikali zingine, ujio wa Akili Mnemba, na mataifa fulani ya wahariri wa Wikipedia kuachwa nje ya maamuzi. Tunahitaji kuzungumza baina yetu, kuwafunza watu wanaojitolea kikanda kuzungumza na vyombo vya habari, na pia kupata watafiti, wanahabari, na wabia wengine wa kushirikiana wasio wa faida kuzungumza nasi kuhusu changamoto. Jambo bora zaidi ambalo linaweza kutokea kwa Harakati za Wikimedia ni kwa Shirika la Wikimedia Foundation na jumuiya ya watumiaji ku 💙 kila mmoja. | |
| Tafadhali eleza uzoefu wako na mabaraza ya usimamizi wa mashirika (yasiyo ya faida au ya faida), ukitaja upeo wa majukumu yako, pamoja na uchangamani wa shirika (kulingana na ukubwa wa shughuli, bajeti, idadi ya watu wanaohusika, au hatua nyingine muhimu) na ukubwa wa bodi au baraza. | Tangu 2018 nimekuwa mpelelezi mkuu kwa utafiti wa Wikipedia katika Shule ya Sayansi ya Data katika Chuo Kikuu cha Virginia. Ninapata ushauri wa kitaalamu kutoka kwa kitivo cha chuo kikuu na usaidizi wa utafiti wa wanafunzi katika sera za umma, uhasibu, sayansi ya kompyuta, idara yangu ya nyumbani, na kila mahali. Kama mdhamini, rasilimali hizi za chuo kikuu zitasaidia kazi yangu ya bodi na kunisaidia kuwasiliana kwa ufanisi zaidi na bodi, vyombo vya habari na watumiaji wa mtandaoni.
Kwa miaka 6 nilisimamia programu ya Wikipedia katika Ripoti za Watumiaji, ambayo ni shirika la watumiaji nchini Marekani. Tuliboresha makala za Wikipedia kwa ajili ya usalama wa matibabu. Tangu 2007 nimehudumu katika bodi ya maadili ya utafiti wa somo la binadamu kuhusu |chanjo za VVU/UKIMWI katika Mtandao wa Majaribio ya Chanjo ya VVU. Utafiti ni wa kiulimwengu, na upeo wangu ni kutetea ufikiaji wa maelezo ya mtandaoni. Niko katika bodi ya chama cha wafanyakazi wa chuo kikuu katika eneo langu, na ninashirikiana na Wafanyikazi wa Mawasiliano wa Amerika. Majukumu haya yote yananihusisha mimi kusimamia miradi, bajeti na mikakati. | |
| Maswali kutoka kwa Jumuiya (lazima) | ||
| Maswali haya yaliyotokana na jumuiya. Maswali haya yanahitajika ili kuzingatia ombi lako kuwa kamili. Ikiwa sehemu hii haijakamilika kabla ya 23:59 Popote Duniani, Julai 8 (11:59 UTC, Julai 9), ombi lako halitazingatiwa. | ||
| Je, unapangaje kuhakikisha uwazi na uwajibikaji katika michakato yako ya kufanya maamuzi kama mjumbe wa Bodi ya Wadhamini? | Ninatoa mahojiano kwa vyombo vya habari, ninachapisha video kwenye YouTube, Nina chapisha kama mtafiti, Ninaandikia gazeti la Signpost, na kufanya lolote niwezalo kupata usikivu. Nitahakikisha uwazi na uwajibikaji kwa kufanya kile ninachofanya kila wakati, ambacho ni kuzungumza mtandaoni.
Nilianzisha mradi wa Right to Information kwenye Meta-Wiki kwa sababu miaka iliyopita, nilitaka taarifa, na sikuweza kupata njia ya kuwasiliana na Shirika. Kama mdhamini, ninahimiza jumuiya ya watumiaji kujipanga ili kuniomba taarifa ya umma. | |
| Je, ni suala gani jipya la kwanza ambalo ungependa kuleta kwa Bodi ili lijadiliwe kwa umakini, na utalishughulikia vipi? | Ninataka kufikia kumbukumbu za fedha za Shirika la Wikimedia Foundation ili niweze kuzichanganua katika chuo kikuu changu, au vinginevyo, WMF inaweza kusema tu moja kwa moja kuwa haitaki kutoa taarifa hii. Hivi sasa ripoti za fedha za WMF hazieleweki kwa jumuiya ya watumiaji. Tunahitaji uwazi katika ripoti hizo ili Wana Wanawikimedia katika kila nchi waweze kujua ni pesa gani Shirika linatumia kwa niaba yao, na mkakati wa maendeleo wa nchi hiyo ni upi.
