Sera za Wafadhili

From Meta, a Wikimedia project coordination wiki
Jump to navigation Jump to search
This page is a translated version of the page Donor policy and the translation is 96% complete.

Haki za Wafadhili

Tunaunga mkono haki za Wafadhili

Uhisani ni msingi wa matendo ya hiari kwa ajili ya manufaa ya wote. Matendo hayo hujengwa na utamaduni wa kutoa na kushirikiana ambao ni wa msingi kwa ubora wa maisha. Ili kuhakikisha kwamba uhisani unapata heshima na imani ya umma kwa ujumla, na kwamba wafadhili na wafadhili watarajiwa wanaweza kuwa na imani kamili kwa mashirika yasiyokuwa na faida na kwa malengo wanayotakiwa kuunga mkono, sisi tunatangaza kwamba wafadhili wote hupewa haki hizi:

 1. Kujulishwa lengo la shirika, njia ambayo shirika linatarajia kutumia rasilimali, na uwezo wake wa kutumia michango yao kwa ufanisi kwa madhumuni yaliyokusudiwa.
 2. Kujulishwa utambulisho wa wanaohudumu kwenye bodi ya shirika la utawala, na kwa kutegemea bodi kufanya hukumu busara katika majukumu yake ya uwakili.
 3. Kupata taarifa za shirika za fedha ya hivi karibuni.
 4. Kuhakikishiwa kuwa zawadi zao zitatumika kwa ajili ya malengo ambayo walipewa.
 5. Kupokea kukiri sahihi na kutambuliwa.
 6. Ili kuhakikishiwa kwamba taarifa kuhusu michango yao itabebwa kwa heshima na usiri kwa kiasi kilichoelezewa na sheria.
 7. Kutarajia kwamba uhusiano wote na watu binafsi wanaowakilisha mashirika ya yenye haja na wahisani utakuwa ni wa kitaalamu katika asili.
 8. Kupashwa taarifa kama wale wanaotaka michango ya kutafuta ni wahanga, wafanyakazi wa shirika au wakili wa kuajiriwa.
 9. Kuwa na fursa ya majina yao kufutwa kutoka kwa orodha ya wanaopokea barua pepe ambayo shirika inakusudia kugawa.
 10. Kujisikia huru kuuliza maswali wakati wa kufanya mchango na kupokea kwa haraka, majibu ya kweli na ya uwazi.

Nakala ya kauli hii katika ukamilifu wake ilianzishwa na Association of Fundraising Professionals (AFP), Association for Healthcare Philanthropy (AHP), BCouncil for Advancement and Support of Education (CASE), na Giving Institute: Mshauri mkuu wa mashirika yasiyo ya kibiashara na kiserikali.

Sera za faragha za Wafadhili wa Wikimedia

Maudhui ya ukurasa huu ni sera rasmi zilizopitishwa na Wakfu wa Wikimedia Bodi ya Wadhamini. Wikimedia inaweka ngazi ya juu ya heshima kwa faragha ya wafadhili wake. Katika kuboresha ahadi yetu na heshima ya haki zako, sisi tumeendeleza Sera hii ya Siri ya wafadhili kuongoza wafanyakazi wetu na wahanga juu ya jinsi wanavyoweza ama ambavyo hawawezi kutumia taarifa yako binafsi.

Habari ambayo sisi hukusanya

Wikimedia Sisi hutumia taarifa binafsi zinazokusanywa kutoka kwa wafadhili kwa ajili ya usindikaji wa malipo na kuwasiliana na wafadhili kuhusu Wikimedia pamoja na kufanya kutafuta fedha na shughuli nyingine ya Wikimedia. Habari hii ni pamoja na jina, kiasi cha msaada, anwani, namba ya simu, maoni ya wafadhili, anwani ya barua pepe, na habari nyingine yoyote ya kibinafsi zinazotolewa kwetu ("Data ya mfadhili"). Kwa ajili ya michango kwa hundi, Data ya mfadhili pia ni pamoja na data wazi juu ya hundi.

