Kampeni/Timu ya Bidhaa ya WMF/Usajili

From Meta, a Wikimedia project coordination wiki
This page is a translated version of the page Campaigns/Foundation Product Team/Registration and the translation is 89% complete.
Outdated translations are marked like this.
Community Content Campaigns

Kuna kampeni nyingi katika harakati za Wikimedia, kama vile Wiki Loves Monuments, WikiGap, #1Lib1Ref, na nyingine nyingi. Japokuwa, hakuna mfumo imara upatikanao mtandaoni katika kurasa za Wiki kwaajili ya kuratibu matukio. Kwa sababu hii, Timu ya Kampeni inalenga kutengeneza njia rahisi ya kujiunga na kampeni za Wikimedia.

Tunakualika kusoma uchambuzi hapa chini na utoe mrejesho wako katika ukurasa wa majadiliano. Mrejesho/maoni yako yataleta tija ya moja kwa moja kuhusu uelekeo wa mradi wetu. Tunatanguliza shukrani zetu kwa ushiriki wako!

Moano ya Mradi

Kwa kuwa na mfumo huu mpya, waratibu wa kampeni wataokoa muda, kwakuwa hawatalazimika tena kutengeneza njia mbadala za kuwaandikisha watu katika kampeni husika. Pia, watakuwa na uwezo wa kukusanya data nzuri kuhusu washiriki wa kampeni zao na mahitaji ya washiriki huku wakiheshimu faragha ya washiriki. Wkati huo huo, washiriki wa kampeni watakuwa na uwezo wa kujiunga na kampeni kiurahisi, na sehemu yao ya kwanza kuanzisha mawasiliano itakuwa kwa namna ya kufurahisha na kuhamasisha!

Tuna mipango mikubwa hapo mbeleni kuhusu suala la kujiandikisha. Kwanza, tunatarajia kuunganisha mfumo wa kujiandikisha na programu ambazo tayari zipo za kuratibu miradi, kama vile Programs & Events Dashboard na Event Metrics. Hii inamaanisha kwamba, baada ya wahiriki kuwa wamejiandikisha, majina yao ya mtumiaji yatajiongeza moja kwa moja katika program husika ya kuratibu miradi ambayo itakuwa imechaguliwa na mratibu wa tukio husika.

Pili, tunatumaini kuwa siluhisho la kuwa na mfumo wa kimtandao wa kujisajili katika tovuti za wiki inaleta mantiki ya kukuza jamii. Kwa sasa, washiriki wengi wa kampeni hawajui nani pia kajisajili kuhudhuria tukio fulani, hususani ikiwa wamejisajili kupitia mifumo mingine tofauti na tovuti za wiki. Tukiwa na suluhishi hili la kuwa mfumo huu mpya wa kujisajili, washiriki wanaweza kuona nani amejiunga na kampeni fulani na kuhusu nani ana maslahi na motisha zinazofanana na watu wanaotaka kujiandikisha kupitia mfumo huo.

Tatu, tunatazamia mfumo wa usajili kuwa sehemu ya jukwaa ya tukio kubwa zaidi katika siku zijazo. Mfumo huu unaweza kujumuisha vipengele vya ziada vya waandaaji na washiriki, kama vile zana ya kuunda matukio na kalenda ya kimataifa ya matukio ya Wikimedia. Baada ya kuunda usajili, tunaweza kutumia zana kama msingi wa miradi na vipengele vya baadaye kwenye jukwaa.

Mwisho, tunataka mradi huu uwe shirikishi kwa kiwango kikubwa iwezekanavyo. Wakati wa maandalizi ya mradi huu, tuliwasiliana na takribani waandaaji/waratibu wa matukio 50. Tunapenda kutoa shukrani za dhati kwa waratibu hawa, ambao walitupa kuelewa mkubwa kuhusu uzoefu wao na changamoto kubwa wanazokumbana nazo katika kuandaa matukio. Sasa, tunawaalika waandaji wa matukio wote kutoa maoni yao katika ukuraasa wa majadiliano wa mradi huu.

Kwanini tunataka kuboresha uandikishaji

Tunaamini kwamba kujiandikisha ni chaguo muhimu la mradi kwa timu yetu kwa sababu zilizoorodheshwa hapa chini.

  1. Kwa sasa hakuna mfumo rasmi kwenye tovuti za wiki. Harakati za Wikimedia zinahitaji mfumo imara wa kujiandikisha ambao umesanifiwa kukidhi mahitaji yake.
  2. Njia mbadala wanazotumia waratibu wa matukio zina changamoto nyingi zana, ikiwemo:
    • Kutumia muda mrefu na ni kazi ya kuchosha kwa waratibu wa matukio kusanidi na kuratibu.
    • Uhaba wa data.Inatoa taarifa chache kuhusu mahitaji ya washiriki na inaleta ugumu kwa waratibu kuelewa nani alishiriki katika matukio yapi.
    • Changamoto za kiufundi na kuwachanganya washiriki wapya
    • Ugumu wa washiriki kuhariri taarifa zao baada ya kujiandikisha
    • Kutokuwa na uwezo wa kudhibiti matokeo ya mtu mmoja kujiandikisha zaidi ya mara moja.
    • Hazijatengenezwa kukidhi matakwa ya lugha nyingi kwaajili ya jamii za aina tofautitofauti.
    • Kutokuwa na uwezo wa kulea mantiki ya jamii na ujumuishwaji baina ya washiriki.
    • Kuwa na mgogoro na maadili ya Wikimedia (mf. nyenzo zilizo nyingi zinamtaka mtu kutoa taarifa za faragha kwa watu/makampuni mengine )
    • Hazijaunganishwa na kurasa zozote/majukwaa yoyote ya Wiki, na hivyo kuongeza ugumu zaidi kwa washiriki wapya.
    • Hazijaundanishwa na mifumo iliyopo ya ufuatiliaji/uratibu wa miradi kama vile ule wa Dashibodi ya Mipango na Matukio (Programs & Events Dashboard)
  3. Waratibu, washirika, na wadau wengine wa harakati wanahitaji taarifa nzuri zaidi kuhusu washiriki na mahitaji yao. Kuunda mfumo wa kujiandikisha ni hatua moja katika kulifanikisha hili.
  4. Usajili ndio msingi wa kazi ya baadaye. Baada ya kuboresha usajili, tunaweza kuanza kuongezea/kuunganisha vitu vingine katika uendeshaji wa kampeni, kama vile kuboreka kwa programu za kuratibu miradi na kuboreka kwa nyenzo za mwasiliano.
  5. Mradi unaweza kutekelezwa na upo ndani ya wigo wa utekelezaji wa timu.

Karibia kila mratibu wa matukio tuliyeongea nae amesanifu mfumo wake wa kujiandikisha. Baadhi ya mifumo hiyo imeigwa kutoka kwa waratibu wengine na baadhi yake inatokana na uzoefu wa zamani wa uratibu wa matukio.Nyingine zimeundwa kulingana na mahitaji maalum ya kiufundi. Lengo letu si kubuni mfumo wa kwanza wa usajili, lakini kutoa suluhu iliyoboreshwa ambayo husaidia kuunda mtiririko thabiti wa waandaaji katika miktadha tofauti.

