Mwongozo wa Kimataifa wa Mwenendo na Maadili/Kamati ya Uratibu/Chaguzi/2024

From Meta, a Wikimedia project coordination wiki
This page is a translated version of the page Universal Code of Conduct/Coordinating Committee/Election/2024 and the translation is 79% complete.
Outdated translations are marked like this.

VOTE HERE

Universal Code of Conduct

Ukurasa huu unaelezea mchakato wa uchaguzi wa Kamati ya Uratibu wa Mwongozo wa Kimataifa wa Mwenendo na Maadili kwa mwaka 2024. Mchakato huu wa uchaguzi umepangwa kufanyika kati ya Machi-Mei 2024.

Muda

Hii ndio ratiba ya matukio inayotarajiwa.

5 Machi 2024 Tangazo la uchaguzi wa U4C
5 Machi - 8 Aprili 2024, End of Day, Anywhere on Earth[1] Wito kwa wagombea wa U4C
10 Aprili 2024 - 24 Aprili 2024 Maswali ya jumuiya kwa wagombea
25 Aprili 2024 - UTC Kipindi cha kupiga kura
Mei 2024 Kutangaza wanachama wa U4C ya kwanza

Wito kwa Wagombea

Kamati ya Kuratibu Mwongozo wa Kimataifa wa Mwenendo na Maadili(U4C) ni kikundi chenye wajumbe kutoka mataifa mbalimbali kilichojitolea kutoa utekelezaji sawa na thabiti wa UCoC. Wanajamii wanaalikwa kutuma maombi yao kwa U4C.

Kama ilivyobainishwa na kifungu cha 2.1 cha mkataba wa U4C, kila mwanachama na mgombea lazima:

  • Akubaliane na UCoC.
  • Awe na angalau umri wa miaka 18 na atie saini makubaliano ya Usiri kwa taarifa zisizo za umma (NDA) na Shirika la Wikimedia Foundation punde tu atakapochaguliwa.
  • Awe hajazuiwa kwenye mradi wowote wa Wikimedia wala kuwa na marufuku inayoendelea ya tukio katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita. Wagombea ambao wamezuiwa wanaweza kukata rufaa kwa Kamati ya Uchaguzi, ambao wanaweza kufanya ubaguzi.
  • Wajitambulishe hadharani wao wenyewe miradi yao ya wiki ya nyumbani na kanda wanayotoka.
  • Wakidhi mahitaji mengine yoyote ya kustahiki yaliyobainishwa wakati wa mchakato wa uchaguzi.
  • Uwe mwanachama aliyesajiliwa wa angalau mradi mmoja wa Wiki kwa angalau siku 365 na uwe na mabadiliko yasiyopungua 500 tarehe 5 Machi 2024 12:00 UTC.

Kulingana na sura ya 2 ya mkataba wa U4C, kuna viti 16 kwenye U4C: viti vinane vya jumuiya kwa ujumla na viti vinane vya kanda ili kuhakikisha U4C inawakilisha utofauti katika hizi harakati. Si zaidi ya wanachama wawili wa U4C wanaoweza kuchaguliwa kutoka wiki moja ya nyumbani.

Kulingana na mbinu ya kieneo ya Shirika la Wikimedia, usambazaji wa kikanda utakuwa kama ifuatavyo:

  • Amerika ya Kaskazini (Marekani na Kanada)
  • Ulaya ya Kaskazini na Magharibi
  • Amerika ya Kusini na

Karibiani

  • Ulaya ya Kati na Mashariki (CEE)
  • Nchi za Kusini mwa Jangwa la Sahara
  • Mashariki ya Kati na Afrika Kaskazini
  • Mashariki, Kusini Mashariki mwa Asia na Pasifiki (ESEAP)
  • Asia Kusini

Ingawa uanachama wa U4C ni wa muda wa miaka miwili, wakati wa uchaguzi wa kwanza, wawakilishi wa kanda watatimiza mihula ya miaka miwili na wawakilishi wa jumuiya kwa ujumla watatimiza masharti ya mwaka mmoja.

Maswali kwa wagombea

Wapiga kura wanaostahiki wanaweza kuuliza maswali kwa wagombea wote kwenye Ukurasa wa Maswali'. Wapigakura wanaombwa kutuma si zaidi ya maswali 2 (mawili) yanayofaa kwa kila mtahiniwa (jumla; yaani, maswali yote ambayo mtahiniwa anahitaji kujibu yanahesabiwa), na kuyaweka kwa ufupi na muhimu iwezekanavyo. Watahiniwa wanaombwa kujibu kwa ufupi na kwa urahisi iwezekanavyo.

Kanuni za kampeni

Wagombea wanaombwa kukagua na kutii sheria za kampeni katika kipindi chote cha uchaguzi.

Teuzi

Tafadhali tembelea ukurasa wa wagombea' ili kujipendekeza mwenyewe kwaajili ya U4C.

Upigaji kura

Ustahiki wa mpiga kura

Tafadhali kagua vigezo vya ustahiki wa mpiga kura ili kujua kama unastahiki kupiga kura.

[Zana ya kuchunguza Ustahiki wa ] inaweza kutumika kuthibitisha kwa haraka ustahiki msingi wa kupiga kura wa mhariri.

Ikiwa unastahiki kupiga kura:

  1. Soma taarifa za wagombea.
  2. Amua ni wagombea gani utawaunga mkono.
  3. Nenda kwenye ukurasa wa upigaji kura wa SecurePoll.
  4. Fuata maagizo yaliyopo kwenye ukurasa huo.

Voting process

  • Voting is conducted by secret ballot, with voters leaving support, oppose and neutral votes for each candidate.
  • Voters are able to vote for candidates from all regions.
  • Neutral votes will not count.
  • Voter eligibility will be decided by the Elections Committee.
  • The candidate must have 60% or higher of votes as calculated by support/(support + oppose). After this qualification:
    • For each candidate the number of opposes will be subtracted from the number of supporters. The candidates with the highest difference will be elected to each seat.
    • If two candidates have the same difference then the percentage calculated by support/(support + oppose) will be used as a tiebreaker.

Kumbukumbu

  1. Hapo awali ilifungwa mnamo 1 Aprili 2024, iliyoongezwa muda wa wiki moja kwa mujibu wa maamuzi ya EC.