Mpango wa Mwaka wa Shirika la Wikimedia/2024-2025/Ushirikiano

From Meta, a Wikimedia project coordination wiki
This page is a translated version of the page Wikimedia Foundation Annual Plan/2024-2025/Collaboration and the translation is 55% complete.
Outdated translations are marked like this.

Ushirikishwaji

Katika miaka michache iliyopita tumeendelea kubadilika na kuboresha mchakato wa kupanga ushirikiano – lengo la Shirika la Wikimedia bado likizingatia wanadamu na teknolojia kutokana na jukumu la kipekee la Shirika kama mtoaji wa jukwaa kwa watu na jamii zinazoongoza mifumo katika utayarishaji wa maarifa kati ya rika hadi rika. Malengo manne makuu (Usawa, Miundombinu, Usalama, Ufanisi) bado yanabakia kuwa kipaumbele bila kubadilika, huku kazi na yanayofikiwa ndani yake yanasisitiza maendeleo makubwa yaliyopatikana katika mwaka huu.

Majadiliano yalianza mwaka huu kwa Talking:2024 - mazungumzo kati ya wafanyakazi wa Shirika, viongozi, wajumbe wa bodi, na Wanawikimedia duniani kote. Walifuatwa na mwaliko kutoka kwa Afisa Mkuu wa Bidhaa na Teknolojia Selena Deckelmann kwaajili ya kutoa maoni kwenye wiki kuhusu malengo yanayopendekezwa kwa ajili ya kazi ya bidhaa na teknolojia ya Shirika mwaka ujao. Malengo haya yanatokana na mazungumzo yanayoendelea kupitia Talking:2024, ambayo yaliangazia umuhimu wa kuendelea kuzingatia mahitaji ya mfumo wetu na wachangiaji mtandaoni.

Tunakaribisha mawazo yako sasa hadi tarehe 31 Mei 2024 na tutasasisha ukurasa huu kadri mijadala mipya kwenye wiki na mijadala ya moja kwa moja itakapofunguliwa katika vituo na lugha mbalimbali. Mijadala hii ni sehemu ambayo Wanawikimedia hutoa maoni yao kuhusu mipango iliyopendekezwa na hutoa maoni yao kuhusu malengo yao ya mwaka ujao. Kwa kuhamasishwa na kile ambacho wengine wengi wanafanya katika kazi zao wenyewe, tunaendelea kupata fursa za kushirikiana na kujifunza kutoka kwenye michakato ya kupanga na kazi ya wengine katika harakati za Wikimedia pamoja na washirika wengine. Mwaka huu kuna njia nyingi za kujihusisha: hapa kwenye Meta-Wiki, katika nafasi za jumuiya zilizoundwa pamoja, kwenye kurasa za mradi wa Wikimedia, na kwenye chaneli za jumuiya.

Nafasi za Jumuiya Zilizoundwa Pamoja

Mwaka huu, wafanyakazi na viongozi kutoka Shirika la Wikimedia Foundation watajiunga na vikao vilivyopo vilivyoandaliwa na jumuiya ili kuwa na upangaji kutoka pande zote mbili katika rasimu ya mpango wa mwaka ujao. Kwa kuongezea, wafanyakazi wa Shirika wanapanga vikao kadhaa vya mtandaoni vya kimaudhui ambavyo mtu yeyote anaweza kuhudhuria kulingana na eneo analopenda. Iwapo ungependa kujiunga na vikao hivyo lakini tafsiri haipatikani katika lugha unayopendelea, tutumie barua pepe kwenda movementcomms@wikimedia.org, na tutafanya mipango inayohitajika. Tafadhali kumbuka kuwa orodha itasasishwa mara kwa mara kadiri tarehe zinavyokamilishwa ili kuhakikisha kuwa una habari iliyosasishwa zaidi.

  1. Mazungumzo ya Kamati ya Masuala ya Jamii ya Wikimedia Foundation na Wadhamini: .
  2. WikiCauserie: , tafsiri inapatikana: Kiingereza - Kifaransa.
  3. Kikao cha Wanajumuiya ya MENA , tafsiri zinapatikana: Kiingereza - Kiarabu.
  4. CEE Catch up: , tafsiri zinapatikana: Kiingereza - Kirusi
  5. Annual Planning Session at ESEAP Conference 2024: .
  6. Kikao cha wazi cha Jumuiya Wanawikimedia wa Igbo: .
  7. Cross-regional meeting: May 15, 2024 (15.00-16.30 UTC), interpretation available: English, French, Polish, Portuguese, Spanish.
  8. Wikimedia AI call: May 16, 2024 (14.00-15.00 UTC). Interpretation: TBD
  9. Afrika Baraza: , tafsiri itapatikana: Kiingereza – Kifaransa, Kiarabu na Kiswahili.
  10. Kikao cha Wazi cha Asia Kusini: .

Kwenye Wiki

Muhtasari wa ujumbe wa kushiriki katika mazungumzo ya mpango wa kila mwaka utachapishwa ndani ya tovuti mahalia kwenye miradi mbalimbali. Toleo kamili la rasimu ya nyenzo za mpango wa kila mwaka na tafsiri zinazoambatana nalo zitapatikana kwenye tovuti hii ya Meta-Wiki. Unaweza kushirikiana nasi kwenye kurasa zote za mazungumzo ya ndani na hapa kwenye ukurasa wa mazungumzo wa Meta-Wiki, kila mara katika lugha unayopendelea. Tutaongeza viungo hapa ambapo maudhui yamechapishwa kadri yanavyopatikana.

Mazungumzo mengine kuhusu upangaji wa kila mwaka pia yanafanyika katika chaneli nyingine za jumuiya kwenye Discord na Telegram. Tunakuhimiza ujiunge na mijadala ikiwa utajisajili katika vituo hivi.

Mazungumzo yanayohusu bidhaa yatafanyika katika vituo tofauti. Mazungumzo ni kati ya wanajamii wanaoshirikiana na timu za Bidhaa za Wikimedia Foundation ambazo zinamiliki malengo na matokeo muhimu katika mpango wa kila mwaka. Wanajamii wanaovutiwa na malengo mahususi na matokeo muhimu yanayomilikiwa na timu za Bidhaa wanaweza kushirikiana na timu kwa maelezo ya kazi ya malengo wanayomiliki, utekelezaji wake, na upatanishi na kazi na maslahi ya jumuiya.

Mazungumzo ni fursa za kuuliza maswali na kupata ufafanuzi kuhusu kazi iliyoainishwa ya timu za bidhaa kwa mwaka wa 2024-25 kulingana na malengo ya mpango wa kila mwaka na matokeo muhimu. Tutaongeza viungo vya mahali ambapo timu za bidhaa zinashirikiana na hadhira yao zitakapopatikana.