Namna ambavyo ujiandikishaji katika jampeni unavyofanya kazi

Tumetambua njia kadhaa ambazo zinatumika kwa sasa zimekuwa zikitumika katika uandikishaji ambazo ni:

Njia za kujisajili katiki Wiki

Kuongeza majina ya watumiaji wewe mwenyewe

Baadgi ya njia za kujiandikisha zinawataka washiriki kuongeza majina yao ya mtumiaji wao wenyewe au saini katika majukwaa ya wiki. Kwa mfano, angalia matukio ya Wiki for Human Rights 2021 in Morocco au Women in Red katika picha hapa chini. Faida ya njia hii ni kwamba imeunganishwa kwenye utendaji kazi uliopo tayari katika Wiki, na taarifa kuhusu waliojiandikisha zinaatikana hadharani (mfano). Hasara ni kwamba inatoa taarifa finyu kwa waratibu kuhusiana na mahitaji ya washiriki, na sio rafiki kwa washiriki wapya.

Washiriki waliombwa kuongeza majina yao wenyewe katika mradi wa Wiki for Human Rights huko Morocco
Sehemu maalumu ya washiriki, ambapo watumiaji wanaongeza wao wenyewe saini zao, kwaajili ya mradi wa Women in Red Agosti 2021.

Maungano ya kiufundi

Baadhi ya waratibu wameunda njia za kiufundiza kutatua suala za ujiandikishaji. Kwa mfano, CEE Spring ina bot inayoweza kufanya kazi katika lugha mbalimbali na inaweza kukusanya data katika miradi kadhaa katika eneo husika. Mradi wa Al Maarifa Project unamtaka kila mtumiaji kutengeneza ukurasa mdogo ambao baadae utatumika na programu nyingine. Nyenzo hizi zinaweza kuwa na manufaa kwa baadhi ya kampeni, lakini ni vigumu watu wengine kuzitumia au kuzitumia tena kwa baadhi ya jumuiya. Pia zinategemea kutengenezwa na wajitoleaji wenye uelewa wa kiufundi kuhusu suluhu hizo, ambao baada ya muda husimama kuendelea kutengeneza nyenzo hizo, na hivyo kutengeneza changamoto kuhusuiana na msaada wa kudumu wa masuala ya kiufundi kuhusu nyenzo hizo.

Suluhu za umiliki nje ya majukwaa ya Wiki

Mifumo ya kujiandikisha kutoka sehemu nyingine

Baadhi ya waandaaji wa matukio hutumia fomu za kujiandikishia kutoka makampuni mengine kama vile fomu za Google ili kuwaandikisha washiriki. Faida ni kwamba, fomu hizo ni rahisi kwa waratibu wa matukio kuunda na washiriki kuzijaza. Changamoto yake ni kwamba hazijakubalika kutumika katika utendaji kazi wa Wikimedia, na zina utofauti wa sera kuhusu faragha na elimu huria. Washiriki pia hawawezi kuona taarifa za waliojiandikisha, kwa hivyo wana uelewa mdogo wa namna wanavyoweza kuunganishwa na wale waliojiandikisha. Pia, nyenzo hizo hazikidhi matakwa ya lugha kiulimwengu na kuzingatia tamaduni mahalia. Kwenye jumuiya zizungumzazo lugha ndogo au wale ambao wapo hatarini, nyenzo hizi maranyingi zinaonesha changamoto kutumia katika hali ya ujumuishi na usalama.

Kwa mfano, tukio la mradi wa Mwezi wa Historia ya Watu Weusi (Black History) Celebrate Women Leaders in the African Diaspora ulioratibiwa na Wikimedia Nigeria, African Women on Board, na AfroCROWD, walitumia fomu ya Google kwa usajili wa washiriki.Angalia mfano wa picha ya skrini hapa chini.

Maelekezo ya kujisajili kwenye mradi wa Black History Month katika kukurasa waa Wanawake viongozi, ambao unawaelekeza watumiaji kwenye Google fomu.

Majukwaa ya usajili kutoka maeneo mengine=

Baadhi ya Kmapeni zinatumia majukwaa mengine kuwasjili washiriki wao, kama vile Eventbrite au Meetup. Faida ni kwamba majukwaa haya yanatoa huduma yenye utajiri wa vitu vingi ndano yake na ni huduma zinazoweza kuasiliwa. Hasara ni kama tu zile za kutumia fomu za kujiandikishia kutoka makampuni mengine.

Kwa mfano, picha ya skrini hapa chini, warsha ya kuandika makala ya Vaccine Safety Edit-a-thon, iliyortibiwa na Wikimedia District of Columbia na Wikimedia Mexico, ilitoa kiungo kuelekeza kwenda register on Eventbrite.

Ukueasa wa tukio ambapo kiungo kinaelekeza kwenda kwenye ukurasa wa usajili wa Eventbrite

Programu zilizoundwa kwaajili ya ufuatiliaji wa kampeni

Dashibodi ya Programu na Matukio

Dashibodi ya Programu na Matukio, ilitengenezwa na Wiki Education Foundation, ni programu ya kufuatilia miradi. Baadhi ya waratibu wanatumia programu kutoka makampuni mengine,baadaye usajili katika dashibodi. Kwamfano, (picha ya skrini hapa chini), unaweza kuona hizi hatua katika mradi wa Africa Wiki Challenge. Kwa upande mwingine, waratibu wa matukio hutumia dashibodi kama njia yao pekee ya usajili.

Faida ya Dashibodi ni kwamba ni nyenzo inayotoa takwimu, kwa hiyo tayari imeunganishwa na ufuatiliaji. Hasara ya kwanza ni kwamba kimsingi dashibodi si programu ya kujisajili. Inatoa taarifa chache kuhusu washiriki kwa wanaoratibu matukio, na inatoa usaidizi finyu kwa washiriki. Pia, dashibodi haitumiki kama programu ya kupima maendeleo ya kampeni zote, na ndio maana baadhi ya kampeni hupendelea programu fuatiliaji tofauti na dashibodi.

Maelekezo ya namna ya kushiriki kama yalivyotolewa katika ukurasa wa mradi wa Africa Wiki Challenge

Fountain

Fountain (documentation), iliundwa na Le Loy, ni programu fuatiliaji ya miradi inayotumika na baadhi ya kampeni, kama Wikipedia Asian Month. Faida na hasara ni zilezile kama zilizopo kwenye matumizi ya Dashibodi ya Programu na Matukio. Vilevile nyenzo hii kama ilivyo kwa mfumowa kujiandikishia katika wiki, una changamoto kwa washiriki wapya na inawafaa zaidi wachangiaji wazoefu.

Mfano wa kutumia nyenzo ya Fountain katika kutafuta kampeni zinazohusiana na "wanawake"

Hakuna usajili rasmi

Baadhi ya kampeni hazina mchakato wa kujiandikisha, badala yake wanawafuatilia washiriki kwa kutumia njia fulani fulani katika utendaji kazi kwenye wiki

Usajili kwa njia ya kupakia

Hii inatumika sana kwa mashindano ya picha, kama vile Wiki Loves Monuments au Wiki Loves Folklore, ambapo usajili unakuwa umeshaunganishwa kwenye mchakato ufuatiliaji. Pale mmoja anapopakia picha na na kuitambulisha kwaajili ya ufuatiliaji katika kampeni husika, wanakuwa washajiandikisha. Mfumo huu hufanya kazi kwa baadhi ya kampeni, lakini sio mfumo wenye matumizi kwa aina zote za kampeni, hususani kwa wale wanaowalenga washiriki wapya katika kuandika makala. Lakini pia haiukusanyi taarifa zaidi za washiriki, ambapo inaweza kusababisha changamoto katika mawasiliano na ufuatiliaji.

