Wikimedia Foundation elections/2022/Community Voting/Election Compass/Answers/sw

From Meta, a Wikimedia project coordination wiki
This page is a translated version of the page Wikimedia Foundation elections/2022/Community Voting/Election Compass/Answers and the translation is 98% complete.
Statement by number Candidate Candidate's position Reasoning/Explanation
1: Shirika la Wikimedia Foundation linapaswa kufanya shughuli zake zote kwa uwazi kabisa (isipokuwa pale ambapo inaweza kusababisha masuala ya kisheria/faragha/usalama) Michał Buczyński Idhinisha Uwazi ni thamani muhimu katika harakati zetu, na kwa hakika WMF inapaswa kuwa wazi zaidi kuhusu mipango yake, bajeti, shughuli, malengo ya SMART na utimilifu wake, maamuzi makuu. Hata hivyo, uwazi huja kwa gharama. Kuandika ripoti, kusambaza maarifa, kuhakikisha uwazi na usalama wa kisheria huchukua muda wa wafanyakazi na wa watu wa kujitolea. Kutokana na uzoefu wangu najua usawa unahitajika, vinginevyo "uwazi kabisa" utamaanisha shirika linalojikita katika kujizungumzia badala ya kufanya mambo.
1: Shirika la Wikimedia Foundation linapaswa kufanya shughuli zake zote kwa uwazi kabisa (isipokuwa pale ambapo inaweza kusababisha masuala ya kisheria/faragha/usalama) Shani Evenstein Sigalov Idhinisha kabisa Ninaunga mkono kuwa muwazi inapowezekana. Muhimu kusisitiza kwamba kama ilivyo katika mabano, kuna masuala yanayohusiana na usalama, ulinzi, au sheria, ambapo uwazi hautakiwi.
1: Shirika la Wikimedia Foundation linapaswa kufanya shughuli zake zote kwa uwazi kabisa (isipokuwa pale ambapo inaweza kusababisha masuala ya kisheria/faragha/usalama) Tobechukwu Precious Friday Idhinisha Ninaamini Shirika la Wikimedia Foundation limekuwa wazi katika kuendesha shughuli hizi na ninaunga mkono kabisa hili ukiachana na pale ambapo ingesababisha masuala ya kiusalama.
1: Shirika la Wikimedia Foundation linapaswa kufanya shughuli zake zote kwa uwazi kabisa (isipokuwa pale ambapo inaweza kusababisha masuala ya kisheria/faragha/usalama) Kunal Mehta Idhinisha Kiasili WMF inapaswa kufanya kazi kwa mkao wa uwazi. Kama unavyoona, sio kila kitu kinaweza kuwa cha umma, lakini ni kwa kadri iwezekanavyo. Hili ni suala muhimu kwangu na jambo ambalo nililitetea mara kwa mara nikiwa mfanyakazi wa WMF (k.m. kurasa za wiki si Hati za Google, IRC si Slack). Ikiwa una muda, ningehimiza kutazama hotuba niliyotoa katika mkutano wa HOPE kuhusu jinsi Wikimedia inavyostawi kwa sababu ya uwazi.
1: Shirika la Wikimedia Foundation linapaswa kufanya shughuli zake zote kwa uwazi kabisa (isipokuwa pale ambapo inaweza kusababisha masuala ya kisheria/faragha/usalama) Farah Jack Mustaklem Idhinisha kabisa Kama mtetezi wa maarifa wazi, inaleta maana kwa Shirika la Wikimedia Foundation kukuza uwazi, na kuongoza kwa mfano na kuendesha shughuli zake kwa uwazi (isipokuwa pale ambapo inaweza kusababisha matatizo ya kisheria/faragha/usalama)
1: Shirika la Wikimedia Foundation linapaswa kufanya shughuli zake zote kwa uwazi kabisa (isipokuwa pale ambapo inaweza kusababisha masuala ya kisheria/faragha/usalama) Mike Peel Idhinisha kabisa Kimsingi harakati za Wikimedia hufanyika kwa uwazi, na hili ni jambo ambalo tunapaswa kutarajia kutoka kwa WMF. Uwazi huleta manufaa mengi katika suala la kushirikiana na jumuiya, na kuziangalia mbinu mara mbil mbili. Ni sawa na kutumia programu huria, ambayo humwezesha mtu yeyote kusaidia kukagua na kutengeneza msimbo.
2: Shirika la Wikimedia linapaswa kutoa usaidizi zaidi wa kiufundi ili kukidhi mahitaji ya jumuiya Michał Buczyński Idhinisha kabisa Asili ya swali ilikuwa Orodha ya Matamanio ya Jamii inayoendeshwa na timu ya Jumuiya ya Teknolojia. Huu ni mpango uliopokelewa vyema wa kutatua masuala madogo yanayopewa kipaumbele na jumuiya. Licha ya mafanikio yake, programu ilikabiliwa na idadi ya ucheleweshaji na mapungufu katika shida zilizochukuliwa kusuluhishwa kwa mwaka. Kama ilivyo mipango kama vile Orodha ya Matamanio kuwapa watu wanaojitolea zana bora zaidi zinazofanya kazi yao iwe rahisi na yenye ufanisi zaidi. na mahitaji yanabaki kuwa juu, kuongezeka kwa ufadhili ni muhimu.
2: Shirika la Wikimedia linapaswa kutoa usaidizi zaidi wa kiufundi ili kukidhi mahitaji ya jumuiya Shani Evenstein Sigalov Idhinisha Kwa kweli naunga mkono kwa kiasi kikubwa, ukiachan na kwamba naunga mkono, kwa vile ninatambua kwamba hatuwezi kufanya kila kitu ambacho tunaweza kutaka kufanya. Tazama video, ambapo ninafafanua zaidi juu ya hilo.
2: Shirika la Wikimedia linapaswa kutoa usaidizi zaidi wa kiufundi ili kukidhi mahitaji ya jumuiya Tobechukwu Precious Friday Idhinisha kabisa Ninaunga mkono hili lakini badala ya Shirika la Wikimedia Foundation kuunda au kutengeneza zana zenyewe kwa misingi ya nadharia, ningependekeza na kuhimiza kwamba jamii ishirikishwe katika uundaji wa zana kwani wanajua ni zana gani ambazo ni muhimu kwao. Zaidi ya hayo, nyenzo yoyote inayokusudiwa kutengenezwa pia inapaswa kuzingatia DEI.
2: Shirika la Wikimedia linapaswa kutoa usaidizi zaidi wa kiufundi ili kukidhi mahitaji ya jumuiya Kunal Mehta Idhinisha kabisa Hasa, "zaidi" inapaswa kuwa juu ya kutumia vipaumbele vinavyoongozwa na jumuiya ili kutoa rasilimali za kiufundi, si lazima kuongeza idadi ya watu. Kuwa na timu moja ya Wanajumuiya wa Teknolojia si endelevu. Kimsingi, timu ZOTE za teknolojia za WMF zinapaswa kufanya kazi zikilenga kuhudumia mahitaji ya jamii, sio moja tu.
