Bodi ya Wadhamini ya Wakfu wa Wikimedia/Wito wa maoni: Uchaguzi wa Bodi ya Wadhamini/Wito wa Maoni kuhusu uchaguzi wa Baraza la Wadhamini sasa umefunguliwa

From Meta, a Wikimedia project coordination wiki

Wito wa Maoni kuhusu uchaguzi wa Baraza la Wadhamini umefunguliwa

Unaweza kupata Ujumbe huu ukiwa umetafsiriwa katika lugha tofauti kwenye Meta-wiki.

Wito wa Maoni: Uchaguzi wa Baraza la Wadhamini sasa umefunguliwa na utafungwa tarehe 7 Februari 2022.

Kwa wito huu wa maoni, Timu ya Mkakati wa Harakati na Utawala inachukua mtazamo tofauti. Mtazamo huu unajumuisha maoni ya jumuiya kutoka 2021. Badala ya kuongoza kwa mapendekezo, wito huu unaundwa kulingana na maswali muhimu kutoka kwa Bodi ya Wadhamini. Maswali muhimu yalitoka kwenye maoni kuhusu uchaguzi wa Baraza la Wadhamini wa 2021. Nia ni kuhamasisha mazungumzo ya pamoja na ukuzaji wa pendekezo shirikishi kuhusu maswali haya muhimu.

Kuna maswali mawili yaliyothibitishwa ambayo yataulizwa wakati wa Wito huu wa Maoni:

  1. Njia ipi ni bora ya kuhakikisha uwakilishi tofauti zaidi kati ya wagombea waliochaguliwa? Baraza la Wadhamini lilibaini umuhimu wa kuchagua wagombeaji ambao wanawakilisha anuwai kamili ya Wikimedia Movement. Michakato ya sasa imewapendelea watu wa kujitolea kutoka Marekani Kaskazini na Ulaya.
  2. Nini matarajio ya wagombea wakati wa uchaguzi? Wagombea wa bodi kwa kawaida wamekamilisha maombi na kujibu maswali ya jumuiya. Je, uchaguzi unawezaje kutoa maarifa yafaayo kwa wagombeaji huku pia ikithamini hadhi ya wagombeaji kama watu wa kujitolea?

Kuna swali moja la ziada ambalo linaweza kuwasilishwa wakati wa wito kuhusu michakato ya uteuzi. Swali hili bado linajadiliwa, lakini Bodi ilitaka kutoa ufahamu kuhusu maswali yaliyothibitishwa haraka iwezekanavyo. Tunatumahi ikiwa swali la ziada litaulizwa, litakuwa tayari katika wiki ya kwanza ya Wito wa Maoni.

Jiunge na mazungumzo.

Katika ubora,

Mkakati wa Harakati na Utawala