Mfano wa picha ya skrini ikionesha programu ya Upload Wizard inayotumika kwaajili ya Wiki Loves Monuments (baada ya kumalizika)

Usajili kwa njia ya Hashtag

Kwa kampeni za #1lib1ref na Wikipedia Pages Wanting Photos (#WPWP) pamoja na shughuli chache zinazofanyika katika programu zingine, Hashtags Tool inatumika kama nyenzo msingi ya kujiandikisha. Kama vile ilivyo kwa mchakato wa kupakia, kuna faida kwamba inadaka data zilizochangiwa. Ingawa, kwakuwa hashtags huwa hazijaunganishwa kwenye mwonekano wa kuhariri, ni vigumu kwa washiriki wapya kuelewa kitendo cha kuongeza hizo hashtags na hata wachangiaji wapya wanaweza kusahau kuongeza hashtag kwasababu si kitu wanachofanya mara kwa mara katika shughuli zao za kila siku. Zaidi ya hayo, ni vigumu kwa waratibu wa matukio kufuatilia maendeleo ya mradi fulani kwa wakati huo huo, na hakuna taarifa inayotolewa moja kwa moja kuhusu washiriki na mahitaji yao.

Mfano wa kutumia hashtag katika sehemu ya Muhtasari wa uhariri, ambapo kitendo hicho hutumika baadaye kufuatilia shughuli iliyofanyika kupitia nyenzo ya hashtag
Nyenzo ya hashtag, ambayo inaweza kutumika kutafuta hariri kutokana na hashtag zilizotumika

Maswali huria

Asante kwa kusoma uchambuzi wetu. Sasa tunataka kusikia kutoka kwako! Tunaomba ujibu maswali yafuatayo hapa chini (au tushirikishe maoni yako yoyote yale)

  1. Unaonaje kuhusiana na mpango wetu wa kutengeneza Mfumo wa Usajili katika Kampeni? Unadhani utakuwa na manufaa kwako, kama muandaaji/mratibu wa matukio au kama mshiriki?
  2. Unaonaje uchambuzi wetu kuhusiana na mchakato wa sasa wa usajili? kuna tuliochosahau ambacho ni cha muhimu kwako?
  3. Kama wewe ni mratibu wa matukio, njia gani ya usajili wa washiriki wako unaitumia? Kipi kinafanya kazi vizuri na kipi hakifanyi kazi vizuri kwenye huo mfumo? Kama ungeweza kubadili kitu kimoja kuhusu mfumo huo, kitu hicho kingekuwa kitu gani?
  4. Kama tukitengeneza mfumo wa usajili, ungependa mfumo huo ufanyeje kazi? Tafadhali elezea kwa undani kadri uwezavyo kulingana na vile ungependa mfumo huo ufanye kazi, au kama tayari unayo mifano kutoka katika programu zingine za usajili ulizowahi kuzitumia hapo kabla!
  5. Sisi ni timu mpya (angalia Ukurasa wetu mpya). Una matumaini gani, maswali, au dukuduku kuhusu timu yetu?
  6. Kuna kingine chochote ungependa kuongeza?

Maoni yako ni muhimu sana kwetu na yatakuwa na mchango wa moja kwa moja kuhusu vipaumbele tutakavyovitekeleza sisi kama timu. Asante , na tunatazamia kusoma maoni yako!

Status Updates

Taarifa za Kinachoendelea

November 15, 2023ː Participant Questions released

The Participant Questions feature has been released to Event Registration. With this feature, organizers can now include questions for participants in the registration process if they agree to a clickwrap agreement. The questions are optional for participants to answer, and the response data is displayed to the organizer. Some of the information is Personally Identifiable Information (PII), so it is displayed in the aggregate only. The PII information is the gender identity, age, and profession of the participant. Other information is not PII, so individual responses can be viewed. The non-PII information is the affiliate membership of the participant (if any) and their level of confidence in contributing to Wikimedia projects.

October 7 & 10, 2023: office hours & upcoming features

We would like to invite everyone to our upcoming community office hours on October 7 and October 10, where we will demo the latest version of the Event Registration tool. We will discuss the new, already released features (multiple organizer support and P&E Dashboard integration) and upcoming features (organizer can email participants and optional participant questions).

July 21, 2023: Registration tool now integrated with Programs & Events Dashboard

The event registration tool now supports integration with the Programs & Events Dashboard. This means that an organizer can specify the link to their Programs & Events Dashboard event when they configure registration. Then, usernames of publicly registered participants are automatically sent to the specified event on the Programs & Events Dashboard.

April 27, 2023: Registration tool now allows multiple organizers

The event registration tool now includes support for more than one organizer (T325101).

December 5, 2022: Office hours and feedback requested

Now that we have enabled the CampaignEvents extension on Meta-Wiki, we would like to invite everyone to our upcoming office hours and to share their feedback on the tool, either on our project talk or in a survey (which is available in Arabic, English, French, and Swahili).

During the office hours, we will demo the tool, answer any questions people may have, and share how people can test the tool on either test wikis (such as the beta cluster, testwiki, or test2wiki) or with real events on Meta-Wiki. The office hours dates and times are:

Session 1:

Session 2:

We hope you can join us!

Additionally, we want to hear your feedback. You can share your feedback on the project talk page, in our V1 feedback survey, or by reaching out to team members directly. The survey and the project talk pages have the same questions, which are available in four languages (Arabic, English, French, and Swahili). Thank you!

November 30, 2022: Meta-Wiki release

We have enabled the CampaignEvents extension on Meta-Wiki, which we will demo in the upcoming office hours.

November 3, 2022ː Test wikis release & other updates

We have enabled the CampaignEvents extension on testwiki and test2wiki. This now means that you can test out the tool on these two wikis, in addition to the beta cluster.

Additionally, we have updated our release schedule. Our next release plan is to enable the CampaignEvents extension on Meta-wiki, roughly scheduled for the end of November. You can check out our release plan page for the latest details.

We have written a comprehensive guide on the event registration tool, which will be updated as we release new features for the tool. Additionally, we have posted a blog post on Diff related to our work and plans in Arabic, English, and French.

If you have any feedback on our latest updates, please share them on the talk page. Thank youǃ

Oktoba 3, 2022: Mafunzo ya V0 na uzinduzi wa V1

Habarini nyote! Tuna masasisho mengi ya kuwashirikisheni, yakiwemo:

  • Muhtasari wa mafunzo tuliyopata kwenye awamu yetu ya jaribio la V0
  • Sasisho juu ya uzinduzi wa kazi ya V1
  • Maswali huria tuliyo nayo kwa wanaojitolea na wanajamii

Tafadhali soma hapa chini ili kujifunza zaidi, na tunatazamia kusoma maoni yako 'kuhusu ukurasa wa mazungumzoǃ

Mafunzo kutokana na V0

Mnamo Julai 2022, tulizindua V0 kwenye jukwaa la beta. Tulikusanya maoni kuhusu V0 katika miundo mbalimbali, ikiwa ni pamoja na: Fomu ya Google, mawasilisho kwa lugha nyingi saa za kazi na Wikimania, majadiliano kwenye ukurasa huu wa mradi, mawasiliano katika vikundi vya mitandao ya kijamii nje ya wiki, na barua pepe zilizotumwa kwetu moja kwa moja. Watu walitoa majibu katika Kiarabu, Kiingereza, Kifaransa, Kireno, na Kiswahili. Kwa jumla, tulisikia kutoka kwa zaidi ya Wanawikimedia 30 .

