Uchaguzi wa Wikimedia Foundation/2022/Tangazo/Pigia kura Matamko ya Dira ya Uchaguzi

From Meta, a Wikimedia project coordination wiki

Pigia kura matamko ya Dira ya Uchaguzi

Unaweza kupata ujumbe huu ukiwa umetafsiriwa katika lugha za ziada kwenye Meta-wiki.

Habarini nyote,

Watu waliojitolea katika uchaguzi wa 2022 wa Baraza la Wadhamini wamealikwa kupiga kura ili kupata matamko ya kutumia katika Dira ya Uchaguzi. Unaweza kupigia kura matamko ambayo ungependa yajumuishwe kwenye Dira ya Uchaguzi kwenye Meta-wiki.

Dira ya Uchaguzi ni zana ya kuwasaidia wapiga kura kuchagua wagombea ambao wanalingana vyema na imani na maoni yao. Wanajamii watapendekeza tamko kwa watahiniwa kujibu kwa kutumia mizani ya Lickert (kukubali/kutokukubali wala kukataa/kutokubali). Majibu ya wagombea kwa taarifa hizo yatawekwa kwenye zana ya Dira ya Uchaguzi. Wapiga kura watatumia zana hiyo kwa kuandika jibu lao kwenye kauli (kukubali/kukataa/kutokukubali wala kukataa). Matokeo yataonyesha wagombea ambao wanalingana vyema na imani na maoni ya mpiga kura.

Huu hapa ni ratiba ya Dira ya Uchaguzi:

  • Julai 8 - 20: Waliojitoleaji wanapendekeza matamko ya Dira ya Uchaguzi
  • Julai 21 - 22: Kamati ya Uchaguzi kupitia taarifa kwa uwazi na kuondoa taarifa zilizo nje ya mada
  • Julai 25 - Agosti 3: Wajitoleaji kupigia kura taarifa
  • Agosti 4: Kamati ya Uchaguzi itachagua matamko makuu 15
  • Agosti 5 - 12: watahiniwa wajipange kulingana na matamko
  • Agosti 16: Dira ya Uchaguzi itafunguliwa ili wapiga kura waitumie ili kusaidia kutoa uamuzi wao wa kupiga kura

Kamati ya Uchaguzi itachagua matamko makuu 15 mwanzoni mwa Agosti

Wenu,


Mkakati wa Harakati na Utawala

Ujumbe huu ulitumwa kwa niaba ya Kikosi Kazi cha Uteuzi wa Bodi na Kamati ya Uchaguzi