2: Shirika la Wikimedia linapaswa kutoa usaidizi zaidi wa kiufundi ili kukidhi mahitaji ya jumuiya Farah Jack Mustaklem Idhinisha Shirika la Wikimedia Foundation hutoa miundombinu ambamo ndani yake miradi ya Wikimedia inafanyika, na hutoa usaidizi kwa bidhaa zilizopo na kubuni bidhaa mpya ili kusaidia jamii. Namna ambayo WMF inayapa kipaumbele masuala ya usaidizi wa kiufundi sio mara zote inawiana na matarajio ya jumuiya, na hii inahitaji kubadilika.
2: Shirika la Wikimedia linapaswa kutoa usaidizi zaidi wa kiufundi ili kukidhi mahitaji ya jumuiya Mike Peel Idhinisha kabisa Usaidizi wa kiufundi kwa jamii umekuwa mdogo kwa muda mrefu sana. Mchakato wa Orodha ya Matamanio ya Jumuiya husaidia, lakini unaweza kushughulikia idadi ndogo tu ya maombi yanayokuja, na wanahitaji uwezo mkubwa zaidi wa kushughulikia maombi zaidi.
3: Sifurahishwi na jinsi WMF inavyozidi kujipa mamlaka ya upande mmoja kufanya maamuzi kuhusu miradi ya Wikimedia ambayo baadaye huathiri jamii. Michał Buczyński Si upande wowote Swali ni la kibinafsi, na katika jumuiya zangu hakuna maendeleo yanayoonekana ya WMF kuchukua udhibiti tangu mwanzo, na kisha kuanzishwa rasmi kwa jukumu la uangalizi na sauti ya kutoaminiana kwa wasimamizi wa kawaida. UCoC imejadiliwa ipasavyo. Hata hivyo, ninasalia na wasiwasi kwani baadhi ya fikra zinaonyesha kutozingatia wafanyakazi wa kujitolea waliopo na uhuru wao, na ni nadra kuona thamani ya uongozi wetu uliosambaa.
3: Sifurahishwi na jinsi WMF inavyozidi kujipa mamlaka ya upande mmoja kufanya maamuzi kuhusu miradi ya Wikimedia ambayo baadaye huathiri jamii. Shani Evenstein Sigalov Si upande wowote Ingawa hii inaweza kuwa lilikuwa hivyo huko nyuma, siamini WMF bado linafanya kazi kwa njia hiyo tena. Shirika kwa sasa limejielekeza kwenye huduma kwa jamii. Suala kuu hapa ni ufafanuzi usio wazi wa majukumu na wajibu. Nina matumaini Mkataba wa Harakati, na Baraza la Kiulimwengu la siku zijazo, vitasaidia kuboresha hilo, pamoja na kazi ya sasa ya WMF kufanya wigo wake kuwa wazi zaidi.
3: Sifurahishwi na jinsi WMF inavyozidi kujipa mamlaka ya upande mmoja kufanya maamuzi kuhusu miradi ya Wikimedia ambayo baadaye huathiri jamii. Tobechukwu Precious Friday Idhinisha kabisa Siungi mkono WMF kujipa mamlaka ya upande mmoja katika kufanya maamuzi juu ya miradi inayoathiri jamii. Siku zote nimekuwa muumini wa demokrasia na harakati za Wikimedia nikiwa mfano wa vitendo wa mtu kupaswa kuhimiza usawa katika kufanya maamuzi. Hatuendeshi mfumo wa upande mmoja bali wa kidemokrasia na tunaweza kushirikiana pamoja ili kufanya maamuzi ya ushindi - maamuzi ya kushinda.
3: Sifurahishwi na jinsi WMF inavyozidi kujipa mamlaka ya upande mmoja kufanya maamuzi kuhusu miradi ya Wikimedia ambayo baadaye huathiri jamii. Kunal Mehta Idhinisha Nina matumaini kwamba Baraza la Kimataifa la uwakilishi linaweza kuchukua rasmi jukumu hili la kufanya maamuzi huku likiheshimu kujitawala kwa wiki.
3: Sifurahishwi na jinsi WMF inavyozidi kujipa mamlaka ya upande mmoja kufanya maamuzi kuhusu miradi ya Wikimedia ambayo baadaye huathiri jamii. Farah Jack Mustaklem Idhinisha Uamuzi wa WMF unapaswa kuwa wa uwazi na kuzingatia maoni kutoka kwa jamii ambazo zitaathiriwa na maamuzi yoyote.
3: Sifurahishwi na jinsi WMF inavyozidi kujipa mamlaka ya upande mmoja kufanya maamuzi kuhusu miradi ya Wikimedia ambayo baadaye huathiri jamii. Mike Peel Idhinisha Najua hii imetokea nyakati tofauti za bahati mbaya huko nyuma. Sina hakika kama hali hii inaongezeka, hata hivyo kwa ujumla sifurahishwi na maamuzi yoyote ya upande mmoja. Wikimedia hufanya kazi kwa makubaliano, si kwa mamlaka.
4: WMF iendelee kutafuta njia ya kupunguza, badala ya kupanua, wigo wa majukumu yake, na kuacha kadri iwezekanavyo uwezo wa kujipanga wa jumuiya. Michał Buczyński Idhinisha Mkataba wetu wa Harakati bado haujaandikwa, lakini mkakati wetu unachukua mgawanyo wa majukumu na ufadhili. Hii kwangu inamaanisha idadi kubwa ya vyombo imara, pamoja na kukabidhi vitendo na rasilimali na kuacha nafasi kwa uongozi wa jumuiya. Hii pia itaruhusu uimara zaidi na nafasi ya majaribio, ikiwezekana usawa zaidi na kudumisha ari yetu ya kujitolea.
4: WMF iendelee kutafuta njia ya kupunguza, badala ya kupanua, wigo wa majukumu yake, na kuacha kadri iwezekanavyo uwezo wa kujipanga wa jumuiya. Shani Evenstein Sigalov Si upande wowote Nakubaliana na sehemu ya kwanza (kupunguza upeo, kufafanua wajibu na majukumu), lakini sikubaliani na sehemu ya pili (jumuiya ya watu waliojitolea inaweza kudhibiti yanayobaki). Ninaamini miundo rasmi inahitajika, kama vile washirika waliopo/wa siku zijazo, ikijumuisha vituo/Baraza la Kimataifa, kufanya kazi ambayo WMF haifanyi. Sio kila kitu kingeweza kufanywa na watu waliojitolea ikiwa tunataka uwajibikaji na usawa.
4: WMF iendelee kutafuta njia ya kupunguza, badala ya kupanua, wigo wa majukumu yake, na kuacha kadri iwezekanavyo uwezo wa kujipanga wa jumuiya. Tobechukwu Precious Friday Si upande wowote Siegamii upande wowote kuhusu hili. Pamoja na kwamba siungi mkono WMF kuendelea kupanua majukumu yake badala yake ijikite kwenye yale ambayo tayari yanashughulikiwa, sishauri majukumu mengi kuachwa kwa Jumuiya pia; kwa sababu kama swali linavyosema, ni uwezo wa kujitolea na nisingependa Jumuiya zielemewe kupita kiasi.
4: WMF iendelee kutafuta njia ya kupunguza, badala ya kupanua, wigo wa majukumu yake, na kuacha kadri iwezekanavyo uwezo wa kujipanga wa jumuiya. Kunal Mehta Idhinisha Ninaunga mkono sheria hii na ninafurahi sana kuona jinsi ubao wa mgawanyo wa majukumu wa mkakati wa harakati unavyogawanyika.
4: WMF iendelee kutafuta njia ya kupunguza, badala ya kupanua, wigo wa majukumu yake, na kuacha kadri iwezekanavyo uwezo wa kujipanga wa jumuiya. Farah Jack Mustaklem Idhinisha kabisa Harakati za Wikimedia zilizogawanywa ni kielelezo tunachopambania kuwa nacho. Majukumu yoyote ambayo yanaweza kuchukuliwa na jamii yanapaswa kuwa mikononi mwa jamii, huku Shirikalikitimiza jukumu lake la kusaidia badala ya kuendesha.
4: WMF iendelee kutafuta njia ya kupunguza, badala ya kupanua, wigo wa majukumu yake, na kuacha kadri iwezekanavyo uwezo wa kujipanga wa jumuiya. Mike Peel Idhinisha WMF inahitaji kuhakikisha kuwa shughuli zake zipo kwenye mtazamo vile ipasavyo, na kuwezesha sehemu nyingine za harakati za Wikimedia kuchukua majukumu ambayo yanawafaa zaidi (k.m., washirika wanaofanya kazi katika nchi na mazingira tofauti). Kuendelea kutafuta kupunguza kazi husaidia kwa hilo - ingawa inahitaji kusawazishwa na kuwa wazi kwa fursa mpya, na kuepuka kupunguzwa au upanuzi wa upande mmoja.
5: Uchangishaji wa fedha wa WMF ni wa udanganyifu: unaleta sura potofu kwamba WMF ina uhaba wa pesa ilhali ni tajiri zaidi kuliko hapo awali. Michał Buczyński Idhinisha Swali hili linachanganya kauli ndogo na fikra. Kwanza, WMF inapaswa kuwa na mali nyingi zaidi kuliko hapo awali, lakini siamini kwamba uchangishaji wake ni mkubwa sana - badala yake ni kwamba uwekezaji uliofanywa kwa mfano. programu ziko chini sana. Kwa upande mwingine, uchangishaji wetu, ingawa unafaa, unasisitiza udumishaji mwingi wa seva, na unapaswa kujivunia na maeneo mengine ya shughuli zaidi: kutoka kwenye kazi ya kiufundi hadi k.m. kupambana na habari potofu.
5: Uchangishaji wa fedha wa WMF ni wa udanganyifu: unaleta sura potofu kwamba WMF ina uhaba wa pesa ilhali ni tajiri zaidi kuliko hapo awali. Shani Evenstein Sigalov Kataa WMF kwa hakika ni tajiri zaidi kuliko hapo awali, lakini bado inahitaji pesa, hasa ikizingatiwa maono yetu kabambe ifikapo 2030, na kufikiria kuhusu uendelevu wa miradi yetu kwa vizazi vijavyo. Sio rahisi na pesa inahitajika. Ninahisi kuwa kampeni ya mtandaoni inaweza kuboreshwa. Tazama video kwa zaidi.
5: Uchangishaji wa fedha wa WMF ni wa udanganyifu: unaleta sura potofu kwamba WMF ina uhaba wa pesa ilhali ni tajiri zaidi kuliko hapo awali. Tobechukwu Precious Friday Kataa Shirika la Wikimedia linafadhiliwa hasa kupitia michango, misaada ya kitaasisi na zawadi pamoja na mapato madogo yanayopatikana kupitia Wikimedia Enterprise. Ninahisi hakuna ubaya na mbinu hiyo kwani hakuna mtu anayelazimishwa kutoa michango. (Watu wanaona thamani katika kile tunachofanya na hivyo hawaoni chochote cha udanganyifu kuhusu uchangishaji wake. Kama shirika kubwa lenye idadi kubwa ya miradi, linahitaji fedha ili kuendelea kufanya kazi.
5: Uchangishaji wa fedha wa WMF ni wa udanganyifu: unaleta sura potofu kwamba WMF ina uhaba wa pesa ilhali ni tajiri zaidi kuliko hapo awali. Kunal Mehta Idhinisha Mbinu ya sasa ya uchangishaji fedha inatokana na WMF kukua kila mara. Bodi na wasimamizi wa juu waliweka malengo ya ukuaji wa nguvu na kisha timu ya uchangishaji inahitaji kuchukua hatua kali zaidi ili kuyafikia, ambayo mwishowe inachukuliwa kuwa ya udanganyifu. Ningependa kuona WMF ikiacha kukua na badala yake itulie kwenye ukubwa wake wa sasa.
5: Uchangishaji wa fedha wa WMF ni wa udanganyifu: unaleta sura potofu kwamba WMF ina uhaba wa pesa ilhali ni tajiri zaidi kuliko hapo awali. Farah Jack Mustaklem Kataa Ninapingana na tabia hii ya hali ya uchangishaji fedha ya WMF. Shirika llingeweza mara nyingi kutumia fedha zaidi kusaidia jamii katika kukuza maarifa bila malipo.
5: Uchangishaji wa fedha wa WMF ni wa udanganyifu: unaleta sura potofu kwamba WMF ina uhaba wa pesa ilhali ni tajiri zaidi kuliko hapo awali. Mike Peel Idhinisha kabisa Nakubaliana na taarifa hiyo, na hili linahitaji kurekebishwa. Hata hivyo, inahitajika kufanywa kwa njia ambayo haizuii mtiririko wa fedha programu huru na kazi zenye leseni huru ya utumiaji, kwa kuwa kuwa na fedha kwa ajili ya kazi hiyo ni muhimu sana. Kuhusisha washirika katika uchangishaji fedha kungesaidia sana katika hili, hasa katika kuboresha mahusiano ya wafadhili, na kuonyesha shughuli za ndani kwa jumuiya ya wafadhili.
6: Shughuli ya msingi ya Shirika laWikimedia Foundation inapaswa kuwa kufadhili juhudi za jumuiya ya Wikimedia Michał Buczyński Idhinisha Shughuli ya msingi ya WMF ni "kuwawezesha na kuwashirikisha watu duniani kote kukusanya na kuendeleza maudhui ya elimu chini ya leseni ya bure au katika leseni huru kwa matumizi ya umma, na kuyasambaza kwa ufanisi na kimataifa." Juhudi za ufadhili huwezesha na kushirikisha watu, na wakati jumuiya zikiaininsha mahitaji ipasavyo na kutoa kipaumbele kuweka juhudi ni njia nzuri ya kusonga mbele. Hata hivyo, katika maeneo mengine mapendekezo ya jumuiya yanaweza yasiwe sawa, na hii ni mojawapo ya kazi ya uongozi wa WMF kubainisha maeneo dhaifu.