Tulipokea maoni mengi mazuri kuhusu V0. Kwa mfano, tulipowauliza watu kama wangetumia zana, zaidi ya 80% ya swali walisema ndiyo. Tulipowauliza waandaaji matukio ya Wimedia ikiwa ufikiaji wa zana utawafanya wawe na uwezekano mkubwa wa kuandaa matukio katika siku zijazo, 90% ya washiriki walisema ndiyo. Baadhi ya aina za kawaida za maoni chanya zilijumuisha: zana ilikuwa angavu na rahisi kutumia, ingeokoa muda kwa waandaaji, na ingeboresha uwezo wa waandaaji kukusanya taarifa za washiriki. Kwa kuwa hili ni toleo la awali la majaribio (na tunapanga kutoa viboreshaji zaidi katika matoleo ya yajayo), ilisisimua sana kwa timu kusikia kwamba hata toleo hili lilifurahisha Wanawikimedia wengi.

Pia tulipokea taarifa kuhusu jinsi tunavyoweza kuboresha zana ya usajili wa tukio. Baadhi ya watu walisema kwamba tayari walikuwa na suluhu za usajili walizopendelea au walitaka kutumia zana baada ya kuwa na muda zaidi wa kuifanyia majaribio. Pia tulipokea maombi mengi ya vipengele. Hapo chini, tumeshirikisha orodha ya maombi na dokezo la lini tunapanga kutekeleza kipengele, ikiwa tutakuwa na mipango yoyote:

  • Kuunganishwa na Dashibodi ya Mipango na Matukio (umepangwa kutekelezwa kwenye V1)
  • Uwezo wa waandaaji wengi kuhusishwa na tukio (umepangwa kutekelezwa kwenye V1)
  • Msaada wa kuweka jiografia (umepangwa kutekelezwa kwenye V1)
  • Barua pepe za uthibitishaji kutumwa kiotomatiki kwa washiriki baada ya washiriki kujiandikisha (umepangwa kutekelezwa kwenye V1)
  • Barua pepe za vikumbusho vya matukio kwa washiriki (tutakuwa tunaunda uwezo wa waandaaji kutuma barua pepe kwa washiriki katika V1; barua pepe za vikumbusho otomatiki bado hazipo kwenye mpango, lakini tunaweza kuzizingatia baadaye)
  • Uwezo wa kuweka mipaka kwa idadi ya washiriki (umepangwa kutekelezwa kwenye V2)
  • Msaada wa kuunda kurasa za tukio (umepangwa kwa mradi wa siku zijazo unaozingatia uundaji wa tukio)
  • Mfumo wa kalenda ya matukio ulioboreshwa (umepangwa kwa mradi wa siku zijazo unaozingatia kalenda ya tukio na/au usaidizi wa ukuzaji wa hafla)

Mapendekezo haya yalikuwa ya muhimu sana kwetu, na tunapanga kujumuisha mengi yao kama vipengele katika toleo la V1 na V2. Kwa hivyo, kwa kusema hivyo, unaweza kusoma mchanganuo kamili wa maoni ya V0 na muhtasari wa mwisho wa kazi ya V0.

Uzinduzi wa V1

Sasa tumeanza rasmi kufanyia kazi V1 ya zana ya usajili wa tukio. Wahandisi kwa sasa wanafanya kazi katika kujenga vipengele vya msingi na uboreshaji wa V1. Bado hatujaweka tarehe mahususi ya kutolewa, lakini tutakapofanya hivyo, tutahakikisha kuwa tunasasisha ukurasa wa toleo. Hata hivyo, tunaweza kukufahamisha kwamba baadhi ya maboresho ya vipengele vya msingi katika V1 ni pamoja na:

  • Usaidizi kwa muandaaji watukio kubainisha saa za eneo
  • Msaada wa kijiografia
  • Barua pepe za uthibitishaji kiotomatiki baada ya washiriki kujiandikisha
  • Uwezo wa mratibu kutuma barua pepe kwa washiriki (kama watatumia barua pepe zinazohusiana na akaunti zao)
  • Kuunganishwa na Dashibodi ya Mipango na Matukio
  • Uwezo wa waandaaji wengi kuhusishwa na tukio
  • Usajili wa kibinafsi: chaguo la washiriki kujiandikisha na kuonyesha tu jina lao la mtumiaji lililosajiliwa kwa waandaaji wa hafla

Ili kupata maelezo zaidi kuhusu maono yetu ya V1, tunakualika uangalie V1 muhtasari wa ukurasa mdogo, ambao unaweka kazi yetu kwa undani zaidi.

Maswali huria

  • Kwa sasa tunafanyia kazi V1 ya zana ya usajili wa tukio. Unaweza kuangalia muhtasari wetu wa mradi. Je, kuna jambo lolote ungependa kutushirikisha kuhusu mpango huu, au jambo lolote unalopendekeza tufanye kwa njia tofauti?
  • Katika siku zijazo, ni nani anayepaswa kufikia zana zetu za kupanga matukio? Kwa maneno mengine, mtu anawezaje kuwa mratibu na mapendeleo fulani kwenye wiki? Kwa mfano, inapaswa kuwa ni kikundi cha watumiaji? Je, inafaa kuwa haki ambayo watu hupokea kiotomatiki baada ya kufanya idadi fulani ya uhariri?
  • Katika siku zijazo, tunapanga kuunda kipengele kwa ajili ya waandaaji kukusanya taarifa kuhusu washiriki. Katika hali hiyo, ni taarifa gani (kama mratibu) ungependa kukusanya kuhusu washiriki kabla ya kujiunga na tukio (kama vile jinsia, eneo, mada zinazokuvutia, n.k)? Je, una mifano yoyote ya fomu za usajili ulizounda zinazouliza baadhi ya maswali haya? Ikiwa ndio, tafadhali tushirikishe nazo!

Tafadhali tushirikishe maoni yako kwenye ukurasa wa mazungumzo; asanteǃ

Tarehe 21 Julai 2022: Fomu ya maoni tayari

Habarini nyote! Sasa tuna [fomu ya maoni https://docs.google.com/forms/d/e/1FAIpQLSe53MNV9CKVBAF3SV2q97baufizH7b_2QJ47H1w0Upvoh4QFQ/viewform]' (inapatikana katika Kiarabu, Kiingereza Kiswahili na Kifaransa) ili watu wawasilishe maoni kuhusu V0 ya zana ya usajili! Tunawaalika nyote kujaza fomu na/au kushirikisha maoni kwenye ukurasa wa mazungumzo ya mradi. Kama ukumbusho, tutakuwa tunaandaa vipindi viwili vya saa za ofisi ya jumuiya ili kutoa mafunzo kuhusu jinsi ya kutumia zana. Kikao cha kwanza kitakuwa leo saa 5pm UTC, na cha pili kitakuwa Julai 23 saa 12 pm UTC.

Tunamshukuru kila mtu ambaye ametoa maoni au kutuunga mkono wakati wowote katika mradi huu, na tunatazamia kujifunza kutoka kwenu nyote wakati wa awamu ya majaribio ya V0! Lengo letu ni kuendelea kuboresha zana kwa awamu mbili zaidi za uchapishaji (V1 na V2), kwa hivyo tutaendelea kusasisha ukurasa huu wa mradi katika mchakato mzima. Kwa sasa, tunatumai kwa dhati utajaza fomu ya maoni na kuhudhuria saa za ofisi ya jumuiya. Tunatazamia kusikia kutoka kwa wengi wenu!

