Kampeni/Timu ya Bidhaa ya WMF/Uundaji wa tukio

From Meta, a Wikimedia project coordination wiki
This page is a translated version of the page Campaigns/Foundation Product Team/Event Creation and the translation is 100% complete.
Community Content Campaigns

Moano ya Mradi

Kwa kuwa sasa timu ya Kampeni imeunda mfumo wa usajili wa tukio, tunapanga kuunda zana ya kuunda tukio. Kwa kutumia zana hii, tunatumai waandaaji wa matukio wataweza kujaza tu taarifa za msingi kuhusu tukio lao katika fomu, na kisha ukurasa utatolewa kiotomatiki bila kuwa na haja ya uhariri mgumu au uumbizaji. Waandaaji watakuwa na chaguo la kujumuisha au kutojumuisha maelezo ya usajili (kupitia zana ya usajili wa hafla) kwenye kurasa zao za hafla. Kurasa zote za tukio zilizoundwa kupitia zana hii zitakuwa kwenye nafasi ya majina ya Tukio.

Tunatazamia kuwa mradi huu utaboresha mchakato wa kuunda tukio na kuboresha kurasa za matukio ili kuifanya itambuliwe zaidi kuliko ukurasa wa kawaida wa wiki. Kwa njia hii, waandaaji wanaweza kuongoza matukio mengi kwa juhudi kidogo, na washiriki wanaweza kuwa na tukio karibishi na lenye kushirikisha zaidi.

Kwa sasa, baadhi ya waandaaji huchagua kuunda kurasa za tukio nje ya tovuti za wiki. Baadhi yao, hutumia jukwaa la watu wengine hurahisisha mchakato wa kushirikiana na washirika au taasisi zinazosimamia kurasa hizi za matukio, hasa pale waandaaji wanapohisi kutoridhika kuunda kurasa za matukio peke yao.

Mradi huu unalenga kuhimiza waandaaji zaidi kuunda kurasa zao za hafla kwenye wiki. Watu wanapaswa kujisikia kutiwa moyo kuendelea kuunda kurasa za matukio katika nafasi nyingine ili kusaidia kueneza habari kuhusu tukio lao. Lakini ni matumaini yetu kwamba, ikiwa tutarahisisha mchakato wa kuunda tukio, waandaaji watataka kuwa na ukurasa wa tukio kwenye wiki.

Kurasa za tukio ni nini?

Katika Wikimedia, kurasa za tukio kwa kawaida hurejelea ukurasa wa wavuti ambapo maelezo yote ya tukio yanaweza kupatikana. Watu hujifunza zaidi kuhusu tukio husika kupitia kurasa hizi. Mara nyingi, pia hutumika kama sehemu ya kujisajilia ambapo washiriki wanaovutiwa wanaweza kujiunga. Ukurasa wa tukio unaweza kuwa rahisi kama ukurasa wa kwenye dashibodi ya uhamasishaji au ngumu zaidi hiyo inajumuisha maelezo ya kina ya malengo ya tukio na ratiba za matukio. Ingawa kurasa hizi zinatofautiana katika muundo na mtindo, kusudi lao ni kutoa habari kuhusu tukio, malengo yake, lini litaanza, lini litaisha, jinsi washiriki wanaweza kushiriki kikamilifu, na jinsi wanavyoweza kuwafikia waandaaji wake.

Je, kurasa za tukio zinaundwa vipi kwenye wiki?

Hivi sasa, hizi ni aina za kawaida za kurasa za matukio zilizoundwa kwenye wiki:

  • Umoja', ukurasa wa pekee (Earth Day 2022 meetup): matukio haya ni ya pekee, matukio ya pekee ambayo ' hayajirudii na si sehemu ya mpango mkubwa wa tukio kwenye wiki. Mara nyingi huwa na unyumbulifu zaidi katika suala la jinsi wanavyowasilisha taarifa, kwa kuwa hawahitaji kupatana na kampeni yoyote kubwa zaidi.
    Matukio yanayojirudia (Women in Red (WikiProject) na Women in Red at University of Edinburgh): Matukio haya hutokea mara kwa mara (kama vile mara moja kwa mwezi). Kila mwezi unaweza kulenga mada tofauti au eneo la kuzingatia. Huenda washiriki wasihitaji kujiandikisha kwa kila tukio, kwa kuwa wamejiandikisha kwa ajili ya tukio linalojirudia kwa ujumla.
  • Matukio ya kimataifa au ya Wiki nyingi yenye matukio madogo (Wikipedia Asian Month, Wiki Loves Monuments, na Wiki Loves Africa): Matukio haya huwa yanahusu wiki nyingi, kwa hivyo yanaweza kushughulikiwa na watu ambao wanahariri katika lugha nyingi, nchi, au jumuiya. Wanaweza kuwa na kamati ya kimataifa ya maandalizi au jopo la waamuzi pamoja na kamati ya ndani ya kuandaa matukio madogo. Matukio madogo yanaweza kutokea katika nyakati na maeneo tofauti, na yanaweza kuwa na muundo tofauti kidogo.
  • Ukurasa mmoja wa tukio ambao ni sehemu ya tukio la kimataifa (WikiGap Prague 2020, WikiGap Ufilipino 2020): Hizi ni kurasa za matukio ambazo zimefungamanishwa na tukio la kimataifa, lakini zina muundo wao huru na mtindo wa uandaaji wa tukio.

Je, ni vipengele vipi vya kawaida kwa ukurasa wa tukio?

Baadhi ya vipengele vya kawaida vinavyopatikana katika kurasa nyingi za matukio ni pamoja na malengo ya matukio, kalenda ya matukio, njia za mawasiliano, ratiba za mikutano na mwongozo wa hatua kwa hatua kuhusu jinsi watu wa kujitolea wanavyoweza kujiunga. Kurasa za matukio ya kimataifa ni za kina zaidi, zikiwa na orodha ya mada inayopendekezwa, marejeleo na maelezo ya ziada kuhusu jinsi ya kuandaa tukio kama hilo ndani ya nchi.

Basic Components

  • Header / Banner
Event page: Home


  • Navigation menu
Juu ya ukurasa (visit page)


Katikati ya ukurasa (tembelea ukurasa)


Pembezoni mwa ukurasa (visit page)
  • Event goals
Sehemu ya Ukurasa wa tukio: Goals
hufafanua upeo na lengo la tukio na kwa kawaida hubainisha jinsi mshiriki anaweza kuchangia.
  • Event details
Sehemu ya ukurasa wa tukio: Matukio ya Jumuiya - Taarifa ya uratibu (tarehe, saa, eneo, viungo vya kujiunga na kikao cha Video mtandanoni, n.k.)
  • Image gallery
Event page section: Gallery - Mkusanyiko wa picha unaweza kuwa collection of event photos na/au collection of submissions
  • FAQs
Event page section: FAQ

Organizer tools

  • Registration list
Event page section: Registration
  • Namna ya kupanga matukio
Event page section: How to organize - Mwongozo wa jinsi mratibu wa ndani anaweza kuunda tukio kwa ajili ya jumuiya yao
  • Orodha ya shughuli
Event page section: Worklist - Orodha ya mada na kazi lengwa za kukamilisha kutayarisha tukio.
  • Kanuni za tukio
Sehemu ya Ukurasa wa tukio: Kanuni za Tukio - Kwa mashindano ya kuandika, hii kwa kawaida inarejelea miongozo ya jinsi michango itakavyo pewa alama.


Zana za Washiriki

  • Jinsi ya kujiunga
Sehemu ya ukurasa wa Tukio: Jinsi ya kujiunga - Sehemu inayotoa maelekezo ya namna ambavyo washiriki wanaweza kujiunga.


  • Rasilimali
Sehemu ya ukurasa wa tukio: Nyenzo - Sehemu iliyo na orodha ya nyenzo za utangulizi kwa wanaoanza katika maandalizi ya kujiunga na tukio.
  • Saa ya kijamii au ya kiofisi
Sehemu ya ukurasa wa Tukio: Saa za Ofisi - Mwaliko kwa saa za kijamii au za kiofisi
  • Muhtasari wa tukio
Event page section: Matukio yaliyopita - Viungo vya marudio ya awali ya tukio.

Zana za mawasiliano

  • Wasiliana na timu ya inayoratibu tukio
Sehemu ya ukurasa wa tukio: Wasiliana na timu inayoratibu tukio - Maelezo kuhusu jinsi mtumiaji anayevutiwa anavyoweza kuungana na ama waandaaji wa tukio. Kwa matukio ya kimataifa, hii ni fursa ya kuungana na waandaaji wanaoendesha tukio moja katika nchi tofauti au mradi wa wiki.
  • Discussion
Event page section: Discussion - Ukurasa ambapo mtumiaji yeyote anaweza kuacha maswali na mapendekezo yake kuhusu tukio hilo.
  • Nyenzo za mitandao ya kijamii
Sehemu ya ukurasa wa tukio: Nyenzo za mitandao ya kijamii- Picha au maandishi ambayo yametayarishwa kushirikishwa kwenye mitandao ya kijamii

Kurasa za matukio kwa kawaida huundwaje hivi sasa?

Kurasa za matukio kwenye wiki huundwa kwa njia sawa na namna ukurasa wa kawaida wa wiki unavyoundwa. Kurasa nyingi za matukio kwa ajili ya kampeni za maudhui ya kimataifa na mikutano huundwa kwenye Meta-Wiki, huku marudio ya ndani ya kampeni hizi pamoja na matukio ya kipekee ya ndani yanaundwa kwenye mradi wa wiki mahususi ambao wanalenga kuboresha. Ingawa baadhi ya wiki zina kanuni za kuunda ukurasa, hakuna njia sanifu ya kuunda ukurasa wa tukio na waandaaji wengi wenye uzoefu wamebuni njia mbalimbali, kwa kutumia mifumo changamano ya kutengeneza violezo ili kuunda hali ya utumiaji iliyo rafiki kwa wageni. Hata hivyo, hatua zifuatazo ni mazoezi ya kawaida yanayofanywa na waandaaji wengi.

  • Kwa kurasa za matukio ya pekee, tukio linalojitegemea: Kwa kawaida kwa matukio mapya na ya kipekee, kurasa za tukio huandaliwa kuanzia mwanzo, na kwa kawaida hujumuisha taarifa za msingi kama vile watetezi, malengo, miradi lengwa ya wiki, kalenda ya matukio, ukumbi na ukurasa wa usajilikwa washiriki wanaovutiwa.
  • Kwa matukio ya mara kwa mara: Waandaaji huwa wanatumia ukurasa wao wa awali wa tukio wenye masahihisho madogo kuhusu malengo yake mapya, shabaha zake na ukurasa mdogo wa kujiandikisha kwa tukio jipya zaidi.
  • Kwa matukio ya kimataifa au ya matukio mengi ya Wiki : Waandaaji wa kampeni ya maudhui duniani huunda kurasa za matukio kwenye Meta-Wiki na nafasi ya ziada ya kualika washirika na waandaaji binafsi kuandaa tukio kama hilo, ushauri kuhusu zana zipi zinaweza kutumika kufuatilia maendeleo, viungo vya miongozo ya jinsi ya kupata kazi mahususi za uhariri na ukurasa unaounganishwa na matukio mengine ya ndani.

Waandalizi wa ndani kwa kawaida husafirisha na kutafsiri ukurasa wa tukio la kimataifa kutoka Meta-wiki hadi miradi yao ya ndani ya wiki, na kuongeza kurasa za usajili na taarifa za ziada zinazohusiana na tukio lao mahalia.

Je, ni matatizo gani ya sasa ya kurasa za tukio?