6: Shughuli ya msingi ya Shirika laWikimedia Foundation inapaswa kuwa kufadhili juhudi za jumuiya ya Wikimedia Shani Evenstein Sigalov Si upande wowote Hiyo inategemea jinsi unavyofafanua "juhudi za Jumuiya". Kwangu hilo halieleweki sana. Je, hiyo inajumuisha kutunza majukwaa, seva, n.k? Kwa sababu sehemu kubwa ya bajeti ya kila mwaka inaelekea hilo, na juhudi nyingine mbalimbali za teknolojia/bidhaa.
6: Shughuli ya msingi ya Shirika laWikimedia Foundation inapaswa kuwa kufadhili juhudi za jumuiya ya Wikimedia Tobechukwu Precious Friday Kataa Sikubaliani na hili. Kwa maoni yangu, jukumu la msingi la WMF ni kuwawezesha na kuwashirikisha watu duniani kote kukusanya na kuendeleza maudhui ya elimu chini ya leseni ya bure au katika leseni huru kwa umma, na kuyasambaza kwa ufanisi na kimataifa. Hili linaweza kufanywa kwa njia kadhaa sio tu kupitia kuzifadhili wa Jumuiya.
6: Shughuli ya msingi ya Shirika laWikimedia Foundation inapaswa kuwa kufadhili juhudi za jumuiya ya Wikimedia Kunal Mehta Idhinisha Sina hakika kabisa kuhusu usemi huu, lakini kazi kuu ya WMF ni kuhudumia miradi.
6: Shughuli ya msingi ya Shirika laWikimedia Foundation inapaswa kuwa kufadhili juhudi za jumuiya ya Wikimedia Farah Jack Mustaklem Kataa Wakati shirika linapaswa kuendelea kufadhili juhudi za jumuiya, hiyo sio kazi ya msingi ya Shirika. Kufadhili teknolojia ambayo inadumisha miundombinu ambamo juhudi zote za jamii zimeegemezwa kwayo ndiyo kazi kuu.
6: Shughuli ya msingi ya Shirika laWikimedia Foundation inapaswa kuwa kufadhili juhudi za jumuiya ya Wikimedia Mike Peel Idhinisha Shughuli kuu ya harakati ni kazi ya jumuiya. Hata hivyo, kuna shughuli zinazohusiana (kama vile upande wa kiufundi wa mambo!) ambazo zinahitaji shughuli muhimu, huku zikiwa hazihusiani moja kwa moja na jumuiya.
7: Kwa ujumla WMF inapaswa kuchagua mawazo yaliyochunguzwa na jumuiya, badala ya mawazo ya ndani, kama msingi wa ramani yake ya shirika. Michał Buczyński Si upande wowote *Kama* itasimamiwa vyema, malengo ya WMF yanapaswa kuwiana vyema na malengo ya Harakati. Na kwa upande wa mawazo na uongozi naamini kuwa 1) jumuiya ni kundi letu la ajabu la viongozi na wataalam 2) WMF inapaswa kuajiri wataalam waliojitolea, na mawazo kutoka kwao yanatarajiwa sana. Mawazo yatekelezwe yanapokuwa yana mantiki bila kujali chanzo; hii ni hatua ya mgawanyo wa majukumu. Pengine, "kubadilika kwa misheni" au uzembe unaweza kudhuru WMF na jamii.
7: Kwa ujumla WMF inapaswa kuchagua mawazo yaliyochunguzwa na jumuiya, badala ya mawazo ya ndani, kama msingi wa ramani yake ya shirika. Shani Evenstein Sigalov Si upande wowote Sina uhakika kama naelewa kauli hii kikamilifu. WMF sasa inaambatana na Mkakati wa Harakati. Hiyo ilikuwa ni juhudi inayoendeshwa na jamii. Kila kitu amabcho tunachofanya sote msingi wake unapaswa kutoka kwa hilo na kufanya kazi kulitimiza hilo. Siamini katika hali yoyote ya kupita kiasi. Ushauri wa kitaalamu unapaswa kuzingatiwa. Pia, sio "sisi dhidi yao", bali kila mtu afanyea kazi kwa ushirikiano kuelekea malengo ya pamoja, na kuwa na mbinu za kubadilishana mawazo na kufikia hitimisho pamoja.
7: Kwa ujumla WMF inapaswa kuchagua mawazo yaliyochunguzwa na jumuiya, badala ya mawazo ya ndani, kama msingi wa ramani yake ya shirika. Tobechukwu Precious Friday Idhinisha kabisa Nakubaliana na hili kabisa. Inatakiwa kuwe na usawa katika kufanya maamuzi na sio kulazimisha maamuzi tu. Hii inajitokeza hasa katika eneo la zana na maendeleo ya teknolojia. Jamii inajua kinachowafaa zaidi kwa hivyo, mawazo yaliyohakikiwa na jumuiya yanapaswa kuhimizwa.
7: Kwa ujumla WMF inapaswa kuchagua mawazo yaliyochunguzwa na jumuiya, badala ya mawazo ya ndani, kama msingi wa ramani yake ya shirika. Kunal Mehta Idhinisha kabisa Kimsingi hii ndiyo dhana ya kuweka vipaumbele kutokea chini kwenda juu ambayo nitaitetea kwenye bodi. Tumeona mara kwa mara, hasa kuhusu masuala ya kiufundi, kwamba bodi na usimamizi wa juu wa WMF hawajaguswa na masuala na matatizo ambayo wahariri na wafanyakazi wa chini wanayakabili. Tunapaswa kuwa tunatafuta mawazo kutoka kwa kweye makundi hayo ya watu kwanza, badala ya kuyapata kutoka juu tu.
7: Kwa ujumla WMF inapaswa kuchagua mawazo yaliyochunguzwa na jumuiya, badala ya mawazo ya ndani, kama msingi wa ramani yake ya shirika. Farah Jack Mustaklem Idhinisha WMF inapaswa kuunga mkono mawazo yaliyotolewa maoni na jumuiya, badala ya kushinikiza mawazo yake yenyewe. Jamii zinajua vyema zaidi kile wanachohitaji, na ikionekana kuwa kinaweza kutekelezwa, zinapaswa kufuatwa na WMF.
7: Kwa ujumla WMF inapaswa kuchagua mawazo yaliyochunguzwa na jumuiya, badala ya mawazo ya ndani, kama msingi wa ramani yake ya shirika. Mike Peel Idhinisha Kama kanuni ya jumla, hii ni nzuri, na mawazo ya jumuiya yanapaswa kuungwa mkono sana. Hata hivyo, wafanyakazi wa WMF bado ni sehemu ya jumuiya, na mawazo ya ndani' ni muhimu - hasa kwa vile yanatoka katika mtazamo tofauti. Yanahitaji kuwa na usawa.