Kama sehemu ya kutoa uzoefu wa mtandao unavyotarajiwa na wafadhili wetu, sisi tunaweza kuhifadhi takwimu mbalimbali ambazo zinakusanywa kama sehemu ya shughuli kiwango cha mtandao (ikiwa ni pamoja na mambo kama masharti wakala wa watumiaji, anwani ya IP, wakala wa referrer, na kuki). Tunaweza kutumia taarifa hii kwa madhumuni ya ilivyoelezwa katika sera hii, ikiwa ni pamoja na mahitaji ya uchambuzi na utendaji bora wa tovuti yetu. Sisi hufanya matumizi madogo ya kuki, ikiwa ni pamoja na kuki za washirika wa ngazi ya tatu (kama vile kuki kutoka kwa wasindikaji malipo), kufuatilia vikao, kusaidia kuhifadhi takwimu, na kutimiza malengo yaliyowekwa katika sera hii. Unaweza kuzuia au kufuta kuki zetu na kurekebisha mpangilio wa kivinjari chako, ingawa hii inaweza kuathiri utendaji wa tovuti.

Wasindikaji wa Malipo na Watoa Huduma nyingine Wasindikaji wa Malipo wanaruhusu wafadhili kutoa kwa njia ya elektroniki kwa kutumia huduma ya malipo ya akaunti, kadi, au njia nyingine ya malipo. Hawa wasindikaji hukusanya taarifa fulani kutoka kwa wafadhili, na unapaswa kushauriana na sera zao za faragha ili kujua utendaji wao.

Kuwapa wafadhili uzoefu bora kadri iwezekanavyo, tunafanya kazi na watoa huduma na kushiriki takwimu za wafadhili na taarifa nyingine, au kuituma iwafikie. Watoa huduma kama hawa ni pamoja na, kwa mfano, collocation facilities na watoa upana-bendi pamoja na mashirika ambayo husaidia mashirika yasiyo ya faida kutafuta fedha.

Jinsi tunavyotumia habari hii

Takwimu ya Mfadhili Takwimu za wafadhili zinaweza kutumika kwa ajili ya madhumuni yafuatayo:

 • Kusambaza risiti na kushukuru wafadhili kwa ajili ya michango yao
 • Kujulisha wafadhili kuhusu mipango ya kutafuta fedha ijayo na shughuli nyingine ya Wikimedia
 • Uchambuzi wa ndani, kama vile utafiti na analytics
 • Kuweka rekodi
 • Kutoa taarifa kwa vyombo husika vya serikali kama inavyotakiwa na sheria
 • Tafiti, vigezo, na malengo mengine ya uchambuzi
 • Malengo mengine kuhusiana na shughuli za kuchangisha fedha

Isipokuwa kama ilivyoelezwa vinginevyo, hatuwezi kuchapisha, kuuza, kufanya biashara, au kukodisha takwimu za wafadhili. Habari ya wafadhili iliyofichwa inaweza kutumika kwa ajili ya shughuli za uhamasishaji na shughuli za kutafuta fedha. Maoni yanayotolewa na wahisani yanaweza kuchapishwa hadharani na yanaweza kutumika katika vifaa vya uhamasishaji. Tunaweza kutumia taarifa zilizopo ili kuongeza Takwimu za Wahisani ili kuboresha taarifa ambayo sisi hutumia kama gari katika jitihada zetu za kutafuta fedha. Tunaweza kuruhusu wafadhili chaguo kuwa na jina lao hadharani kuhusishwa na mchango wao isipokuwa vinginevyo alivyo omba kama sehemu ya mchakato wa mchango mtandaoni.

Sisi hutumia takwimu zilzosanywa kwa ajili ya wasindikaji wa malipo na watoa huduma wengine kwa madhumuni yaliyoelezwa katika sera hii.

Habari za Kifedha

Ni sera zetu za ndani ya kupunguza upatikanaji wa taarifa za fedha kwa wafanyakazi wa kitaalamu na wa kujitolea ambao wanahitaji kuchakata habari hiyo kwa madhumuni yaliyoelezwa hapo juu. Habari binafsi ya kifedha haiuzwi kwa au kufanywa biashara na vyama vingine.

Sisi hutumia washirika kutoa huduma za usindikaji wa malipo kwa mtandao.Kawaida, sera za faragha ya mashirika haya yatawasilishwa kwako kwenye tovuti zao na kwa kawaida pia kama sehemu ya mchakato wa mchango wako.Kama utaulipa na kadi ya mikopo, hatuwezi kuhifadhi habari ya kadi yako, namba ya akaunti ya benki, au takwimu za kifedha za akaunti ambazo hutumwa moja kwa moja kwa watoa huduma hizo za usindikaji.

