Jump to content

Uchaguzi wa Shirika la Wikimedia Foundation/2025/Mchakato wa kuorodhesha orodha fupi

From Meta, a Wikimedia project coordination wiki
This page is a translated version of the page Wikimedia Foundation elections/2025/Shortlisting process and the translation is 94% complete.

Katika uchaguzi wa 2025, kutakuwa na viti viwili vya wazi. Kamati ya Uchaguzi na Bodi ya Wadhamini iliamua kwamba wagombea 10 wangekuwa idadi inayofaa kwa wapigakura kupitia. Iwapo kuna zaidi ya wagombea 10 wanaostahiki kama ilivyoamuliwa na Kamati ya Uchaguzi, mchakato wa kuorodhesha utafanyika. Mchakato huo utalenga kuorodhesha wagombea 6, na wagombea hawa 6 watashiriki katika awamu ya upigaji kura ya jumuiya. Ikiwa kuna wagombea 10 au wachache, hakutakuwa na mchakato wa kuorodhesha.

Itifaki ya orodha fupi

Ikiwa kuna mchakato wa kuorodhesha, mchakato ufuatao utafuatwa:

  • Kila mshirika ataombwa kuteua mwakilishi 1 (mmoja) ambaye atawawakilisha katika mchakato wa kuorodhesha. Mwakilishi anaweza kuwa mtu wa kwanza kuwasiliana kwa Mshirika huyo au mtu mwingine yeyote anayefanya kazi katika nafasi rasmi akiwamwakilisha Mshirika. Timu ya usaidizi itatuma ujumbe kwa Washirika wote kuwauliza wataje mwakilishi wao.
  • Wawakilishi wa Washirika watachagua hadi 6 (sita) kutoka kwa wagombea wote watakaobainishwa kuwa wanastahili na Kamati ya Uchaguzi katika jukwaa la kupigia kura lililoteuliwa na Kamati ya Uchaguzi. Uamuzi wao unapaswa kutegemea upatanishi wa wagombea na mahitaji ya Bodi na vigezo vinavyohitajika kwa wagombea.

Kamati ya Uchaguzi itatuma kiungo cha uchunguzi kupitia barua pepe kwa mwakilishi aliyetambuliwa kwa 15 Julai 2025. Mchakato wa kuorodhesha utaanza 15 Julai 2025 saa 00:01 UTC hadi 28 Julai 2025 saa 23:59 UTC.

Uchunguzi utauliza maswali yafuatayo:

  • Jina au jina la mtumiaji la mwakilishi
  • Tafadhali chagua hadi wagombea 6 ambao Mshirika wako aliamua kuwa wanapatana zaidi na mahitaji ya Bodi na vigezo vinavyohitajika.
    • Kumbuka: kutakuwa na orodha ya wagombea wote wanaostahiki, na mwakilishi mshirika ataweza kuchagua idadi ya mwisho ya wagombea 6; wagombea hawa hawajaorodheshwa
  • Tafadhali toa hati kuhusu mchakato wa kufanya maamuzi wa mshirika ili kufikia uchaguzi huu
  • Maoni (ikiwa kuna kitu kingine chochote ambacho hakijashughulikiwa na fomu hii)

Matokeo ya mchakato wa kuorodhesha yatatangazwa kwa njia iliyofafanuliwa hapa chini, ili kuweka usawa wa wajibu kwa uwazi wa umma na kuzingatia kuhusu ushawishi usiofaa wa kura ya jumuiya:

  • Baada ya mchakato wa kuorodhesha kukamilika, wagombea 6 watakaopata idadi kubwa zaidi ya kura watatangazwa na Kamati ya Uchaguzi, lakini bila kutaja hadharani nafasi zao.
  • Baada ya jumuiya kupiga kura, data kuhusu idadi ya Washirika walioshiriki katika mchakato wa kuorodhesha na ni wagombea gani waliowapigia kura itatolewa hadharani.

Shortlisted candidates

The shortlisting process concluded on 28 July 2025. These candidates proceeded to the candidate review process: