Jump to content

Mwongozo wa Kimataifa wa Mwenendo na Maadili/Mazungumzo/Jopo la Maswali na Majibu ya 2023

From Meta, a Wikimedia project coordination wiki
This page is a translated version of the page Universal Code of Conduct/Conversations/Panel Q&A 2023 and the translation is 100% complete.

Timu ya Sera ya Uaminifu na Usalama ya Wikimedia Foundation itakuwa ikiandaa Jopo la Maswali na Majibu na wanajamii tarehe 15 Januari 2023 katika xx UTC ili kujadili Miongozo ya Utekelezaji wa Mwongozo wa Kimataifa wa Mwenendo na Maadili (UCoC) na hitaji la kuhusika kwa jamii katika upigaji wa kura ya Uidhinishaji ujao. Lengo maalumu la tukio litakuwa kuhusu kwa nini ni muhimu kwa jamii ndogo na za kati za Wikimedia kushiriki katika kura ya uidhinishaji.

Wanajopo ni: Uzoma Ozurumba, Tanveer Haasan, Ruby Damenshie-Brown, na Claudia Lo.

Tukio hili ni sehemu ya juhudi zetu za kushirikisha, kuelimisha na kufahamisha jamii ya Wikimedia kuhusu UCoC, Miongozo ya Utekelezaji na pia kura inayokuja ya Kuidhinishwa kwa Miongozo ya Utekelezaji Iliyorekebishwa.

Tunakuomba uwaalike watu wengine wa kujitolea katika jamii yako ili kuwafahamisha na kuwezeshwa kupiga kura! Tafadhali jiandikishe hapa au utume barua pepe kwa ucocproject@wikimedia.org ikiwa ungependa kuhudhuria.