Mwongozo wa Kimataifa wa Mwenendo na Maadili/Kamati ya Uratibu/Uchaguzi/2024/Tangazo- Upigaji kura umefunguliwa
Ukumbusho kuhusu kupiga kura sasa ili kuchagua washiriki wa U4C ya awamu ya kwanza
- Unaweza kupata ujumbe huu ukiwa umetafsiriwa katika lugha za ziada kwenye Meta-wiki. Please help translate to your language
Ndugu Mwanawikimedia,
Unapokea ujumbe huu kwa sababu hapo kabla uliwahi kushiriki katika mchakato wa UCoC.
Huu ni ukumbusho kwamba kipindi cha kupiga kura kwa Kamati ya Kuratibu Mwongozo wa Kimataifa wa Mwenendo na Maadili (U4C) kitamalizika tarehe 9 Mei 2024. Soma maelezo kwenye ukurasa wa kupiga kura kwenye Meta- wiki ili kupata maelezo zaidi kuhusu upigaji kura na ustahiki wa mpiga kura.
Kamati ya Kuratibu Mwongozo wa Kimataifa wa Mwenendo na Maadili (U4C) ni kikundi cha kimataifa kilichojitolea kutoa utekelezaji sawa na thabiti wa UCoC. Wanajamii walialikwa kutuma maombi yao kwa U4C. Kwa maelezo zaidi na majukumu ya U4C, tafadhali pitia Mkataba wa U4C.
Tafadhali washirikishe ujumbe wanajumuiya wenzako ili nao waweze kushiriki.
Kwa niaba ya timu ya mradi wa UCoC,