Translations:Wikimedia Foundation elections/Board elections/2013/14/sw

From Meta, a Wikimedia project coordination wiki

Uchaguzi wa Baraza la wadhamini mwaka 2013 utafanyika kuanzia tarehe 8 hadi 22 mwezi Juni mwaka 2013. Wanachama wa jumuiya ya Wikimedia watapata fursa ya kuchagua wagombea watatu ambao watafanya kazi kwa kipindi cha miaka miwili ambacho kitakamilika mnamo mwaka wa 2015. Bodi ya wadhamini ndiyo yenye mamlaka makuu katika Wikimedia Foundation, shirika lisilokuwa la kifaida lenye usajili nchini Marekani. Shirika la Wikimedia linasimamia miradi mingi mbali mbali kama vileWikipedia na Commons.