Julai 18, 2022: V0 imezinduliwa kwenye beta

Tuna furaha kubwa sana kutangaza kwamba zana ya usajili sasa inapatikana kwaajili ya majaribio kwenye beta! Unaweza kusoma Nyaraka za Usaidizi kuhusu jinsi ya kutumia zana kwenye Mediawiki.org.

Kama hatua inayofuata, tutakuwa tukitoa mafunzo ya jinsi ya kutumia zana. Kwa sababu hii, tunawaalika wafanyakazi wa kujitolea kukutana na timu na kushiriki katika mafunzo katika mojawapo ya saa zetu zijazo za ofisi ya jumuiya, ambayo yatafanyika Alhamisi, Julai 21 saa 5 pm UTC na/au Jumamosi, Julai 23 saa 12 pm UTC. Unaweza kutembelea ukurasa wa saa za ofisini kwenye Meta-Wiki ili kujiandikisha kwa kipindi kimoja au vyote viwili na upate maelezo zaidi.

Kwa sasa tunakamilisha fomu yetu ya maoni kwaajili ya watu wanaojitolea kuhusu na zana ya usajili. Tutawashirikisha fomu ya maoni katika saa zijazo za ofisi, na tutawashirikisha kwenye ukurasa huu wa mradi hivi karibuni pia. Wakati huo huo, jisikie huru kutushirikisha maoni yako kwenye ukurasa wa mazungumzo, ikiwa ungependa kuangalia zana kabla ya saa za kazi.

Wakati huo huo, asante kwa kila mtu ambaye ameshirikiana nasi kwenye mradi huu hadi sasa, na tunatumai kuwaona wengi wenu katika saa zetu za kazi zijazo!

Julai 8, 2022

Timu inajiandaa kwa ajili ya uzinduzi wa V0 kwa nguzo ya beta ya, ambayo itafanyika hivi karibuni. Tutasasisha ukurasa huu wa mradi wakati toleo litakapotolewa kwenye kundi la beta. Baada ya kuchapishwa, tutakaribisha saa mbili za kazi za jumuiya ili kutoa mafunzo na usaidizi kwa mtu yeyote ambaye angependa kujaribu zana na kushirikisha maoni yao. Kwa taarifa iliyosasishwa zaidi, tafadhali tembelea ukurasa wa Ratiba ya toleo na mafunzo kwa mradi.

Mei 23, 2022

Habarini nyote! Kwanza, asante kwa kila mtu ambaye ameshiriki kutoa maoni yake katika ukurasa wetu wa mazungumzo, wakati wa saa za kazi, au majadiliano kwenye chaneli za mazungumzo ya makundi. Kwakweli maoni na maarifa yako yamekuwa muhimu sana kwa mradi wetu, na tunathamini sana mchango wako. Pia tuna masasisho kemkem (na maswali mapya!), ambayo tutakushirikisha hapa chini:

Masasisho ya uhandisi

Wahandisi wa timu yetu wanaendelea na kazi ya kuunda mfumo wa usajili wa matukio. Wamejenga miundombinu mingi ya msingi, na sasa wamejikita katika kujenga sehemu ya mbele (yaani, muonekano wa mfumo kwa huo mtumiaji). Tunatazamia kuwa toleo la awali linaloweza kufanyiwa majaribio la suluhu la usajili litapatikana kwenye betawiki ifikapo Julai 2022.Ili kujifunza zaidi kuhusu kazi ya wahandisi wa timu yetu, unaweza kuangalia ufafanuzi wa schema yetu kwenye Gerrit.

Masasisho ya Programu-mfano

Tuna Programu-mfano iliyosasishwa, ambayo iliundwa na mbunifu wa timu yetu, ili kuangalia (tazama viungo hapa chini). Mfano huu ni wa Programu-mfano ya V0 (toleo la kwanza la zana ambayo tutakuwa tukitoa matoleo yake). Tafadhali kumbuka kuwa hii ni mifano tu; Si programu ambazo tayari zinafanya wiki moja kwa moja. Programu mfano hizi hutoa hisia ya jumla ya jinsi bidhaa iliyokamilika itakavyoonekana, itakavyodhaniwa na kufanya kazi pindi tutakapotoa suluhu la usajili, ingawa pengine kutakuwa na mabadiliko fulani fulani.

Mpango wetu wa kutoa matoleo

Mpango wetu wa kutoa matoleo: Sasa tuna mpango wa msingi wa kutoa matoleo. Tunapanga kutoa suluhisho la usajili katika sehemu tatu, ambazo tutazielezea hapa chini:

  • V0: Hili ni toleo la zana, ambalo tumejikita kulijenga sasa. Litatolewa hapo baadae kwenye kundi la beta, pengine Julai 2022. Tunaliita V0 kwa sababu ni awamu ya majaribio ambayo hawekwa kufanya kazi kwenye wiki zozote za moja kwa moja (ni kwaajili ya wiki ya majaribio tu). Madhumuni ya toleo hili yatakuwa kukusanya maoni ya watumiaji katika kutayarisha toleo la V1. Katika toleo hili, waandaaji wataweza kuongeza usajili kwenye kurasa za tukio na kuona orodha ya washiriki waliosajiliwa. Hili litakuwa toleo la kwenye Komputa za mezani pekee. Unaweza kutazama programu-mfano kwenye viungo vilivyotolewa hapo juu (angalia "Sasisho za Prototype"):
  • V1: Toleo hili litakuwa uboreshaji wa V0, kwa kujumuisha vipengele zaidi, kama vile: uwezo wa waandaaji kuwasiliana na washiriki, kuunganishwa na Dashibodi ya Mipango na Matukio, na usaidizi wa eneo la kijiografia. Pia tutajumuisha maoni tunayopokea kutoka kwa watumiaji katika awamu ya majaribio ya V0. Toleo hili litaoana na matoleo ya kompyuta ya mezani na ya mtandao wa simu ya wiki, na tunapanga kuliweka kwenye angalau tovuti moja ya wiki ya moja kwa moja (pengine Meta-Wiki). Toleo hili ni uboreshaji mkubwa na mengi ya kujadiliwa, kwa hivyo tutatoa sasisho tofauti la hali ili kukusanya maoni kuhusu mahitaji na mifano ya V1. Unaweza kutarajia sasisho hili la kinachoendelea kwenye V1 litakalochapishwa hivi karibuni.
  • V2: Toleo hili litakuwa uboreshaji wa V1, kulingana na maoni ya mtumiaji na nyongeza ya vipengele zaidi. Hatujatimiza mahitaji kikamilifu, na bado hatuna mfano. Unaweza kutarajia sasisho zaidi kwenye toleo hili la mwisho katika sasisho la lijalo.