  • Kwa waandaaji, inaweza kuwa ngumu na kitendo cha kufadhaisha kuunda kurasa: Kwa sasa, waandaaji kwa kawaida huhitaji kuunda kurasa zenye maandishi ya wiki, violezo, na chaguo zingine zozote zinazopatikana kwao. Tatizo ni kwamba wanaunda ukurasa wa tukio na kihariri ambacho kinakusudiwa kuunda makala ya ensaiklopidia, ili wasiwe na zana muhimu zaidi au angavu. Matokeo yake, waandaaji mara nyingi hutumia muda mwingi kuunda kurasa za matukio, na mafanikio ya bidhaa ya mwisho inategemea uzoefu wa mratibu. Kurasa zingine zinaweza kuonekana kama vile mratibu alipendezesha, ilhali zingine zinaweza kuwa na kasoro sana, lakini mratibu hajui jinsi ya kuziboresha.
  • Kwa washiriki watarajiwa, mara nyingi hawavutii, hawaaliki, au hawavutii: Kurasa nyingi za matukio huonekana kama makala za Wikipedia zilizorekebishwa, zaidi au kidogo. Hili sio kosa la mratibu; ni kile ambacho kwa kawaida kinawezekana kwa waandaaji kwa sasa. Hata hivyo, matokeo ya mwisho ni ukurasa ambao kwa kawaida haushawishi wala kuvutia sana, hasa kwa wageni kwenye Wiki ambao hawaelewi ugumu wa jumuiya na desturi za Wikimedia.
  • Kwa washiriki watarajiwa na waangalizi katika vuguvugu kubwa la Wikimedia, maono na athari sio wazi kila wakati: Kwa wageni ambao hawajui dhana kama vile edit-a-thons, dira na malengo ya tukio huenda yasieleweke kuwa wazi. Wanaweza kuona ukuta wa maandishi na wasielewe dhana kwa urahisi kama vile: tukio linalenga wageni, tukio hutoa mafunzo, tukio linakusudiwa kuhusisha na kufurahisha, n.k. Kwa waandaaji wenye uzoefu zaidi, wito mahususi wa kuchukua hatua na athari inayokusudiwa ya tukio pia inaweza kuwa wazi katika baadhi ya kesi, kulingana na jinsi mratibu miundo ukurasa na yaliyomo.

Ni nini athari ya matatizo haya kwenye kurasa za matukio?

Kutokana na matatizo haya ya kurasa za matukio, baadhi ya yafuatayo yanaweza kuwa yanatokea kwenye wiki sasa:

  • Waandaaji mara nyingi hutumia muda mrefu sana kuunda kurasa za matukio, ambayo huchukua muda wao ambao unaweza kuutumia vyema kwa mambo mengine (kama vile kutengeneza maudhui ya programu, kutangaza tukio, n.k.)
  • Huenda waandaaji wakahisi kuchanganyikiwa na kuchoshwa, na huenda wasiweze kuanzisha matukio katika siku zijazo
  • Kwa kuwa hakuna kurasa au miundo ya tukio iliyosanifiwa kwa waandaaji kurejelea, kila mratibu anahitaji "kubuni upya muundo" na kuunda ukurasa wao wa tukio, ambayo ina maana kwamba wanaweza kukosa baadhi ya miundo au mazoea ya manufaa ambayo laiti wangelijua wangependa kufanya.
  • Waandalizi wa hafla mara kwa mara huhisi kulazimishwa kubuni kurasa za matukio nje ya mfumo ikolojia wa Wikimedia, hivyo kufanya iwe vigumu kwa wanajamii kwenye Wiki kuona matukio na kuelewa malengo na mbinu zao za kuchangia. Hii inaweza kusababisha mzozo kati ya jumuiya za kwenye wiki na waandaaji.
  • Washiriki watarajiwa wanaweza kukatishwa tamaa ya kuamua kujiandikisha kwa ajili ya matukio, kwa kuwa kurasa za tukio zinaweza kuonekana za kutisha, zisizoalikwa, au zisizoeleweka kulingana na malengo.
  • Watu wanaojiandikisha kwa ajili ya matukio wanaweza kuwa na uwezekano mdogo wa kuhudhuria matukio kwa vile hawakuhisi kuhamasishwa au kuchochewa na ukurasa wa tukio.
  • Matukio yakishakamilika, inaweza kuwa vigumu zaidi kwa Wana Wikimedia kuelewa maono yao, malengo, au athari kwa sababu ya habari isiyotosheleza au muundo wa kutatanisha wa ukurasa.

Je, mradi huu unawezaje kuboresha hali hii kwa waandaaji?

