Mwongozo wa Kimataifa wa Mwenendo na Maadili/Kamati ya Uratibu/Chaguzi/2024/Tangazo- Wito kwa wagombea
Ripoti ya uidhinishaji wa Mkataba wa U4C na wito kwa Wagombea wa U4C sasa upo tayari
- Unaweza kupata ujumbe huu ukiwa umetafsiriwa katika lugha za ziada kwenye Meta-wiki. Please help translate to your language
Habarini nyote,
Ninawaandikieni leo nikiwa na vipande viwili muhimu vya habari. Kwanza, ripoti ya maoni kutoka kwenye Kamati ya Kuratibu uidhinishaji wa Mkataba wa Mwongozo wa Kimataifa wa Mwenendo na Maadili(U4C) sasa ipo tayari. Pili, wito kwa wagombea wa U4C umefunguliwa kuanzia sasa hadi hapo Aprili 1, 2024.
Kamati ya Kuratibu Mwongozo wa Kimataifa wa Mwenendo na Maadili (U4C) ni kundi lenye wanachama kutoka mataifa mbalimbali linalojitolea kutoa utekelezaji sawa na thabiti wa UCoC. Wanajamii wanaalikwa kutuma maombi yao kwa U4C. Kwa maelezo zaidi na majukumu ya U4C, tafadhali pitia Mkataba wa U4C.
Kwa mujibu wa katiba, kuna viti 16 kwenye U4C: viti vinane vya jumuiya kwa ujumla na viti vinane vya kanda ili kuhakikisha U4C inawakilisha utofauti katika hizi harakati.
Soma zaidi na utume maombi yako kwenye Meta-wiki.
Kwa niaba ya Timu ya Mradi wa UCoC,