Michango kwa Wikimedia iliyotolewa kwa hundi huenda kwenye kisanduku kilichofungwa cha benki. Hii inatoa kiwango hasa cha juu cha usalama na siri.

Wasiliana nasi

Kama una maswali kuhusu sera hii ya faragha ya wafadhili au maombi juu ya hali na usahihi wa takwimu yako ya mfadhili, tafadhali tuma barua pepe kwa donate <at> wikimedia.org au andika kwa:

Wikimedia Foundation, Inc.
1 Montgomery Street
Suite 1600
San Francisco, CA 94104
USA

Kama unataka kutoa mchango kwa hundi, tafadhali itume kwa:

Wikimedia Foundation, Inc.
P.O. Box 98204
Washington, DC 20090-8204
USA
Note: donations by check are processed directly at our centralized lockbox location which is in Washington, DC.

Usalama

Sisi ni nia yetu ni kulinda habari binafsi za wafadhili kutokana na upatikanaji usioruhusiwa, mabadiliko, kutoa tarifaa, au uharibifu. Pamoja na mambo mengine, sisi hufanya mazoea mbalimbali ya usalama, ikiwa ni pamoja na hatua za kusaidia usalama wa upatikanaji wa takwimu hii nyeti na kufanya jitihada za kukabiliana na udhaifu usalama kwa ajili ya zana mbalimbali na hifadhidata.

Matangazo mengine

Tunaweza kutoa taarifa kwa mujibu wa sheria, wakati inahitajika kulinda haki zetu, usiri, usalama, mali, wafadhili, au watumiaji, na wakati muhimu kutekeleza masharti yetu ya huduma.

Masasisho

Tunaweza kubadili Sera za faragha za Wahisani mara kwa mara.Mabadiliko yoyote na mabadiliko yote yatakuwa yakijitokeza kwenye ukurasa huu. Mabadiliko makubwa pia yanaweza pia kutangazwa kwa kupitia njia zingine na ambazo sisi hutumia kuwasiliana na watumiaji wetu na jamii. Unapaswa mara kwa mara kuangalia ukurasa huu kwa ajili ya mabadiliko yoyote ya sera ya sasa.

Takwimu inakoelekea

Wikimedia ni shirika la duniani kote. Kwa kuchangia, wewe umekukubaliana na uhamisho wa taarifa zilizokusanywa kwa nchi za Marekani na maeneo mengine kama inaweza kuwa ni lazima kutekeleza madhumuni na malengo yaliyowekwa katika sera hii.

Uhifadhi wa Takwimu

Tunataka kuhifadhi habari kuhusiana na wafadhili kama tu inavyohitajika kutimiza malengo yalivyoelezwa katika sera hii isipokuwa tena kama kipindi kirefu cha uhifadhi kinahitajika kwa mujibu wa sheria au kanuni.Kwa mfano, sheria ya kodi nchini Marekani na Jimbo la Florida inahitaji Wakfa kuweka taarifa za mawasiliano na kiwango cha mchango wachwafadhili kwenye faili.

Haki

Una haki fulani kwa heshima ya taarifa ambayo sisi hukusanya kuhusu wewe. Baada ya ombi, tutakuambia ni taarifa gani sisi tumeshikilia inayokuhusu wewe na kusahihisha maelezo yoyote yasiyo sahihi. Sisi pia tutafanya juhudi ya kufuta taarifa yako kama wewe utatuuliza kufanya hivyo, isipokuwa vinginevyo tunatakiwa kuitunza.

Wigo

Sera hii haswa inatumika kwa kuwa aliyeichapisha . Kama wewe umetembelea ukurasa wa michango wa Wikimedia kutoka eneo ambayo lina Sura, unaweza kuwa - ingawa si lazima - kuelekezwa kwa tovuti ya Sura. Sura ni huru na huenda baada ya sera tofauti na mazoea kulingana na mahitaji ya ndani ya sheria na masuala mengine. Sura ambazoo hushiriki katika kutafuta fedha, hata hivyo, zinatarajiwa kuzingatia kanuni za jumla zilizowekwa katika sera hii. Sera hii haina haishughulikii takwimu kutoka vyanzo vingine ila michango tu, kama vile hariri au michango ya maudhui ya miradi au makala.

Ilisasishwa mwisho, Septemba 2011
Sera za hapo awali (Julai 2011) (kwa kumbukumbu)
Sera za awali (2009) (kwa kumbukumbu)
Privacy-related pages