Ripoti ya hivi karibuni sana yinasema kwamba 34% ya pesa ni "msaada kwa watu wanaojitolea", lakini zaidi ya uchaguzi huu wa wadhamini, watu wanaojitolea hawana usemi wa kutosha katika kuangalia jinsi pesa zinavyotumika na chaguzi chache za kuangalia jinsi pesa zinavyotumika. Jumuiya zetu nyingi za watumiaji hufanya programu kulingana na nchi au lugha, kwa hivyo ikiwa Shirika la Wikimedia Foundation ungekuwa wazi zaidi kuhusu matumizi yake ya kikanda, basi ingekuwa rahisi kwa jumuiya kupanga mikakati yao wenyewe, kuajiri wanafunzi wa uhasibu na biashara kama washauri, kutoa maoni kuhusu bajeti zao wenyewe, na kupanga maelekezo yao ya baadaye bila kuhitaji kuwasiliana na mtu wa utamaduni mwingine katika Shirika la Wikimedia Foundation. Jumuiya ya Wikimedia inataka uhuru na uwezo wake wa kupanga mustakabali wake wenyewe wakijua rasilimali walizonazo. Ukosefu wa taarifa ni tatizo zaidi kuliko kuwa waaminifu kwamba tuna rasilimali chache. | |
| Ni namna gani uamuzi kuhusu mbadala na upendeleo katika maeneo ya teknolojia au bidhaa uangaliwe | Sababu ya sisi kuwaruhusu watumiaji kuwapigia kura wadhamini ni ili watumiaji wawe na uwezo katika mchakato huu wa kufanya maamuzi. Kwa hivyo, uamuzi moja muhimu ni kuongeza ushiriki wa jamii dhidi ya kuwaachia wataalam maamuzi fulani.
Kuna vipengele vingi vya jukwaa la Wikimedia ambavyo hufanya kazi vizuri bila ushiriki mkubwa wa jamii. Mnamo Mei 2025, Wikidata ilikuwa na mgawanyiko wa grafu kwa ajili ya WikiCite, na ilihitaji kufanya maamuzi ya kitaalamu kwa kanzidata. Mamia ya watumiaji walioathiriwa wanaofanya miradi ya sayansi wazi walitaka Wikidata ifanye kazi, lakini hawakuhitaji kujifunza muundo wa kanzidata. Nilielezea suala la kiufundi vile nilivyoweza, na kwa kujibu, wafanyakazi wa Wikimedia Foundation walinipa masasisho ya kusaidia uundaji wa hati za jumuiya. Uzoefu huu unaonyesha kwamba wakati masasisho ya teknolojia yanatatiza uhariri wa watumiaji, basi wastawishaji programu wa Wikimedia wanaotoa taarifa hupata usaidizi wa jumuiya. Mchakato mwingine ambao hufanya kazi vyema na maelfu ya washiriki wa jumuiya ni Community Wishlist, ambapo mtu yeyote anaweza kuomba kipengele kwa ajili ya wafanyakazi kuendeleza na wengine kupiga kura ili kukiunga mkono. Suluhu mara nyingi ni kuwa na mazungumzo ya kujenga na kudumisha uaminifu. | |
| Idadi ya washirika wa Wikimedia imeongezeka kwa kiasi kikubwa katika miaka michache iliyopita, lakini kuhakikisha kuwa kuna rasilimali za kutosha kunaweza kuwa changamoto. Kwa kuzingatia hili, tunawezaje kufikiria upya mfumo wa ikolojia wa harakati, ikijumuisha jinsi washirika wanavyotathminiwa, shirikishwa, na kufadhiliwa? | Hatujawahi kuwa na mchakato wa kutathmini athari za mashirika ya jumuiya ya Wikimedia. Washirika huandika ripoti za mwaka na kuonyesha vipimo, lakini Shirika la Wikimedia Foundation halina wafanyakazi wanaoonyesha matumizi ya ripoti hizi. Ninashukuru juhudi za kufupisha mchakato wa kuripoti mwaka 2024, lakini bado wanajamii hutumia maelfu ya saa kwa mwaka kuandika ripoti za wanachofanya. Ikiwa tutaomba ripoti, basi tunahitaji kuziheshimu kwa kuzichambua. Kuna suluhu rahisi: kabla ya Shirika la Wikimedia Fondation kuuliza jumuiya chochote, kuna haja ya kuwa na makadirio ya umma ya saa ngapi za kujitolea zinaombwa. Mara nyingi, Shirika la Wikimedia Foundation hutaka muda kidogo tu wa jumuiya, lakini huuliza swali kimakosa kwa njia ambayo husukuma watu 1000 wa kujitolea kwa kila mmoja kuchangia saa za kazi. Umakini wa jamii ni rasilimali adimu. Tunapaswa kuomba tu wakati ikiwa tuna mpango wa kuutumia, na tunapaswa kupima na kuripoti muda unaotumiwa kwa watu wakujitolea kwa ajili ya kuwashukuru vyema kwa kushiriki. | |
| Afisa Mtendaji Mkuu wa Shirika Wikimedia Foundation (CEO) anapobadilika, ni sifa zipi unaamini kuwa kiongozi anayekuja anapaswa kuwa nazo, na je, hizi zinaweza kuchangia vipi katika kuendeleza harakati za Wikimedia? | Natamani Afisa Mtendaji Mkuu angekuwa mwangalifu kusema mambo mazuri tu kuhusu jumuiya yetu ya watumiaji.
