Jump to content

Uchaguzi wa Wikimedia Foundation/2022/Tangazo/Pendekeza matamko ya Dira ya Uchaguzi ya 2022

From Meta, a Wikimedia project coordination wiki

Pendekeza taarifa za Dira ya Uchaguzi ya 2022

Unaweza kupata ujumbe huu ukiwa umetafsiriwa katika lugha za ziada kwenye Meta-wiki.

Habarini nyote,

Watu waliojitolea katika uchaguzi wa 2022 wa Baraza la Wadhamini wamealikwa kupendekeza matamko ya kutumia katika Dira ya Uchaguzi.

Dira ya Uchaguzi ni zana ya kuwasaidia wapiga kura kuchagua wagombea ambao wanalingana vyema na imani na maoni yao. Wanajamii watapendekeza kauli kwa watahiniwa kujibu kwa kutumia mizani ya Lickert (kukubali/kutokukubali wala kukataa/kutokukubali). Majibu ya wagombea kwa matamko hayo yatawekwa kwenye zana ya Dira ya Uchaguzi. Wapiga kura watatumia zana hiyo kwa kuandika majibu yao kwenye kauli (kukubali/kukataa/kutokukubali wala kukataa). Matokeo yataonyesha wagombea ambao wanalingana vyema na imani na maoni ya mpiga kura.

Hii hapa ni ratiba ya Dira ya Uchaguzi:

Julai 8 - 20: Waliojitolea wanapendekeza taarifa za Dira ya Uchaguzi

Julai 21 - 22: Kamati ya Uchaguzi kupitia taarifa kwa uwazi na kuondoa taarifa zisizo nje ya mada

Julai 25 - Agosti 3: Wajitoleaji kupigia kura matamko

Agosti 4: Kamati ya Uchaguzi itachagua matamko makuu 15

Agosti 5 - 12: watahiniwa kujipanga na matamko

Agosti 16: Dira ya Uchaguzi itafunguliwa ili wapiga kura waitumie ili kusaidia kutoa uamuzi wao wa kupiga kura

Kamati ya Uchaguzi itachagua matamko makuu 15 mwanzoni mwa Agosti. Kamati ya Uchaguzi itasimamia mchakato huo, ikiungwa mkono na Timu ya Mkakati wa Harakati na Utawala. MSG itaangalia kama maswali yako yako wazi, hakuna nakala rudufu, hakuna makosa ya kuandika, na kadhalika.

Wenu,

Mkakati wa Harakati na Utawala

Ujumbe huu ulitumwa kwa niaba ya Kikosi Kazi cha Uteuzi wa Bodi na Kamati ya Uchaguzi