Tunaomba maoni yako

Tunataka maoni yako kuhusu tabia ya ukurasa wa tukio: Katika sehemu ya maswali ya wazi, tumeshirikisha baadhi ya maswali kuhusu jinsi matukio na kurasa za matukio zinapaswa kushughulikiwa. Tungependa kusikia maoni yako (tazama hapa chini):

  1. Kwa usajili wa tukio, ni tabia gani inayopendekezwa kwa watumiaji waliozuiwa? Je, watumiaji waliozuiwa wanapaswa kujiunga na matukio ya kampeni? Kama ndiyo kwa nini au kama sio kwa nini? Na je, ni muhimu, kulingana na aina za vizuizi (kama vile kizuizi kigumu, kizuizi laini, n.k)?
  2. Kwa kurasa za tukio katika maeneo ya wwki ya tukio, je, tunapaswa kuruhusu kurasa zihamishwe?
    1. Kama ndio: Je, nini kitatokea ikiwa ukurasa wa tukio utahamishwa hadi kwenye eneo lingine la Wiki na tayari ukurasa wa mwanzo una majina na una washiriki waliojiandikisha?
    2. Ikiwa ndio: Je, tabia/maonyo yanapaswa kuwaje kwa mtumiaji kama anataka kuhamisha ukurasa?
    3. Kama ndio: Je, nini kifanyike ikiwa ukurasa wa tukio utahamishwa hadi kwenye eneo la Wiki ambapo kurasa za tukio haziruhusiwi?
  3. Kwa kurasa za tukio katika eneo la wiki la tukio, je, tunapaswa kuruhusu kurasa hizo kufutwa?
    1. Kama ndio: Nani anafaa kuwa na uwezo wa kufuta kurasa za tukio?
    2. Ikiwa ndio: Je, nini kifanyike ikiwa ukurasa wa tukio utafutwa na una washiriki waliojiandikisha?
    3. Ikiwa ndio: Ikiwa watu wamejiandikisha, nini kifanyike kuhusu data ikiwa ukurasa utafutwa?

Kuna kitu kingine chochote ungependa kuongeza (kuhusu nyenzo-mfano za V0, mpango wa kuzindua, au kitu kingine chochote)?

Tunatanguliza shukrani kwa maoni yako, na tunatazamia kusoma majibu yako!

Machi 4, 2022

Habarini Nyote! Tumekuwa na matukio mbalimbali kwa hii miezi michache iliyopita, na sasa tunayo furaha kuwashirikisha baadhi ya taarifa mpya. Pia, tunaomba radhi kwa kuchelewa kutuma kutuma hizi taarifa mpya. Utendaji kazi wetu ulipungua kuanzia Oktoba hadi Desemba, hiyo yote ni kutokana na msimu wa likizo na watu wapya kujiunga na timu yetu. Kisha, katika mwaka mpya, tulihitaji muda wa kuimarisha na kukamilisha mpango wetu wa mambo ya kiufundi. Hata hivyo, kazi yetu sasa inazidi kushika kasi na awamu ya ujenzi wa mradi imeanza rasmi. Pia, tunamshukuru kila mtu ambaye ametushirikisha maoni yake hadi sasa! Sasa, tunakualika usome masasisho yetu mapya (taarifa zetu mpya) na tushirikishe maoni yako kwenye ukurasa wa majadiliano ya mradi. Maoni yote ni muhimu kwetu, na tunatumai kuendelea kujifunza kutoka kwenu nyote. Asanteni!

Pendekezo la kuunda majina mapya ya Programu

Timu ya Kampeni inapendekeza kwamba tuunde majina mawili mapya majina mapya ya Programu katika MediaWiki, ambayo itaitwa "Event" na "Event Talk." Unaweza kuona pendekezo katika T302040 kwenye Phabricator. Madhumuni ya sehemu hizi mbili za majina ni kwamba patakuwa mahali palipotengwa katika wiki kwa matukio yote, kama vile kampeni, makongamano, mikutano, saa za kazi, au matukio mengine. Tunataka njia ya kubainisha kwa urahisi ukurasa wa 'tukio' ni nini, ili tuweze kufanya mambo yafuatayo:

  • Kuongeza usajili kwa kurasa za tukio (na kuepuka kuongeza usajili kwa kurasa zisizohusika na matukio, kama vile kurasa za makala)
  • Kuonesha matukio yote katika kalenda ya tukio katika siku zijazo
  • Kuanza kupata data sahihi zaidi kuhusu shughuli za tukio kama harakati (kama vile idadi ya matukio na aina gani za matukio yanayoendelea)
  • Kufanya iwe rahisi kwa kila mtu kujua ukurasa wa tukio ni nini, kwa kuwa sasa hivi kurasa za matukio mara nyingi zinafanana sana na kurasa za makala
  • Kuangazia ukweli kwamba kuandaa au kushiriki katika hafla ni aina muhimu ya shughuli ya harakati, na kwamba mtu anaweza kuwa Mwanawikimedia mwenye tija kwa njia zaidi ya kuchangia kwenye tovuti za wiki.

Masasisho ya uhandisi

Kati ya Oktoba na Januari, wahandisi watatu na meneja wa uhandisi walijiunga na timu yetu. Tangu wakati huo, tumeweza kufanya mipango ya kiufundi na kuzindua rasmi awamu ya ujenzi wa mradi. Wahandisi watajikita katika kujenga miundombinu ya msingi ya jukwaa la matukio ya kampeni na zana ya usajili. Wakishaunda kitu ambacho kinaweza kujaribiwa, tutawashirikisheni ninyi nyote. Kwa sasa, unaweza kufuatilia kazi yetu katika Bodi ya Mradi wa Usajili na wasifu wa mradi kwenye Phabricator.

Sasisho za muundo

Timu ya wabunifu imeunda toleo jipya la mifumo ya awali itakayofanya kazi katika kompyuta za mezani kulingana na maoni tuliyopokea katika majaribio ya utumiaji, ukurasa wa majadiliano ya mradi na njia zingine. Sasa, timu yetu ya ubunifu inafanya raundi ya pili ya majaribio ya utumiaji kwenye toleo jipya la mifumo ya awali itakayofanya kazi katika kompyuta za mezani. Mara tu tunapokamilisha mifumo hii ya awali itakayofanya kazi katika kompyuta za mezani, tutaishirikisha kwenu katika dondoo zijazo kuhusiana na hali ya mifumo hiyo. Zaidi ya hayo, timu ya wabunifu inatengeneza toleo la kwanza la mfumo huu wa usajili utakaofanya kazi kwenye simu, ambalo pia tunapanga kuwashirikisheni katika sasisho la hali ya mfumo huo hapo baadaye.

Taarifa za Balozi

Mabalozi watatu wa bidhaa wamejiunga na timu yetu: Antoni Mtavangu (Balozi wa Jumuiya ya Waswahili), Georges Fodouop (Balozi wa Jumuiya ya Kifaransa), and M. Bachounda (Balozi wa Jumuiya ya Kiarabu). Mabalozi wa bidhaa watakuwa wanafanya kazi kwa kushirikiana na timu kufanya uhamasishaji na kukusanya maoni kutoka kwa jumuiya za Wikimedia, na watachangia mawazo yao kuhusu maono na mkakati wa mradi huu. Pia watatusaidia kuelewa mahitaji ya waandaaji wa matukio kwa mtazamo wa mbali zaidi ya tulipo katika mradi wetu huu wa kwanza, ili tuendelee kupanga mipango zaidi kwa ajili ya kazi ya baadaye.

Fungua huria

  • Je, unafikiri itakuwa muhimu kwako (au Wanawikimedia wengine) kuunda majina mapya ya Programu kwaajili ya Mazungumzo ya Tukio na Tukio? Kwa nini ni muhimu au kwa nini sio muhimu?
  • Je, una maswali au wasiwasi gani kuhusu kuunda mifumo hii mipya itakayoshughulikia masuala ya matukio?
  • Je, kuna kitu kingine chochote ungependa kushiriki kuhusu dondoo za hali ya mradi au mradi kwa ujumla?

Tafadhali tushirikishe maoni yako kwenye ukurasa wa majadiliano ya mradi!