8: Kanuni ya Maadili ya Jumla ni nyongeza chanya kwa harakati za Wikimedia Michał Buczyński Idhinisha kabisa UCoC hujibu mahitaji ya wanajamii yaliyotolewa wakati wa mchakato wa kimkakati. Inainua viwango vya kawaida katika suala la usalama na ujumuisho - na hata kama maelezo bado yanajadiliwa, na bado tunahitaji kuangalia kwa makini utekelezaji katika mazoezi, viwango vya kimataifa vilikuwa hatua katika mwelekeo sahihi.
8: Kanuni ya Maadili ya Jumla ni nyongeza chanya kwa harakati za Wikimedia Shani Evenstein Sigalov Idhinisha kabisa UCoC ni hatua ya muhimu kuelekea utekelezaji wa mapendekezo mengine yoyote ya kimkakati, na ni sehemu ya juhudi kubwa kwa ajili ya Harakati bora zaidi, salama na jumuishi zaidi.
8: Kanuni ya Maadili ya Jumla ni nyongeza chanya kwa harakati za Wikimedia Tobechukwu Precious Friday Idhinisha kabisa Ninaunga mkono UCoC kwani inasaidia Wanawikimedia kufanya kazi katika kiwango cha msingi huku wakiheshimiana.
8: Kanuni ya Maadili ya Jumla ni nyongeza chanya kwa harakati za Wikimedia Kunal Mehta Idhinisha Sera za ustaarabu zipo kwenye miradi mingi, toleo la kimataifa linaonekana kuwa muhimu kadiri miradi inavyokuwa kwa ukaribu zaidi. Ibilisi yuko katika maelezo na tunapaswa kuwa tayari kuhariri na kurekebisha matatizo katika UCoC inapotolewa.
8: Kanuni ya Maadili ya Jumla ni nyongeza chanya kwa harakati za Wikimedia Farah Jack Mustaklem Idhinisha kabisa UCoC ni hati ambayo ina maadili ya kawaida ambayo yanapaswa kufuatwa na wote.
8: Kanuni ya Maadili ya Jumla ni nyongeza chanya kwa harakati za Wikimedia Mike Peel Idhinisha Ingawa si kamilifu, UCoC inasaidia sana harakati kwa kuhakikisha afya bora ya jamii. Faida zake huzidi hasara zake.
9: Viti vya jumuiya za baadaye vya Baraza la Wadhamini vinapaswa kujazwa tu kura ya mchangiaji (mhariri, msanidi wa kujitolea, na kadhalika) kwa kuwapigia kura wote walioteuliwa. Michał Buczyński Idhinisha Watu wote wa kimwili (wanachama wa jumuiya) na washirika wanastahili uwakilishi wao kwani kwa sasa WMF bado ina jukumu kubwa na huathiri maisha yao. Kwa ujumla viti hivi havihitaji kuunganishwa, na chaguzi tofauti zinaweza kuyapa makundi yote mawili uwakilishi bora (au angalau mtazamo wake bora).
9: Viti vya jumuiya za baadaye vya Baraza la Wadhamini vinapaswa kujazwa tu kura ya mchangiaji (mhariri, msanidi wa kujitolea, na kadhalika) kwa kuwapigia kura wote walioteuliwa. Shani Evenstein Sigalov Kataa kabisa Jambo hili sio wazi. Je, inarejelea viti vya sasa vya washirika wa jumuiya, au viti vyote, ikipendekeza kwamba kusiwe na viti vyovyote ambavyo Bodi yenyewe inateua? Ikiwa wa kwanza, thanaffiliates wanapaswa pia kuhusika. Ikiwa hilo la mwisho, basi napinga kabisa, kwani Bodi lazima iwe na uwezo fulani wa kuendana na mazingira kuhusu kuteua watu wenye weledi wa kitaalamu, ambao wanaweza wasichaguliwe na jumuiya, ili kufuata sheria.
9: Viti vya jumuiya za baadaye vya Baraza la Wadhamini vinapaswa kujazwa tu kura ya mchangiaji (mhariri, msanidi wa kujitolea, na kadhalika) kwa kuwapigia kura wote walioteuliwa. Tobechukwu Precious Friday Si upande wowote Sijali kuhusu hili. Mimi ni mtu anayehimiza utofauti. Maadamu wana shauku na ukereketwa wa misheni, sina shida hilo.
9: Viti vya jumuiya za baadaye vya Baraza la Wadhamini vinapaswa kujazwa tu kura ya mchangiaji (mhariri, msanidi wa kujitolea, na kadhalika) kwa kuwapigia kura wote walioteuliwa. Kunal Mehta Idhinisha Nimefurahi kuona kwamba Bodi iliamua kujielekeza kwenye kura nyingi za jumuiya kwa kile ambacho kwa kawaida kingekuwa viti vilivyochaguliwa na washirika. Katika uchaguzi huu, utumiaji wa washirika kama msingi haukufaa, kwani kamati ya uchanganuzi ilitumia muda mwingi kuliko thamani iliyotoa. Hatimaye, tunapaswa kulenga kuweka mchakato rasmi kuwa rahisi na wa moja kwa moja kadri iwezekanavyo.
9: Viti vya jumuiya za baadaye vya Baraza la Wadhamini vinapaswa kujazwa tu kura ya mchangiaji (mhariri, msanidi wa kujitolea, na kadhalika) kwa kuwapigia kura wote walioteuliwa. Farah Jack Mustaklem Si upande wowote "Kura za wachangiaji kwa wote walioteuliwa ni muhimu, lakini kura za washirika ni muhimu vile vile. Mfumo wa sasa wa mseto unajaribu kusawazisha kura za aina hizo mbili.

"

9: Viti vya jumuiya za baadaye vya Baraza la Wadhamini vinapaswa kujazwa tu kura ya mchangiaji (mhariri, msanidi wa kujitolea, na kadhalika) kwa kuwapigia kura wote walioteuliwa. Mike Peel Idhinisha Ni muhimu kwamba viti vya jumuiya vijazwe na michakato ya jumuiya, na wachangiaji ni sehemu kubwa na muhimu ya hilo. Hata hivyo, jumuiya inakwenda zaidi ya michango tu ya wahariri na wasanidi: wale wanaofanya kazi katika upande wa shirika wa Wikimedia (k.m., kuandaa matukio ya ana kwa ana) wanatoa michango muhimu kwa harakati za Wikimedia ambayo haipimwi kwa idadi ya hariri, nao pia wanapaswa kupewa nafasi ya kuweza kupiga kura katika uchaguzi wa bodi ya WMF.
10: Sifurahishwi na jinsi shirika la WMF linavyoendelea kuongeza idadi ya wafanyakazi na bajeti yake na kuchukua majukumu zaidi na zaidi ambayo hayahusiani moja kwa moja na miradi ya Wikimedia ya kujitolea na jamii zinazoifanyia kazi. Michał Buczyński Idhinisha Nina hofu na ukosefu wa umakini, sio tu katika WMF lakini kwa ujumla harakati za Wikimedia, na vishawishi vya kujaribu kutatua shida zote za ulimwengu, ambayo husababisha kuyumba kwa utendajikazi". Baadhi ya shughuli mpya au zilizoimarishwa zinawiana vyema na kile tunachofanya (k.m. ulinzi wa jumla wa uhuru wa kujieleza), baadhi yao chini ya hapo (Hazina ya Usawa wa Maarifa, athari za mazingira). Bodi ya Wadhamini BoT inahitaji kuyapa kipaumbele masuala muhimu zaidi ili Harakati ihifadhi maadili ya msingi na iendelee kuwa muhimu kiteknolojia na kijamii.
