Mwongozo wa Kimataifa wa Mwenendo na Maadili/Kamati ya Uratibu/Chaguzi/2024

From Meta, a Wikimedia project coordination wiki
This page is a translated version of the page Universal Code of Conduct/Coordinating Committee/Election/2024 and the translation is 86% complete.
Universal Code of Conduct

Ukurasa huu unaelezea mchakato wa uchaguzi wa Kamati ya Uratibu wa Mwongozo wa Kimataifa wa Mwenendo na Maadili kwa mwaka 2024.

Muda

Hii ndio ratiba ya matukio inayotarajiwa.

5 Machi 2024 Tangazo la uchaguzi wa U4C
5 Machi – 8 Aprili 2024, End of Day, Anywhere on Earth[1] Wito kwa wagombea wa U4C
10 Aprili 2024 – 24 Aprili 2024 Maswali ya jumuiya kwa wagombea
25 Aprili 2024 – UTC Kipindi cha kupiga kura
Mei 2024 Kutangaza wanachama wa U4C ya kwanza

Wito kwa Wagombea

Kamati ya Kuratibu Mwongozo wa Kimataifa wa Mwenendo na Maadili(U4C) ni kikundi chenye wajumbe kutoka mataifa mbalimbali kilichojitolea kutoa utekelezaji sawa na thabiti wa UCoC. Wanajamii wanaalikwa kutuma maombi yao kwa U4C.

Kama ilivyobainishwa na kifungu cha 2.1 cha mkataba wa U4C, kila mwanachama na mgombea lazima:

  • Akubaliane na UCoC.
  • Awe na angalau umri wa miaka 18 na atie saini makubaliano ya Usiri kwa taarifa zisizo za umma (NDA) na Shirika la Wikimedia Foundation punde tu atakapochaguliwa.
  • Awe hajazuiwa kwenye mradi wowote wa Wikimedia wala kuwa na marufuku inayoendelea ya tukio katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita. Wagombea ambao wamezuiwa wanaweza kukata rufaa kwa Kamati ya Uchaguzi, ambao wanaweza kufanya ubaguzi.
  • Wajitambulishe hadharani wao wenyewe miradi yao ya wiki ya nyumbani na kanda wanayotoka.
  • Wakidhi mahitaji mengine yoyote ya kustahiki yaliyobainishwa wakati wa mchakato wa uchaguzi.
  • Uwe mwanachama aliyesajiliwa wa angalau mradi mmoja wa Wiki kwa angalau siku 365 na uwe na mabadiliko yasiyopungua 500 tarehe 5 Machi 2024 12:00 UTC.

Kulingana na sura ya 2 ya mkataba wa U4C, kuna viti 16 kwenye U4C: viti vinane vya jumuiya kwa ujumla na viti vinane vya kanda ili kuhakikisha U4C inawakilisha utofauti katika hizi harakati. Si zaidi ya wanachama wawili wa U4C wanaoweza kuchaguliwa kutoka wiki moja ya nyumbani.

Kulingana na mbinu ya kieneo ya Shirika la Wikimedia, usambazaji wa kikanda utakuwa kama ifuatavyo:

  • Amerika ya Kaskazini (Marekani na Kanada)
  • Ulaya ya Kaskazini na Magharibi
  • Amerika ya Kusini na

Karibiani

  • Ulaya ya Kati na Mashariki (CEE)
  • Nchi za Kusini mwa Jangwa la Sahara
  • Mashariki ya Kati na Afrika Kaskazini
  • Mashariki, Kusini Mashariki mwa Asia na Pasifiki (ESEAP)
  • Asia Kusini

Ingawa uanachama wa U4C ni wa muda wa miaka miwili, wakati wa uchaguzi wa kwanza, wawakilishi wa kanda watatimiza mihula ya miaka miwili na wawakilishi wa jumuiya kwa ujumla watatimiza masharti ya mwaka mmoja.

Maswali kwa wagombea

Wapiga kura wanaostahiki wanaweza kuuliza maswali kwa wagombea wote kwenye Ukurasa wa Maswali'. Wapigakura wanaombwa kutuma si zaidi ya maswali 2 (mawili) yanayofaa kwa kila mtahiniwa (jumla; yaani, maswali yote ambayo mtahiniwa anahitaji kujibu yanahesabiwa), na kuyaweka kwa ufupi na muhimu iwezekanavyo. Watahiniwa wanaombwa kujibu kwa ufupi na kwa urahisi iwezekanavyo.

Kanuni za kampeni

Wagombea wanaombwa kukagua na kutii sheria za kampeni katika kipindi chote cha uchaguzi.

Teuzi

Tafadhali tembelea ukurasa wa wagombea' ili kujipendekeza mwenyewe kwaajili ya U4C.

Upigaji kura

Ustahiki wa mpiga kura

Tafadhali kagua vigezo vya ustahiki wa mpiga kura ili kujua kama unastahiki kupiga kura.

[Zana ya kuchunguza Ustahiki wa ] inaweza kutumika kuthibitisha kwa haraka ustahiki msingi wa kupiga kura wa mhariri.

Ikiwa unastahiki kupiga kura:

  1. Soma taarifa za wagombea.
  2. Amua ni wagombea gani utawaunga mkono.
  3. Nenda kwenye ukurasa wa upigaji kura wa SecurePoll.
  4. Fuata maagizo yaliyopo kwenye ukurasa huo.

Mchakato wa upigaji kura

Kwa mujibu wa kipengele cha 2.5. cha Mkataba wa U4C:

  • Upigaji kura unafanywa kwa kura ya siri, huku wapiga kura wakitoa uungaji mkono, kupinga na kura zisizoegemea upande wowote kwa kila mgombea.
  • Wapiga kura wanaweza kuwapigia kura wagombea kutoka kanda zote.
  • Kura za zisizoegamia upande wowote hazitahesabiwa.
  • Ustahiki wa wapiga kura utaamuliwa na Kamati ya Uchaguzi.
  • Ni lazima mgombea awe na asilimia 60 au zaidi ya kura kama ilivyokokotolewa na usaidizi/(uungwaji mkono + kupinga). Baada ya sifa hii:
    • Kwa kila mgombea idadi ya wapinzani itatolewa kutoka kwenye idadi ya wafuasi. Wagombea walio na tofauti kubwa zaidi watachaguliwa kwa kila kiti.
    • Iwapo watahiniwa wawili wana tofauti sawa basi asilimia inayokokotolewa kupitia kukubalika/(kukubalika + kupingwa) itatumika kama kitenganishi cha mfungamano wa kura.

Results

Regional seats (two-year term):

  • Northern and Western Europe
  • Middle East and North Africa
  • East, South East Asia and Pacific (ESEAP)

Community-at-large seats (one-year term):

Evaluation

A community evaluation phase for the election processes is open. Please post your feedback directly to this page.

Kumbukumbu

  1. Hapo awali ilifungwa mnamo 1 Aprili 2024, iliyoongezwa muda wa wiki moja kwa mujibu wa maamuzi ya EC.