Jump to content

Movement Charter/Drafting Committee/Announcement 2021 07 27/sw

From Meta, a Wikimedia project coordination wiki
This page is a translated version of the page Movement Charter/Drafting Committee/Announcement 2021 07 27 and the translation is 100% complete.

Wito kwa Wagombea kuwa Mwanakamati wa Kamati ya kuunda Movement Charter

Kamati inayoshughulika na Mpango mkakati wa Harakati za Wikimedia Fiundation inawatangazia wito rasmi kwa wagombea wanaotaka kuwa wanakamati wa kamati ya kuunda Movement Charter. Wito huo unafunguliwa rasmi Agosti 2, 2021 na utafungwa mnamo September 14, 2021.

Kamati inatarajiwa kuwa na uwakilishi wa watuwa aina tofautitofauti katika harakati za Shirika la Wikimedia Foundation.Utofauti huo wa watu ni katika minajiri ya jinsia, lugha, jiografia na uzoefu. Hii inahusisha ushiriki katika miradi, washirika wa WMF, na katika Shirika lenyewe la Wikimedia Fiundation.

Uzoefu wa kuongea kiingereza hauhitajiki kuwa mojawapo ya kigezo ili kuwa mwanakamati.Pale itakapohitajika, msaada wa tafsiri na ufafanuzi utatolewa. Wanakamati watapokea posho kwaajili ya gharama zitakazotokana na ushiriki wao.Posho hizo ni dola za kimarekani 100 (US$100) kila baada ya miezi miwili.

Tunatafuta watu walio na baadhi ya sifa zifuatazo:

  • Ajue namna ya kuandika kwa ushirikiano/kwa kushirikiana.(atakayeonesha uzoefu wake kwa vitendo itakuwa ni faida kwake zaidi kuhusu kupata nafasi hii)
  • Awe na uwezo kutafuta maelewano
  • Ajikite kwenye masuala ya ujumuishwaji na utofauti wa watu
  • Awe na ujuzi kuhusiana na uendeshaji wa mijadala na mashauriano na wanajamii
  • Awe na uzoefu wa kimawasiliano na watu wa tamaduni mbalimbali
  • Awe na uzoefu wa kiutawala au uzoefu wa kiuongozi katika mashirika yasiyo ya faida
  • Awe na uzoefu wa kujadiliana na pande tofauti na kufikia mwafaka

Kamati inategemewa kuanza na watu 15.Kama watu watakuwa 20 au zaidi, njia mchanganyiko ya uchaguzi na uteuzi itatumika.Kama kutakuwa na wanakamati 19 au pungufu ya hapo, basi njia ya kuchagua itatumika bila kuitisha uchaguzi.

Je, utalisaidia shirika la Wikimedia lisonge mbele kwenye kwa kuwa mmojawapo wa wanakamati? Basi tuma maombi yako kuomba uwanakamati hapa