10: Sifurahishwi na jinsi shirika la WMF linavyoendelea kuongeza idadi ya wafanyakazi na bajeti yake na kuchukua majukumu zaidi na zaidi ambayo hayahusiani moja kwa moja na miradi ya Wikimedia ya kujitolea na jamii zinazoifanyia kazi. Shani Evenstein Sigalov Si upande wowote Nakubaliana na sehemu ya kwanza -- ninaamini kuwa chini ya usimamizi uliopita, WMF imekua kwa kasi sana. Baada ya kusema hayo, tuna usimamizi mpya, na lengo sasa ni kukomesha ukuaji huo na kuimarisha shirika. Kuhusu sehemu ya pili -- sikubaliani nayo. Kwa ufahamu wangu, WMF *haifanyi* chochote ambacho hakihusiani moja kwa moja na dhamira yetu kuu. Kinyume chake, hatuonekani kuwa na uwezo wa kufanya yote ambayo yanahitajika kufanywa / au kutakiwa na jamii
10: Sifurahishwi na jinsi shirika la WMF linavyoendelea kuongeza idadi ya wafanyakazi na bajeti yake na kuchukua majukumu zaidi na zaidi ambayo hayahusiani moja kwa moja na miradi ya Wikimedia ya kujitolea na jamii zinazoifanyia kazi. Tobechukwu Precious Friday Idhinisha Naunga mkono jambo hili. Ninahisi WMF inapaswa kuacha kuajiri na kujaribu kufanya kazi na wafanyakazi waliopo ili kutekeleza dhamira hiyo vyema na kwa ufanisi.
10: Sifurahishwi na jinsi shirika la WMF linavyoendelea kuongeza idadi ya wafanyakazi na bajeti yake na kuchukua majukumu zaidi na zaidi ambayo hayahusiani moja kwa moja na miradi ya Wikimedia ya kujitolea na jamii zinazoifanyia kazi. Kunal Mehta Idhinisha kabisa Sifurahishwi na hili kwani naamini hatujaona ongezeko la matokeo linloendana sambamba na ongezeko la idadi ya watu.
10: Sifurahishwi na jinsi shirika la WMF linavyoendelea kuongeza idadi ya wafanyakazi na bajeti yake na kuchukua majukumu zaidi na zaidi ambayo hayahusiani moja kwa moja na miradi ya Wikimedia ya kujitolea na jamii zinazoifanyia kazi. Farah Jack Mustaklem Kataa kabisa "Kwa kweli kiuhalisia nakubaliana kuhusu WMF kuchukua majukumu ambayo yanahusiana na dhamira kuu ya harakati, hata kama hayahusiani moja kwa moja na mradi wa Wikimedia.

"

10: Sifurahishwi na jinsi shirika la WMF linavyoendelea kuongeza idadi ya wafanyakazi na bajeti yake na kuchukua majukumu zaidi na zaidi ambayo hayahusiani moja kwa moja na miradi ya Wikimedia ya kujitolea na jamii zinazoifanyia kazi. Mike Peel Idhinisha kabisa Sifurahishwi na ongezeko kubwa la bajeti ya WMF kwa miaka mingi. Ninataka kuona hili likisahihishwa (na nimekuwa nikijaribu kulikazania ili liboreshwe kwa muda mrefu, kwa mfano, kupitia mapendekezo ya Kamati ya Usambazaji wa Fedha). Hata hivyo, kuna masuala muhimu ambayo WMF inahitaji kuyafanyia kazi ambayo hayaathiri moja kwa moja jamii. Viendelezi vya hakimiliki ni mfano unaofaa sana hapa: tunapaswa kuhakikisha kuwa kazi zinaingia kwenye matumizi ya umma kwa muda mwafaka.
11: Zaidi ya asilimia 50 ya gharama za Shirika la Wikimedia hutumiwa kwa mishahara nchini Marekani; hiyo asilimia ni kubwa mno Michał Buczyński Idhinisha Kwanza, jukumu na sura ya baadaye ya WMF, pamoja na muundo wa Harakati nzima za Wikimedia, inaweza kuwa tofauti sana baada ya Mkataba wa Harakati. Kwa kuzingatia hali ya sasa ya WMF, kuna nafasi kubwa ya ugawanyaji wa majukumu na kugeuza au kukasimisha shughuli mbalimbali zinazoendeshwa na taasisi nyingine za shirika. Ugawanyaji majukumu yakiunganishwa na utofauti, usawa na kutafuta ufanisi, inapaswa kumaanisha vyombo vikubwa zaidi, vilivyo nje ya California.
11: Zaidi ya asilimia 50 ya gharama za Shirika la Wikimedia hutumiwa kwa mishahara nchini Marekani; hiyo asilimia ni kubwa mno Shani Evenstein Sigalov Kataa Hili haliko wazi. Kubwa sana ukilinganisha na nini? Kwaajili ya nani? Ni njia ipi nzuri ya kuhukumu hilo? Ni nambari gani ya kuridhisha? Kwangu mie, sio juu ya suala la namba, lakini ni juhudi endelevu za kuwatendea haki wafanyakazi wote. Tuna wafanyakazi katika zaidi ya nchi 50. Ni ngumu sana, na tunapoajiriwa nchini Marekani, kwa hakika tuna kundi kubwa la wafanyakazi (na wafanyakazi wakuu) nchini Marekani. Hiyo inaathiri jinsi pai inavyogawanywa. Lakini je, hicho ndicho kipimo sahihi cha usawa na ujumuishi? Sina uhakika.
11: Zaidi ya asilimia 50 ya gharama za Shirika la Wikimedia hutumiwa kwa mishahara nchini Marekani; hiyo asilimia ni kubwa mno Tobechukwu Precious Friday Si upande wowote Siegemei upande wowote kuhusu hili na hivyo basi nahimiza WMF kuacha kuajiri.
11: Zaidi ya asilimia 50 ya gharama za Shirika la Wikimedia hutumiwa kwa mishahara nchini Marekani; hiyo asilimia ni kubwa mno Kunal Mehta Si upande wowote Sina maelezo ya kutosha kuthibitisha hili. Ningependa kuona WMF ikijihusisha na uwazi wa mishahara. Kuwa na wafanyikazi zaidi wanaotokea maeneo mbalimbali kila wakati ni jambo zuri, lakini kuna wapangaji wengi zaidi wa utofauti kuliko tu suala la mahali ambapo mtu anaishi leo.