Mnamo 2015, Niliandika insha kuhusu jinsi wafanyakazi na uongozi wa Shirika la Wikimedia Foundation wakati mwingine hukosoa jumuiya ya watumiaji wa Wikipedia. Mara kwa mara mimi huwasilisha programu za Wikipedia kwenye hafla na mikutano ya umma, na najua kutokana na uzoefu kwamba wageni ambao hawahariri Wikipedia watanikaribia kusema kwamba Wikipedia ina upendeleo dhidi ya wanawake na walio wachache. Wanapata wazo hili kutoka kwa Kampeni za mawasiliano za Shirika la Wikimedia Fondation ambazo huchukua sauti mbaya huku wakiwa hawasherehekei mafanikio yetu. Ninatambua kuwa tuna mapungufu makubwa ya utofauti, lakini wakati huo huo, ni kweli pia kwamba Wikipedia ina mkusanyiko mkubwa zaidi ulimwenguni, wa kina zaidi, ulioangaliwa ukweli, wa aina mbalimbali ya wasifu na makala za mada za kitamaduni kwa makundi mengi ya wachache. Wikipedia ina upendeleo, lakini kila kitu kingine ni mbaya zaidi. Shirika la Wikimedia Fondation linapaswa kuwasiliana kwa uwazi kwamba jumuiya yetu ya watumiaji inaunda chanzo cha habari kisichopendelea zaidi, mchakato bora wa ustaarabu unaofanya kazi, na jumuiya pekee ya watumiaji ambayo ina utawala wa watumiaji. Majadiliano yangekuwa rahisi ikiwa tungeona chanya na kuitikia kwa njia ya kujenga, badala ya kuona hasi na kukosoa kile tulicho nacho. | |
| Maswali ya hiari - Uzoefu wa Weledi, Ujuzi na Elimu | ||
| Maswali haya ni ya hiari. Majibu yatakuwa sehemu ya kikomo cha jumla ya maneno kwenye ombi lako. (Kumbusho: Hutakuwa na fursa nyingine za kutoa taarifa hii). | ||
| Tafadhali eleza uzoefu wako wa kitaaluma na uhusiano wake kwa kazi ya bodi. | I study artificial intelligence as Wikimedian in Residence at the School of Data Science. I already mentor student researchers, and as trustee, I would collaborate with students from all disciplines to assist me with board work. I would send students into Wikipedia to help me analyze, report, and uplift, and deliver Wikipedia community conversations and decisions to researchers, media, and public policy discussions.
I was Wikimedian in Residence at Consumer Reports from 2012-18, and before that I did clinical research through which I also did medical Wikipedia editing. In all these things I did project management, budgeting, and strategy. | |
| Tafadhali eleza jinsi ulivyoshughulikia, au kuwashauri wengine kuhusu, tatizo tata katika shirika. Ulifanyaje kazi na wengine kushughulikia hali hiyo? Ni mabadiliko gani yaliyotokana na juhudi zako? | At my school I helped to develop our open access guidelines. It is a common wish for Wikimedians that universities, museums, and organizations would adopt open source practices and implement them. Organizations worry about losing control of their media, but demonstrating the reach and popularity of Wikipedia is a great argument to convince organizations to freely share their knowledge online. | |
| Tafadhali eleza historia yako ya elimu, ikijumuisha shahada, cheti, na kozi za masomo ulizomaliza, na uhusiano wake kwa kazi ya bodi. | I studied chemistry and am a research professional at a university. I do things the university way and not the way of a corporation, NGO, or government. | |
| Tafadhali ongeza viungo husika vinavyoelezea historia yako ya kitaaluma, uzoefu, wasifu (kama vile LinkedIn, ukurasa wa wafanyakazi, n.k.). | -
| |
| Maswali ya hiari - Uzoefu wa Uongozi | ||
| Maswali haya ni ya hiari. Majibu yatakuwa sehemu ya kikomo cha jumla ya maneno kwenye ombi lako. (Kumbusho: Hutakuwa na fursa nyingine za kutoa taarifa hii). | ||
| Tafadhali eleza njia ambazo umesaidia kuunda daraja kati ya jumuiya nyingi (kama vile kwa kufanya kazi kwenye miradi nje ya wiki yako ya nyumbani, au kufanyia kazi ushirikiano kati ya washirika wengi). | To form bridges, people have to become friends by socializing repeatedly over time. An amazing part of Wikipedia that feels amazing is continually having positive interactions with other users by collaborating on projects. Bridges are the result of friendly collaboration on Wikimedia projects.
