Privacy policy/Supplement/sw
Appearance
Sera ya Faragha ya Wakfu wa Wikimedia Chagua Maelezo ya Watoa Huduma
Sera Yetu ya Faragha inafafanua maelezo ya binafsi tunayokusanya na kutumia ili kuendesha Tovuti za Wikimedia. Wakati mwingine tunatumia watoa huduma wa kampuni nyinginezo ili kutusaidia kuboresha Tovuti za Wikimedia, na tunaweza kuwapa watoa huduma hawa idhini ya kufikia Maelezo yako ya Kibinafsi wakiyahitaji ili kutuhudumia au ili tuweze kutumia zana na huduma zao. Baadhi ya watoa huduma wetu hutuomba tuchapishe viungo za sera zao za faragha. Orodha ya watoa huduma hawa na viungo vya sera zao vinaweza kupatikana hapa chini.
Tafadhali kumbuka kuwa hii si orodha kamili ya watoa huduma wote ambao tunashiriki nao maelezo ya kibinafsi; huduma zingine pia huenda zitatumia data yako, kulingana na Sera yetu ya Faragha.
- Tunatumia Zendesk kutuma na kujibu maswali na maombi yanayotumwa kwa barua pepe. Maelezo ya Zendesk yanapatikana kwenye kiungo hiki. Zendesk ina masharti maalum ya ziada yanayotumika katika nchi fulani. Ili usome masharti hayo, tafadhali rejelea sehemu hii ya sera yao.