11: Zaidi ya asilimia 50 ya gharama za Shirika la Wikimedia hutumiwa kwa mishahara nchini Marekani; hiyo asilimia ni kubwa mno Farah Jack Mustaklem Idhinisha "Shirika la Wikimedia Foundation linapaswa kujitahidi kuleta ujumuishi katika masula yake ya kuajiri. Ingawa Wikimedia Foundation ina msingi wake Marekani, miradi yake kwa asili ni ya kimataifa.

"

11: Zaidi ya asilimia 50 ya gharama za Shirika la Wikimedia hutumiwa kwa mishahara nchini Marekani; hiyo asilimia ni kubwa mno Mike Peel Kataa WMF ni shirika la Marekani. Ni kawaida kutarajia kwamba inatumia pesa zake nyingi kwa mishahara nchini Marekani. Hii ndiyo sababu tuna washirika wanaofanya kazi kote ulimwenguni: badala yake tunapaswa kutumia pesa nyingi za harakati kupitia washirika, badala ya WMF.
12: Kamati ya Uchaguzi lazima iwajibike kikamilifu na kuchaguliwa au kuteuliwa na jumuiya Michał Buczyński Idhinisha Utawala bora unahitaji kiwango fulani cha uwajibikaji wa moja kwa moja kutoka kwa Kamati ya Uchaguzi, na mchakato unaohusisha watu wa kujitolea ni njia ya kuvutia kwa viongozi wapya wa jumuiya. Hata hivyo, kwa sheria ndogo za sasa kuchagua wanachama wapya wa BoT ni utaratibu wa WMF, na mahitaji yao ni muhimu. Pia tunataka kuzuia ushawishi mwingi ambao unaweza k.m. kupotosha matokeo na watu wachache waliojitolea.
12: Kamati ya Uchaguzi lazima iwajibike kikamilifu na kuchaguliwa au kuteuliwa na jumuiya Shani Evenstein Sigalov Si upande wowote Ni afadhali nisizungumzie kamati ya uchaguzi wakati wa uchaguzi wenyewe. Ninaona ni ya ajabu na ufanyaji kazi mbaya. Tayari niko kwenye kumbukumbu nikikubali kwamba baadhi ya vipengele vya mchakato wa uchaguzi vinaweza kuboreshwa, ambavyo ni pamoja na kamati ya uchaguzi, lakini sio wao pekee. Lakini kwa vyovyote vile, wagombea kutoa maoni yao zaidi wakati wa uchaguzi ambapo wao ni sehemu ya huo uchaguzihali hiyo inaonekana katika ladha mbaya na sio mchakato sahihi wa kubadilisha mambo.
12: Kamati ya Uchaguzi lazima iwajibike kikamilifu na kuchaguliwa au kuteuliwa na jumuiya Tobechukwu Precious Friday Idhinisha Nakubaliana na hili. Kamati inapaswa kuwajibika kwa usawa kwa jamii kwa uwiano bora na harambee.
12: Kamati ya Uchaguzi lazima iwajibike kikamilifu na kuchaguliwa au kuteuliwa na jumuiya Kunal Mehta Idhinisha kabisa Wanaoendesha chaguzi za jumuiya wanapaswa kuwajibika kwa jamii. Bodi za Uchaguzi wa 2021 na 2022 zimeonesha kuwa malengo ya kamati ya kudumu ya uchaguzi hayajatimizwa. Tunapaswa kutathmini upya katiba na muundo wa kamati kwa ujumla wake mara tu baada ya uchaguzi huu kukamilika.
12: Kamati ya Uchaguzi lazima iwajibike kikamilifu na kuchaguliwa au kuteuliwa na jumuiya Farah Jack Mustaklem Idhinisha Jumuiya inapaswa kusimamia utendaji kazi wa Kamati ya Uchaguzi na kuiwajibisha.
12: Kamati ya Uchaguzi lazima iwajibike kikamilifu na kuchaguliwa au kuteuliwa na jumuiya Mike Peel Idhinisha kabisa Ninasikitishwa na jinsi Kamati ya Uchaguzi inavyoteuliwa, kwa kuwa haionekani kuhusisha jamii katika mchakato huo. Pia nina wasiwasi kuhusu jinsi inavyoitikia maswali wakati wa uchaguzi, na nadhani inahitaji kufanya kazi nyingi zaidi za kupanga kabla ya uchaguzi kuanza, ili kuhakikisha kuwa mchakato huo unawekwa wazi kabla ya uchaguzi kuanza.
13: Rahisisha Mchakato wa Uchaguzi wa Bodi ya Wadhamini ili kuwafanya Wanajumuiya kuwa na hamu na kushirikishwa Michał Buczyński Idhinisha Kama ilivyobainishwa hapo juu, chaguzi za kujitegemea za jumuiya za wanaojitolea na washirika zinapaswa kutoa uwakilishi bora (au angalau mtazamo wake bora) na uelewa zaidi, matokeo yake itakuwa kwa kutoa ushiriki zaidi.
13: Rahisisha Mchakato wa Uchaguzi wa Bodi ya Wadhamini ili kuwafanya Wanajumuiya kuwa na hamu na kushirikishwa Shani Evenstein Sigalov Idhinisha kabisa (n/a)
13: Rahisisha Mchakato wa Uchaguzi wa Bodi ya Wadhamini ili kuwafanya Wanajumuiya kuwa na hamu na kushirikishwa Tobechukwu Precious Friday Idhinisha kabisa Siwezi kukubaliana kidogo. Watu hawapewi moyo wa kugombea kwa sababu ya mchakato mgumu.
13: Rahisisha Mchakato wa Uchaguzi wa Bodi ya Wadhamini ili kuwafanya Wanajumuiya kuwa na hamu na kushirikishwa Kunal Mehta Idhinisha kabisa Uchaguzi hufanyika vizuri pale ambapo wapiga kura wanaelewa kikamilifu na kujihusisha na mchakato. Mchakato huu wa uchaguzi umefanya kinyume chake kabisa.
13: Rahisisha Mchakato wa Uchaguzi wa Bodi ya Wadhamini ili kuwafanya Wanajumuiya kuwa na hamu na kushirikishwa Farah Jack Mustaklem Idhinisha Uhusiano wa mtumiaji na muda wa umakini ni mdogo. Katika mzunguko wa sasa wa uchaguzi, Kamati ya Uchaguzi imejaribu kurahisisha sana mchakato huo. Bado kuna hatua ambazo zinaweza kuchukuliwa ili kurahisisha zaidi.
13: Rahisisha Mchakato wa Uchaguzi wa Bodi ya Wadhamini ili kuwafanya Wanajumuiya kuwa na hamu na kushirikishwa Mike Peel Idhinisha kabisa Hii ni mara ya pili kwangu kuwa kwenye mchakato huu, na mara zote mbili imekuwa ngumu sana - lakini kwa njia tofauti. Mchakato wa moja kwa moja, wenye sheria na taratibu zilizoshirikishwa kwa uwazi mapema (na kujadiliwa na jumuiya), ungesaidia sana hapa.