Oktoba 8, 2021

Habari, kwa kila mmoja! Tunayofuraha kubwa kuwashirikisha taarifa za hali ilivyo kuhusiana na mradi wa Mfumo wa Usajili unaoratibiwa na kitengo cha kitengo cha programu za kuendesha kampeni (Campaign Product team). Awali ya yote, tutawashirikisha misingi ya mradi wetu. Pili, tutawashirikisha toleo la awali mahususi kwa kompyuta za mezani (tolea la kwenye simu litashirikishwa hapo baadaye).Tatu, tutawapa maswali ninyi nyote. Asante kwa kila mmoja, na tunatazamia kusoma maoni yako katika ukurasa wa majadiliano wa mradi huu!

Misingi ya mradi

Kadri mradi ulivyoendelea, tumetambua misingi kadhaa ambayo ni ya muhimu kwa kazi yetu:

  • Kwa mpango wa muda mrefu, tunataka kutengeneza jukwaa, na sio tu nyenzo: Baadhi ya watu wameuliza kwanini hatutumii programu zilizopo za wazi kwaajili ya matumizi ya usajili. Tutachunguza njia zilizopo, na hadi sasa hakuna bado ambacho kimetolewa maamuzi ya mwisho. Lakini, pengine tungependa kuunda suluhu yetu wenyewe. Hii ni sababu ya kwanini kadri muda unavozidi kwenda tunataka kutengeneza Jukwaa la Usajili la Kampeni na sio tu suluhu ya usajili. Ili kutengeneza jukwaa hili, tutahitaji kutengeneza muundombinu muhimu, na mradi wa usajili ni hatua ya mwanzo kufanya hili litokee. Ili kujifunza zaidi, unaweza kutembelea sehemu ya mipango & maono
  • Tunataka kutengeneza kwaajili ya lugha mbalimbali, jumuiya za aina tofauti tofauti:Waratibu wa matukio wameelezea kwamba mfumo uliopo hautoi msaada wa kutosha kwa ulimwengu, na jumuiya zinazozungumza lugha mbalimbali. Tunakubaliana kabisa. Kwa sababu hii, hatuta chukulia mradi huu kuwa umemalizika mpaka tutakapotengeneza suluhu ambayo inatumika kwaajili ya miradi ya wiki kwa lugha zote na Miradi ya Wikimedia.
  • Tunapanga kutengeneza kwa njia ya majaribio: Toleo la kwanza la suluhu hii ya Mfumo wa usajili itakuwa ni ya msingi kabisa. Tunaiita MVP(au “Minimum Viable Product”), kwakuwa itakuwa na vitu vichache tu vya msingi ili ifanye kazi. Tunafanya kazi kwa namna hii ili tuanze kupokea maoni kuanzia mwanzo kabisa, na tunaweza kubaini matatizo kabla hatujawekeza nguvu kubwa kwenye kitu husika. Baada ya kutoa toleo la MVP, tutatengeneza matoleo ya juu zaidi ya mfumo wa usajili.
  • MVP itakuwa tu na vitu vinavyohitajika: Kwa MVP, lengo letu ni kutengeneza mfumo rahisi wa usajili, mpangilio na uratibu wa matukio. Matoleo ya awali tuliyoshirikisha hapa chini ni kwaajili ya toleo la MVP
  • Tutaongeza maboresho hapo baadaye: Baada ya kuunda toleo la MVP, tunaweza kuongeza uwezo wa waratibu wa matukio kuongeza maswali watakayotaka katika fomu ya kujisajilia, kama vile kuuliza kuhusu jinsia za washiriki, mahali walipo, uzoefu wa kuhariri tovuti za wiki, au kwanini wamejiunga na tukio husika. Tunaweza pia kuongeza uwezo wa waratibu kuandika maswali wanayopendelea wao wenyewe.

Matoleo: Toleo la tarakilishi/Kompyuta ya mezani

Katika matoleo hapo chini, tutaelezea jinsi toleo la MVP litakavyoonekana katika kompyuta za mezani.Matoleo haya ya awali (Wireframes) ni mojawapo ya hatua katika kutengeneza programu fulani, ambapo tunafikiria muonekano na jinsi nyenzo itakavyofanya kazi. Matoleo haya ya awali ni ya kinadharia; muonekano unaweza kubadilika pale wahandisi watakapoanza kutengeneza nyenzo yenyewe. Kumbuka kuwa tutawashirikisha matoleo ya kwenye simu kwenye taarifa zinazofuata hapo baadaye.

Kutengeneza usajili kwaajili ya tukio

Fikia kituo cha mratibu Tunataka kutengeneza “Kituo cha mratibu,” Kwa mradi huu, tunaweza kutengeneza kituo cha mratibu cha msingi kabisa (kisichokuwa na mambo mengi) ambacho kitapanuka taratibu kadri muda unavozidi kwenda. Nyenzo ya kwanza itakayowekwa katika Kituo cha Mratibu itakuwa ni Mfumo wa Kujisajili. Ili kukifikia Kituo cha Mratibu, watumiaji wanaweza kwenda kwenye Michango (Contributions)> Matukio ya Kampeni (Campaign Events).

Ikumbukwe kwamba, hapo baadaye, Kituo cha Mratibu kitakuwa pengine sehemu ya jukwaa kubwa la Matukio ya Kampeni. Ili kujifunza zaidi, unaweza kutembelea mipango & maono

Kufikia jukwaa la Matukio ya Kampeni

Kuchagua nyenzo ya kutengenezea usajili: Baada ya kwamba mratibu yupo kwenye Kituo cha Mratibu, wanaweza kuchagua kutengeneza mfumo wa usajili kwaajili ya tukio la kampeni. Ili kufanya hivi, watabonyeza “Tengeneza usajili kwaajili ya matukio ya kampeni yako.”

Kufikia nyenzo ya kutengenezea usajili

Kutengeneza usajili kwaajili ya tukio la kampeni: Baada ya kwamba mtumiaji amechagua kutengeneza fomu ya usajili, muonekano mpya utaonekana. Mratibu ataingiza taarifa zifuatazo: URL ya tukio, jina la tukio, tarehe, muda, saa za eneo husika, kama ni tukio la mtandaoni au la watu kufika kabisa, programu fuatiliaji ipi itatumika, URL ya kufuatilia mwenendo wa mradi kwa muda husika, majina ya watumiaji ya waratibu wa mradi,na kiungo kuelekea kwenye kundi la soga.Nyenzo fuatilizi na kundi la soga yatakuwa ni mambo ya ziada. Mtumiaji anabonyeza “Tengeneza Usajili” au “Create Registration” kwa kiingereza wakishamaliza kuongeza taarifa.

Baada ya zoezi la kutengeneza usajili kumalizika, muonekano wa usajili utaonekana moja kwa moja kwenye ukurasa wa tukiola kampeni. Tafadhali rejea kipengele kinachofuata ("Kuwasajili washiriki") kwa tarifa zaidi.

Ni muhimu kuzingatia kwamba, ili kutumia mfumo huu, waratibu watatakiwa kuandaa vitu kadhaa kabla ya kuutumia: Ukurasa wa kampeni, programu fuatiliaji (kwa mfano Dashibodi ya Programu na Matukio, na kundi la soga)

Kwa toleo la kwanza la mfumo wa usajili, tutakuwa tu tukiwauliza kuhusiana na majina ya watumiaji ya washiriki. Hii ni kwa sababu ni rahisi kutekeleza. Ingawa, baada ya kwamba toleo la kwanza limekwishatolewa, tutaangalia namna ya kuruhusu waratibu kuunda fomu za usajili za kisasa zaidi ambazo zitauliza washiriki maswali ya hiari kuhusu wao wenyewe na kwanini wanajiunga na kampeni husika.