As described above, I have hosted 100s of Wikimedia events. Away from Wikipedia, I operated a queer punk rock house concert venue which presented 100 bands and indexed them in Wikidata. | |
| Je, unaweza kuelezea sera, kwenye wiki au nje ya wiki, ambayo ulisaidia kuunda au kubadilisha? Umejifunza nini kutokana na uzoefu huu? | There is no need to turn a conversation into a conflict. We are Wikipedia and we can present all sides in our disagreements just like we do in encyclopedia articles.
There have been times when 1000 volunteer users signed petitions, but not a single WMF staff person publicly joined the conversation. Surely there must be at least one staff person who wished to sign, but felt afraid to do so. Humans define Wikipedia's values and ethics, and when the user community is having deep conversations on major issues, then WMF staff need to feel safe to join those discussions. I was active in organizing community demonstrations including for Superprotect, the removal of the CEO, the rebranding, fundraising messages, and others. These are major wiki demonstrations with many petitioners. The lesson to learn is that we have to listen to all sides, collaborate, and edit the story together. | |
| Je, umewezaje kuwawezesha watu kutoa sauti zao zisikike? | I lived in the small rural town of West Orange, Texas from birth to age 18. Because I had problems for being gay, I moved to Seattle not knowing anyone there just because it was a big city far away. I did not have money so I lived for years in a building with no water or electricity. I experienced how society exploits vulnerable people.
I am more fortunate now, but because of my personal experience, I find other Wikipedia editors from fringe backgrounds. Wikipedia has editors who are homeless, unemployed, disabled, in poverty, in drug abuse, doing sex work, serving as caretakers for others, displaced or immigrant, but who still edit Wikipedia because they believe in sharing information. Editing Wikipedia is a pleasurable productive activity to all kinds of people. I try to make Wikipedia more accessible to the scared young person I used to be. | |
| Je, unaweza kueleza jinsi ambavyo umeonyesha uwezo wa kuwaongoza wengine katika kutatua matatizo, kukabiliana na mabadiliko au kufikia malengo, hasa katika ngazi ya uongozi au usimamizi? | Management in Wikimedia projects means finding ways to consistently convert the money from Wikipedia donations into the impact that we decide is most meaningful. I recommend that Wikimedia community organizations ask questions like, "How much money does it cost to recruit a new editor?", "What is the worth of a Wikipedia article which is read 5000 times monthly?", or "What museums will sponsor Wikipedia programs if we develop GLAM tools?"
The leaders of a program should publish brief fantasy best case scenarios for their programs, and more realistic probable outcomes. After a project, compare the predictions to the outcome. Doing these exercises will confirm that the development team and community have a shared dream of a good outcome. For anyone applying for grants to the Wikimedia Foundation or for anyone making Wikipedia products, make these predictions before you begin. | |
| Maswali ya hiari - Mawazo ya kimkakati | ||
| Maswali haya ni ya hiari. Majibu yatakuwa sehemu ya kikomo cha jumla ya maneno kwenye ombi lako. (Kumbusho: Hutakuwa na fursa nyingine za kutoa taarifa hii). | ||
| Tafadhali eleza uzoefu wako wa kushiriki au kuongoza shirika katika kupanga mustakabali wake. Je, kazi yako ilichangia vipi katika kuchagua njia sahihi ya shirika? | At the start of any project, write a draft of your final report so that you have a clear idea of how success should look. The right path is the one that leads to the dream that everyone wrote at the start of the project. | |
| Verification | Identity verification performed by Wikimedia Foundation staff and eligibility verification performed by the Elections Committee | |
| Eligibility: |
Identification: Verified by: – NahidSultan (WMF) (talk) 04:57, 16 July 2025 (UTC) | |