14: Utengenezaji wa programu unapaswa kulenga maendeleo ya mara kwa mara na vipengele vya msingi badala ya miradi mifupi na vipengele vipya. Michał Buczyński Si upande wowote Nadhani maneno ya swali hili hayajakaa sawa. Kuna mifano mingi mizuri ya vitu vidogo k.m. kuboresha ubora wa maisha na tija ya wanaojitolea. Kwa kuzingatia mantiki ya swali, labda lingepasa kuuliza "Uendelezaji wa programu unapaswa kupangwa kimkakati na kwa muda mrefu, kujenga vyote misingi na vipengele."
14: Utengenezaji wa programu unapaswa kulenga maendeleo ya mara kwa mara na vipengele vya msingi badala ya miradi mifupi na vipengele vipya. Shani Evenstein Sigalov Si upande wowote Kauli hii haieleweki sana kwangu ili kutoa maoni yangu. Ninakubaliana na baadhi tu ya sehemu zake, na sikubaliani na wengine. Itabidi nielewe vizuri zaidi kilichomaanishwa hapa ili nitoe maoni vizuri.
14: Utengenezaji wa programu unapaswa kulenga maendeleo ya mara kwa mara na vipengele vya msingi badala ya miradi mifupi na vipengele vipya. Tobechukwu Precious Friday Idhinisha kabisa Nakubali kabisa. Ndiyo maana Programu kwenye app store husasishwa mara kwa mara. Tunapaswa kuzingatia zana ambazo ni endelevu na zinazoweza kusasishwa badala ya zana za muda mfupi ambazo zinapitwa na wakati
14: Utengenezaji wa programu unapaswa kulenga maendeleo ya mara kwa mara na vipengele vya msingi badala ya miradi mifupi na vipengele vipya. Kunal Mehta Kataa Tunahitaji zote mbili. Tunahitaji timu thabiti ya jukwaa ili kudumisha vipengele muhimu, lakini pia timu zinazoweza kubuni vipengele vipya ambavyo hatuna. Hivi majuzi tumefanya uundaji wa vipengele vipya sana na hatujadumisha vya kutosha. Ninataka pia kusisitiza kwamba maendeleo ya kiufundi lazima yawe ni ya ushirikiano kati ya wafanyakazi wa kujitolea na wafanyakazi wa shirika.
14: Utengenezaji wa programu unapaswa kulenga maendeleo ya mara kwa mara na vipengele vya msingi badala ya miradi mifupi na vipengele vipya. Farah Jack Mustaklem Si upande wowote Ukuzaji wa vipengele vya msingi ni muhimu kama vile kutekeleza vipengele vipya. Nisingetoa pesa moja ili kuzingatia nyingine.
14: Utengenezaji wa programu unapaswa kulenga maendeleo ya mara kwa mara na vipengele vya msingi badala ya miradi mifupi na vipengele vipya. Mike Peel Idhinisha Tunayo maombi mengi ya kiufundi na urekebishaji wa hitilafu kutoka kwenye jumuiya, ambayo yanahitaji kutatuliwa. Pia tuna vipengele vingi vya msingi ambavyo vinahitaji kuviendeleza na uboreshaji muhimu. Hata hivyo, tunahitaji pia vipengele vipya vinavyotengenezwa (kama vile muonekano wa ndani wa programu ya mtumiaji unaoweza kupanuka vizuri ambao unafanya kazi vizuri kwenye vifaa vikubwa na vidogo!). Kuna haja ya kuwa na uwiano bora hapa, ambao unahitaji kufanywa kwa kushauriana na jamii.
15: WMF inapaswa kuanzisha mchakato shirikishi wa bajeti, ambapo jumuiya ya wahariri inashiriki katika ugawaji wa fedha. Michał Buczyński Idhinisha Usaidizi wa kiuangalifu kwasababu maneno yenye utata yanaweza kuleta dhana mbalimbali. Kwanza, michakato kama hii ipo, ikijumuisha kamati za ruzuku na Utafiti wa Orodha ya Matamanio. Pili, kiwango cha ushiriki kinatakiwa kiwe cha kuridhisha kwa pande zote - k.m. mjadala wa bajeti nzima na jumuiya nzima unaweza kushindwa kufikiwa na kila mtu kabisa- hata hivyo tathmini ya kina kutoka kwa wawakilishi (k.m. FDC) au bajeti kubwa ya orodha ya matamanio na fursa kwa jumuiya pana inastihili kusifiwa.
15: WMF inapaswa kuanzisha mchakato shirikishi wa bajeti, ambapo jumuiya ya wahariri inashiriki katika ugawaji wa fedha. Shani Evenstein Sigalov Si upande wowote WMF inapaswa kuruhusu maoni kuhusu Mchakato wa Mipango wa Mwaka, ambao tayari umetekelezwa. Sidhani kama tunaweza kuendesha bajeti kwa njia shirikishi kwa asilimia zote. Sipati picha jinsi mchakato kama huo utakabyofanya kazi, kivitendo, kwa njia endelevu na kwa wakati unaofaa. Pia, jukumu la Bodi ni kusimamia bajeti na uendeshaji. Jumuiya huchagua kile kilichokubalika na wadhamini wengi. Uwe na imani na wateule wako kuacha wafanya kazi yao. Hatimaye, ikiwa kuna pendekezo la vitendo la mchakato kama huo, lipeleke kwa Kamati ya Masuala ya Jamii ili lifikiriwe.
15: WMF inapaswa kuanzisha mchakato shirikishi wa bajeti, ambapo jumuiya ya wahariri inashiriki katika ugawaji wa fedha. Tobechukwu Precious Friday Si upande wowote Sijali kuhusu hili
15: WMF inapaswa kuanzisha mchakato shirikishi wa bajeti, ambapo jumuiya ya wahariri inashiriki katika ugawaji wa fedha. Kunal Mehta Idhinisha Ningependa kuona maelezo zaidi juu ya jinsi jambo hili linavyofanya kazi kwa vitendo, lakini ninaunga mkono michakato ambayo inaanzia chini kwenda juu.
15: WMF inapaswa kuanzisha mchakato shirikishi wa bajeti, ambapo jumuiya ya wahariri inashiriki katika ugawaji wa fedha. Farah Jack Mustaklem Idhinisha Kati ya kanuni ya uwazi na ujumuishwaji shirikishi, jamii inapaswa kuwa na sauti katika ugawaji wa fedha.
15: WMF inapaswa kuanzisha mchakato shirikishi wa bajeti, ambapo jumuiya ya wahariri inashiriki katika ugawaji wa fedha. Mike Peel Idhinisha Nimeshiriki katika kamati shirikishi za ruzuku za Wikimedia kwa muongo mmoja uliopita, na zinafanya kazi vizuri sana katika kuleta maoni na uzoefu tofauti ili kusaidia kuboresha mipango ya kila mwaka. Michakato shirikishi ya bajeti itakuwa hatua kubwa huko mbeleni - ingawa nadhani hatua ya kwanza ni kuelekea kwenye mapitio shirikishi ya mpango wa mwaka wa WMF.