Mobile Projects/WLM App Fact Sheet/sw

From Meta, a Wikimedia project coordination wiki

Jedwali la Habari za Zana za Android Wiki Loves Monuments[edit]

Jedwalii hili linajumlisha habari za msingi kuhusu Zana za WLM ambazo ni muhimu kwa shindano, wandaaji na washiriki. Kama unataka kitu kiongezwe, tafadhali toa maoni yako katika ukurasa wa Majadiliano.

Zana hizi zinafanya nini?[edit]

  • Zana zinatoa njia mbili za kutafuta makumbusho, yaani, monuments: kwa nchi/mkoa/mji na kwa mahali ilipo.
  • Zana hizi zinakupa fursa ya kupakia picha za simu ya mkononi kutoka hifadhi ya picha zako katika simu au picha mpya ambazo unazipiga wakati unatumia zana hizi moja kwa moja na kuzipeleka katika commons.wikimedia.org.
  • Picha zinapakiwa kwa jina la kipekee, ukumbusho ID, jamii sahihi, maelezo ya leseni—na kila kitu kinachohitajika kufanya ingizo hilo ni mahususi kwa shindano.
  • Pia unaweza kutazama historia ya picha ulizopakia na zile ambazo unataka kuzipakia baadaye vilevile. Upakiaji wa baadaye unaweza kuwa rahisi wakati gharama za kuzunguka ni kubwa, wakati mtandao upo chini, na wakati ukitaka kuoanisha makumbusho na picha ulizopiga katika kamera.

Hapa katika toleo fupi:

  • Tafuta makumbusho kwa nchi/mkoa/mji na kwa mahali ulipo
  • Pakia kutoka katika hifadhi ya picha au piga picha mpya
  • Miundo na picha ziwe katika mfumo unaotakikana kwa ajili ya uwasilishaji kwa shindano
  • Kuonesha historia ya vilivyopakiwa na zile ambazo zimeahirishwa hadi hapo baadaye kuhifadhi katika mahali pa kumbukumbu

Wapi naweza kupata zana hizi?[edit]

  • Pia unaweza kupakua Zana za Wiki Loves Monuments Android Beta kwenye hifadhi ya Google Play, inaanza Agosti 15, 2012 - tafuta kwa kuandika "Wiki Loves Monuments beta."

Hilo ni jina refu kwa zana hii. Je, naweza kulifupisha?[edit]

  • Zana za WLM ni toleo fupi mno ambalo linawezekana kufupisha katika majina ya zana hizi. Pia linaweza kufupishwa kwa kuliita WLM Android App. Kwa vile toleo la shindano la mwaka huu litakuwa Android tu, inawezekana kukawa na ulazima wa kuingiza neno Android katika baadhi ya miuktadha.

Katika lugha gani na nchi zipi itakuwa inapatikana?[edit]

  • Zana hii itatafsiriwa na jumuia ya wanaojitolea katika translatewiki.net. Tafsiri zitakuwa zinaboreshwa katika kila toleo la zana hizi.
  • Hata kama zana hii itakuwa haijatafsiriwa, ina maana ya kwamba kusano za mtumiaji zitakuwa zinaonekana kwa Kiingereza, itaonesha makumbusho katika kila nchi itakayoshiriki katika shindano.
  • Google Play ipo kiulimwengu na zana zake zinapaswa kupatikana katika kila nchi ambapo Google Play inapatikana. Hii itajumlisha nchi zote zitakazoshiriki katika shindano.

Vipi naweza kueneza neno kuhusu zana hii?[edit]

  • Tafadhali tumia malighafi zozote zile za masoko zinazopatikana hapa.
    Download the app

Tafadhali weka nakiungo cha kupakulia, logo, kitufe cha Google Play au msimbo wa QR vyovyote unavyoona sawa.

  • Tafadhali jaribu pia kutaja zana hizi katika matangazo ya vyombo vya habari na masoko yoyote yanayohusiana na Wiki Loves Monuments.
  • Jisikie huru kubadili grafiki ili kufikia vipengele vya masharti ya kubana nafasi yanayohitajika - kupata mafaili halisi ya Photoshop, tafadhali tuma barua pepe kwa hwalls at wikimedia dot org.

Je, ninahitaji akaunti katika Commons?[edit]

  • Ndiyo. Kawaida akaunti ya Wikipedia inafanya kazi pia kwenye Commons, la kama sivyo, akaunti mpya kwenye Commons utalazimika kuifungua.
  • Zana hii inatoa kiungo cha kuingia na kuanzisha akaunti katika Commons, lakini itakuwa vizuri zaidi kama utafungua akaunti kabla.

Je, zana hii itaweka picha zangu katika Wikipedia?[edit]

  • Picha ulizopakia zinatafikiriwa kuwekwa katika makala za Wikipedia, mchakato ambao unaanza na maamuzi ya shindano. Iwapo picha yako itawekwa kwenye makala hiyo ni juu ya jumuia za Commons na Wikipedia.
  • Moja ya lengo kuu la shindano ni kuleta picha zaidi za ukumbusho kwenye makala za Wikipedia za makumbusho hayo. Kwa hiyo jaribu kadiri uwezavyo, na usaidie "ufahamu wa bure kuwa bora zaidi"!

Je, naweza kutumia leseni nyingine mbali na zile zilizotolewa na zana hii?[edit]

  • Katika hali zote, kila nchi inayoshiriki katika shindano limechagua leseni moja ambayo watatumia katika mawasilisho yote. Hata hivyo, inawezekana kubadilisha leseni hapo baadaye kwa kwenda katika commons.wikimedia.org, tafuta picha yako na hariri maelezo ya leseni.
  • Pia inawezekana ya kwamba ukatengeneza hali ya uvunjaji wa hakimili kwa bahati mbaya. Kwa mfano, katika baadhi ya nchi sanamu/picha za ukumbusho zenye umri fulani hairuhusiwi kupiga picha. Tafadhali pitia sheria za kila nchi, na hatimaye ukiukwaji wowote wa hakimiliki utajulikana. Kwa ujumla, sanamu ambazo zinaonekana katika zana hii ruksa kwa kupigwa picha na leseni unayoichagua hakikisha ni ya picha.

Kuna kikomo cha muda, au kikomo kingine chochote, katika kutumia zana hii?[edit]

  • Shindano hili linaisha mwishoni mwa mwezi wa Septemba. Inategemea na wandaaji wa shindano, inaweza ikawezekana kuwasilisha picha baada ya kwisha kwa Septemba, lakini kwanza unatakiwa uongee na na wandaaji wa shindano katika nchi yako. Zana hii haitofanya kazi baada ya Oktoba.
  • Unaweza kupiga picha kadiri simu yako inavyoweza. Upakiaji wa baadaye unakupa fursa ya kupakia kwa fungu kwa hivyo upakiaji unaweza kufanyika kwa mara moja tu.

Wapi naweza kupata taarifa kwa ujumla kuhusiana na shindano la mwaka huu?[edit]