  • Ufanisi zaidi katika utendakazi wa waratibu: Tunataka kurahisisha waandaaji kuunda kurasa za tukio. Mratibu anaweza kujaza fomu yenye taarifa kuhusu tukio, kisha ukurasa unaweza kuzalishwa kiotomatiki ambao una vipengele vingi vya kawaida vya ukurasa wa tukio.
  • Ujumuishaji na zana ya usajili wa tukio: Mratibu atakuwa na chaguo la kutumia zana ya usajili wa tukio kwenye ukurasa wao wa tukio. Kwa njia hii, wanaweza kuruhusu washiriki kujiandikisha kwa ajili ya tukio kwa urahisi. Vipengele vingine vya kipengele cha usajili wa tukio ni pamoja na uwezo wa washiriki kujiandikisha hadharani au kwa faragha na uthibitisho wa kiotomatiki unaotumwa kwa washiriki.
  • Kuunganishwa na Dashibodi ya Mipango na Matukio: Ikiwa mwandalizi atachagua kutumia zana ya usajili wa tukio, washiriki wote waliosajiliwa hadharani wataongezwa jina lao la mtumiaji kwenye tukio la dashibodi lililoundwa na mwandalizi. Mratibu pia anaweza kuwa na kiungo cha tukio la dashibodi kuonyeshwa kwenye ukurasa wa tukio kupitia mchakato wa kuunda tukio.
  • Utumiaji ulioboreshwa kwa washiriki: Watu wanaokuja kwenye ukurasa wa tukio wataweza kuelewa kwa urahisi zaidi kuwa ukurasa huo ni ukurasa wa tukio (sio makala ya Wikipedia) na wanaweza kuhisi kuhamasishwa zaidi au kufurahishwa na ukurasa. Kwa hivyo, wanaweza kuwa na uwezekano mkubwa wa kujiandikisha kwa tukio, kushirikisha kurasa za tukio kwenye mitandao yao, na kuhudhuria matukio hayo.
  • Uwazi zaidi kuhusu matukio ndani ya vuguvugu la Wikimedia: Kwa sasa, baadhi ya waandaaji wanachagua kutounda kurasa za matukio kwenye wiki. Wakati mwingine hii ni kwa sababu hawajisikii vizuri kuunda kurasa za tukio, au wana wasiwasi kwamba kurasa za tukio wanazounda zinaweza kuwa zisiwaalike wageni. Iwapo tunaweza kuboresha mchakato wa kuunda kurasa za matukio, basi tunaweza kuwa na kurasa nyingi za matukio kwenye wiki na kwa hivyo kutoa uwazi zaidi kama harakati kuhusu matukio yote yanayotokea na athari zake (kama vile viwango vya ushiriki, michango, n.k.) .
  • Muunganisho wa siku zijazo na orodha za kazi: Katika siku zijazo, timu ya Kampeni ingependa kuzindua mradi unaoangazia orodha za kazi za matukio. Hasa, tunataka kuboresha mchakato wa kuunda orodha za kazi za matukio. Baada ya kufanyia kazi mradi huu, tunaweza kutafuta njia za kujumuisha mchakato wa kuunda orodha ya kazi katika mchakato wa kuunda tukio la jumla.

Maswali huria

Asante kwa kusoma uchambuzi wetu. Sasa tunataka kusikia kutoka kwako! Tunaomba ujibu maswali yaliyo hapa chini (au utushirikishe maoni mengine yoyote!) kwenye ukurasa wa mazungumzo ya mradi:

  1. Una maoni gani kuhusu mpango wetu wa kuunda mfumo wa kuunda matukio? Je, unafikiri itakuwa na manufaa kwako, kama mratibu/mshiriki wa tukio?
  2. Una maoni gani kuhusu uchanganuzi wetu wa michakato ya sasa ya kuunda hafla? Je, tunakosa chochote muhimu kwako?
  3. Ikiwa wewe ni mwandalizi wa hafla, kwa kawaida huwa unaunda vipi kurasa za matukio sasa? Je, ni nini na hakifanyi kazi vizuri kwenye mfumo wako wa sasa? Ikiwa ungeweza kubadilisha jambo moja kuhusu hilo, lingekuwa nini?
  4. Ikiwa tutaunda zana ya kuunda tukio, ungependa ifanyeje kazi? Tafadhali toa maelezo mengi kutoka kwa yale ungependa yatendeke au, ikiwa unayo mifano kutoka kwa zana zingine za usajili ambazo umetumia hapo awali!
  5. Je, kuna kitu kingine chochote ungependa kuongeza?

Maoni yako ni muhimu sana kwetu na yataathiri moja kwa moja chaguzi tunazofanya kama timu. Asante, na tunatarajia kusoma maoni yako!