Kutengeneza mfumo wa usajili kwaajili ya tukio la kampeni

Kuwasajili washiriki

Usajili kuongezwa kiotomatiki kwenye ukurasa wa tukio: Mara tu mratibu wa tukio atakapounda usajili wa tukio, hali ya usajili itaongezwa kiotomatiki kwenye URL ya ukurasa wa tukio iliyobainishwa na mratibu. Uzoefu wa usajili ni sehemu ya chini inayofunika ukurasa wa tukio. Tulichagua muundo wa kuwa na sehemu ya chini ili uweze kufanya kazi kwa aina nyingi tofauti za kurasa za tukio. Katika sehemu ya chini, kuna kitufe cha "Jisajili kama Jina la mtumiaji." Kwa hivyo, ikiwa jina la mtumiaji la mtu lilikuwa Lola, lingesema, "Jiandikishe kama Lola." Mtumiaji anaweza kubofya kitufe ili kujiandikisha.

Mfano wa ukurasa wa tukio wenye sehemu ya chini ya usajili ambayo imeongezwa kiotomatiki

Maelezo zaidi: Ikiwa mtumiaji atabofya “Maelezo Zaidi,” wanaweza kuona maelezo zaidi kuhusu tukio, kama vile tarehe, eneo, waandaaji na orodha ya washiriki. Kisha wanaweza kubofya "Jisajili kama Jina la mtumiaji" katika mwonekano huu pia. Baada ya mtumiaji kujiandikisha, wanapaswa kuona ujumbe wa uthibitisho.

Mtazamo wa habari zaidi wa uzoefu wa usajili; jopo la upande kwenye ukurasa wa tukio

Msaada wa kuingia na kuunda akaunti: Ikiwa mtumiaji hajaingia, ataona kiotomatiki dirisha ibukizi wanapobofya "Jisajili kama Jina la mtumiaji." Wanaweza kuchagua kuingia, ikiwa tayari wana akaunti, au wanaweza kujiandikisha, ikiwa hawana akaunti tayari. Mara tu watakapoingia au kuunda akaunti, watasajiliwa kiotomatiki katika tukio la kampeni husika.

Mfano wa dirisha ibukizi wakati mtumiaji anajaribu kujiandikisha kwa tukio la kampeni
Mfano wa dirisha ibukizi wakati wa kujisajili ikiwa mtumiaji atajaribu kujiandikisha kwenye kampeni bila ya akaunti ya wiki

Usajili uliofanikiwa: Baada ya mshiriki kusajiliwa kwa ufanisi, dirisha ibukizi litaonekana kuthibitisha usajili wao. Dirisha ibukizi litatoweka kiotomatiki baada ya muda mfupi. Ikiwa wana anwani ya barua pepe inayohusishwa na akaunti zao, tungependa pia barua pepe itumwe kiotomatiki, ambayo hutoa maelezo kuhusu tukio, kama vile kikundi cha gumzo ambacho wanaweza kujiunga nacho. Ikiwa washiriki wangependa kuondoka kwenye tukio, wanaweza kubofya "Hariri usajili" (kupitia sehemu ya chini au sehemu ya pembeni), ambayo itawauliza wathibitishe ikiwa wanataka kuondoka kwenye tukio.

Katika siku zijazo, washiriki wanaweza kuongeza maelezo ya hiari kuhusu wao wenyewe pale watakapojisajili (kama vile kiwango cha uhariri wa wiki, kwa nini wanajiunga na tukio la kampeni, n.k). Kama usaidizi huu ukiongezwa, washiriki pia wataweza kuhariri taarifa hii pia.

Angalia baada ya mshiriki kujiandikisha kwenye ukurasa wa tukio kwa kutumia sehemu ya chini
Tazama baada ya mshiriki kujiandikisha kwenye ukurasa wa tukio kupitia sehemu ya pembeni
Angalia itakavyokuwa kwa mshiriki anayetaka kujiondoa kwenye kampeni

Kusimamia usajili

Tazama fomu zote za usajili: Pindi mratibu wa tukio akishaunda fomu ya usajili, ataweza kuona fomu zote za usajili kwa matukio yao. Wanaweza kubofya mojawapo ya fomu ili kupata maelezo zaidi ya usajili, ikiwa ni pamoja na orodha ya washiriki. Wanaweza pia kufuta, kuhariri, au kufunga fomu za usajili kwa urahisi kupitia mwonekano huu.

Orodha ya fomu za usajili zinazoweza kutumika kwa mratibu

Kutazama, kufuta, na kutuma ujumbe kwa washiriki: Pindi tu fomu ya usajili itakapokuwa imeundwa, yeyote aliyebainishwa kama mratibu anaweza kutazama taarifa za mshiriki aliyejisajili, ikijumuisha: jina la mtumiaji la mshiriki, na tarehe na saa ya usajili. Wataweza kuchagua baadhi au washiriki wote kutoka kwenye orodha, na wataweza kuwatumia ujumbe au kuwafuta kutoka kwenye orodha.

Waandaaji wataweza kutuma ujumbe kwa washiriki, inaweza kuwa kwenye ukurasa wao wa mazungumzo au kwa barua pepe zao. Kulingana na ugumu wa kiufundi wa kazi, tunaweza kuchagua kutoa toleo la MVP ambalo hutuma tu ujumbe kwenye ukurasa wa majadiliano, au toleo la MVP linaweza kuruhusu chaguo zote mbili. Vyovyote vile, mpango wetu ni hatimaye kuruhusu njia zote mbili za ujumbe.

Mratibu anaweza kuangalia, kufuta au kutuma ujumbe kwa washiriki waliosajiliwa

Maswali huria

  1. Una maoni gani kuhusu mfumo wetu unaopendekezwa wa kuunda na kusimamia usajili wa matukio, kama mwandaaji wa kampeni? Je, mfumo huu unatoa faida gani ikilinganishwa na mfumo wako wa sasa? Je, mfumo huu una hasara gani ikilinganishwa na mfumo wako wa sasa?
  2. Una maoni gani kuhusu mfumo uliopendekezwa kuhusiana na kusajili washiriki kwenye ukurasa wa tukio? Je, mfumo huu unatoa faida gani ikilinganishwa na mfumo wako wa sasa? Je, mfumo hhuu una hasara gani ikilinganishwa na mfumo wako wa sasa?
  3. Kwanza tunapanga kuunda toleo la mwanzo (pia linajulikana kama "MVP," au toleo la chini kabisa la bidhaa inayotumika) la zana ya usajili.
  4. Je, ni vipengele gani muhimu ambavyo toleo hili la kwanza linapaswa kuwa navyo ili uweze kulitumia?"
  5. Unapoendesha kampeni, ni taarifa gani huwa unatuma kwa washiriki, na huwa unaituma wapi (k.m., ukurasa wa majadiliano, barua pepe, mitandao ya kijamii, n.k)?
  6. Kuhusu Mfumo wa Usajili; Je, unapendelea tutengeneze kipi kwanza, toleo la kompyuta ya mezani kwanza au toleo la simu la kwanza?
  7. Kuna kitu kingine chochote ungependa kuongeza?

Tafadhali tushirikishe maoni yako kwenye ukurasa wa majadiliano; Asante!