Wikimedia Future Lab

Wikimedia Futures Lab ni mchakato na mkutano ulioandaliwa na Wikimedia Foundation na Wikimedia Deutschland ambao utasaidia wote tujifunze kuhusu mienendo ya kiulimwengu na mijadala muhimu juu ya harakati za Wikimedia. Kutakuwa na mkutano wa ana kwa ana utakaofanyika tarehe 30 Januari – 1 Februari, 2026 mjini Frankfurt, Ujerumani. Mkutano ujamuisha washiriki 100. Tunatazamia kuwa na mjumuiko wadau na wachangiaji mbalimbali na wataalamu kutoka nje.
Tunakaribisha washiriki kuchunguza mitindo ya kimataifa kupitia mtazamo wa ndani wa jamii zao. kwa mfano:
- Unaonaje mitindo muhimu ya kimataifa inavyoweza kusaidia jamii yako na maudhui yake?
- Nini maoni ya umma, kuhusu ukuaji wa wachangiaji au kanuni za kisheria kwenye eneo lako ndani ya eneo lako?
- Maendeleo gani ya hivi karibuni yanaathiri jamii yako?
Dhumuni la Mkutano
Katika kipindi hiki cha mabadiliko makubwa ya kimataifa, Harakati za Wikimedia zinakabiliwa na changamoto kuhusu umuhimu na ustahimilivu wa miradi yetu. Tunahitaji kuongeza uelewa wetu kuhusu jinsi dunia na mtandao zinavyobadilika karibu nasi, jinsi mabadiliko haya yanavyoathiri watu na miradi yetu, na kuandaa majibu ya pamoja yanayounga mkono dhamira yetu ya pamoja ya maarifa huria. Watumiaji wa Wikimedia tayari wameshaanza kujadili mitindo ya kimataifa (mfano: Mpango wa Mwaka wa Wikimedia Foundation 2025/26, Uchambuzi wa Harakati kuhusu Mitindo ya Kimataifa) inayoathiri jamii na miradi yetu, kuanzia kupungua kwa imani kwenye taarifa za mtandaoni, kuongezeka kwa maudhui yanayotengenezwa na AI, mabadiliko ya mfumo wa kisheria, na mengine mengi.
Lengo namba 1: Kuimarisha hisia za kuwa sehemu ya harakati
- Matarajio: Washiriki wapate uelewa kuhusu mitazamo tofauti na muktadha wa jamii, washirikiane kuunda uelewa wa pamoja na changamoto na fursa, na kuibua taswira za mustakabali wa Wikimedia.
Lengo namba 2: Kujadili mitindo muhimu na jinsi inavyoathiri Wikimedia
- Matarajio: Washiriki washirikiane na wataalamu na tafiti ili kuongeza uelewa wa Harakati kuhusu mitindo muhimu inayowagusa Wikimedia, na kujadili jinsi maendeleo ya kimataifa yanavyoathiri muktadha wa kanda.
Lengo namba 3: Kupendekeza na kubadilisha mikakati ili kubaki na umuhimu
- Matarajio: Washiriki kijadili mikakati inayowezekana ili kukabiliana na mitindo hii na kuibua mawazo ya awali yanayoweza kuendelezwa baada ya tukio.
Additional Futures Lab conversations
- Wikimania workshop
- Session at the CEE Meeting
- Session at the German WikiCon
- Session at the WikiCon North America
Information about online engagement will follow.