Jump to content

Uchaguzi wa Shirika la Wikimedia Foundation/2025/Miongozo ya ustahiki wa wapiga kura

From Meta, a Wikimedia project coordination wiki
This page is a translated version of the page Wikimedia Foundation elections/2025/Voter eligibility guidelines and the translation is 98% complete.
Outdated translations are marked like this.

Wahariri

Unaweza kupiga kura kutoka kwa akaunti yoyote iliyosajiliwa unayomiliki kwenye Wikimedia wiki. Unaweza kupiga kura mara moja pekee, bila kujali unamiliki akaunti ngapi. Ili kuruhusiwa, akaunti hii moja lazima:

  • haijazuiwa kwa sasa duniani kote;
  • kutozuiliwa kabisa katika zaidi ya mradi mmoja wa umma;
  • haijafungwa kwa sasa;
  • isiwe roboti;
  • wamefanya angalau hariri 300 kabla ya [TAREHE YA MWISHO - siku 30 kabla ya siku ya kwanza ya kupiga kura] kote katika Wikimedia; na
  • wamefanya angalau mabadiliko 20 kati ya [TAREHE YA KUANZA - miezi 12 kabla ya siku ya kwanza ya kupiga kura] na [TAREHE YA MWISHO - siku 30 kabla ya siku ya kwanza ya kupiga kura]

Zana ya AccountEligibility inaweza kutumika kuthibitisha kwa haraka ustahiki msingi wa kupiga kura wa mhariri.

Wastawishaji

Wastawishaji wanaruhusiwa kupiga kura ikiwa:

  • ni wasimamizi wa seva za Wikimedia walio na ufikiaji wa shell; au
  • Wamefanya walau badiliko moja la muuganiko kwa hazina zozote za Wikimedia kwenye Gerrit, kati ya [TAREHE YA KUANZA - miezi 12 kabla ya siku ya kwanza ya kupiga kura] na [TAREHE YA KUMALIZA - siku 30 kabla ya siku ya kwanza ya kupiga kura].

Vigezo vya ziada

Wastawishaji wanaweza kuruhusiwa kupiga kura ikiwa:

  • Wamefanya walau badiliko moja la muuganiko kwa hazina yoyote ya Wikimedia kwenye nonwmf-extensions au nonwmf-skins, kati ya [TAREHE YA KUANZA - miezi 12 kabla ya siku ya kwanza ya kupiga kura] na [TAREHE YA KUMALIZA - siku 30 kabla ya siku ya kwanza ya kupiga kura]; au
  • Wamefanya walau badiliko moja la muuganiko kwa hazina yoyote ya zana za Wikimedia (kwa mfano, magnustools) kati ya [TAREHE YA KUANZA - miezi 12 kabla ya siku ya kwanza ya kupiga kura] na [TAREHE YA KUMALIZA - siku 30 kabla ya siku ya kwanza ya kupiga kura]; au
  • ni watunzaji/wachangiaji wa zana, roboti, vifaa na moduli zozote za Lua kwenye wiki za Wikimedia; au
  • wamejihusisha kwa kiasi kikubwa katika kubuni na/au kupitia michakato ya maendeleo ya kiufundi inayohusiana na Wikimedia.

Wafasiri

Wafasiri wanaruhusiwa kupiga kura ikiwa wamefanya angalau hariri 300 kabla ya [TAREHE], na hariri 20 kati ya [TAREHE YA KUANZA - miezi 12 kabla ya siku ya kwanza ya kupiga kura] na [TAREHE YA MWISHO - siku 30 kabla ya siku ya kwanza ya kupiga kura], kwenye translatewiki.net.

Wafanyakazi na wakandarasi wa Wikimedia Foundation

Wafanyakazi wa sasa wa Shirika la Wikimedia Foundation na wakandarasi wanaruhusiwa kupiga kura ikiwa wameajiriwa na Shirika kufikia [TAREHE YA MWISHO - siku 30 kabla ya siku ya kwanza ya kupiga kura].

Wafanyakazi na wakandarasi wa washirika wa Wikimedia

  • Tawi la sasa la Wikimedia, shirika la mada au wafanyakazi wa kikundi cha watumiaji na wanakandarasi wanaruhusiwa kupiga kura ikiwa wameajiriwa na shirika lao kuanzia [TAREHE YA MWISHO - siku 30 kabla ya siku ya kwanza ya kupiga kura].
  • Wanachama wa mashirika rasmi kama ilivyofafanuliwa katika sheria ndogo za Matawi ya sasa ya Wikimedia, mashirika ya mada au vikundi vya watumiaji wanaruhusiwa kupiga kura ikiwa wamekuwa wakihudumu katika shughuli hizo kuanzia [TAREHE YA MWISHO - siku 30 kabla ya siku ya kwanza ya kupiga kura].

Watu wanaoomba kupiga kura chini ya aina hii lazima wajumuishe uthibitisho kutoka kwa washirika wao. Mshirika wao lazima achukuliwe "ikibali" na mahitaji yao ya kuripoti. Kamati ya Ushirikiano na Kamati ya Uchaguzi itathibitisha orodha ya Washirika wanaostahiki wa Wikimedia kabla ya [TAREHE YA MWISHO - siku 30 kabla ya siku ya kwanza ya kupiga kura].

Wajumbe wa bodi ya Wikimedia Foundation na wajumbe wa bodi ya ushauri

Wanachama wa sasa na wa zamani wa Bodi ya Wadhamini ya Wikimedia Foundation na Bodi ya Ushauri ya Wikimedia Foundation wanaruhusiwa kupiga kura.

Wanakamati wa harakati za Wikimedia

Wanachama wa sasa wa kamati za harakati za Wikimedia wanaruhusiwa kupiga kura ikiwa wamekuwa wakihudumu katika shughuli hizo kuanzia [TAREHE YA MWISHO - siku 30 kabla ya siku ya kwanza ya kupiga kura].

Kwa madhumuni ya mwongozo huu, kamati za harakati za Wikimedia zinafafanuliwa kama Kamati ya Mawasiliano, Kamati ya Uchaguzi, Kamati ya Lugha, Baraza la Ushauri la Bidhaa na Teknolojia, Kamati ya Kimataifa ya Usambazaji wa Rasilimali, na Kamati ya Kuratibu Mwongozo wa Kimataifa wa Mwenendo na Maadili.

Waandaaji wa jumuiya za harakati za Wikimedia

Waandalizi wa jumuiya walio na hadhi nzuri, ambao hawana sifa ya kupiga kura chini ya makundi mengine, wanaruhusiwa kupiga kura iwapo watakutana na mojawapo ya yafuatayo:

  • wametuma maombi, kupokea na kuripoti angalau ruzuku moja ya Wikimedia Foundation tangu [TAREHE YA KUANZA - miezi 12 kabla ya siku ya kwanza ya kupiga kura].
  • walikuwa waandaaji wa angalau tukio moja la hackathon lililofadhiliwa, shindano au tukio lingine la Wikimedia lililo na hati kwenye Wiki na angalau wahudhuriaji/wageni/washiriki 10 kati ya [TAREHE YA KUANZA - miezi 12 kabla ya siku ya kwanza ya kupiga kura] na [TAREHE YA MWISHO - siku 30 kabla ya siku ya kwanza ya kupiga kura].
  • ni mfanyakazi, mkandarasi, au mjumbe wa Bodi ya kituo cha majaribio ambacho hupokea ufadhili kutoka kwa WMF mahususi kwa ajili ya majaribio ya kituo hicho tangu [TAREHE YA KUANZA - miezi 12 kabla ya siku ya kwanza ya kupiga kura].

Watu wanaoomba kupiga kura chini ya kundi hili lazima wajumuishe uthibitisho wa shughuli zao. Ikiwa ulipokea ruzuku ya Wikimedia Foundation, tafadhali toa kiungo cha ripoti yako ya ruzuku. Kwa waandaaji, tafadhali toa kiungo kwa ukurasa wa mwaliko au uthibitisho wowote wa tukio mtandaoni.

Kumbuka

Ukitimiza vigezo vya wahariri wakuu, utaweza kupiga kura mara moja. Kwa sababu ya vikwazo vya kiufundi vya SecurePoll, watu wanaotimiza vigezo vya ziada huenda wasiweze kupiga kura moja kwa moja, isipokuwa watimize vigezo vingine. Iwapo unafikiri umetimiza vigezo vya ziada, tafadhali tuma barua pepe kwa electcom(_AT_)wikimedia.org ukiwa na hoja angalau siku nne (4) kabla ya tarehe ya mwisho ya kupiga kura. Ikiwa unakidhi vigezo, tutakuongeza kwenye orodha ya mwongozo, ili uweze kupiga kura.