Chaguzi za Wikimedia Foundation/2022/Tangazo/Kutangaza wagombea sita wa uchaguzi wa Bodi ya Wadhamini wa 2022/Kifupi

From Meta, a Wikimedia project coordination wiki

Kutangaza wagombeaji sita kwa uchaguzi wa Bodi ya Wadhamini wa 2022

Unaweza kupata ujumbe huu ukiwa umetafsiriwa katika lugha za ziada kwenye Meta-wiki.


Habarini nyote,

Wawakilishi Washirika wamemaliza muda wao wa kupiga kura. Wagombea waliochaguliwa wa Bodi ya Wadhamini wa 2022 ni:

Unaweza kuona maelezo zaidi kuhusu Matokeo na Takwimu ya uchaguzi huu wa Bodi.

Mashirika ya Washirika yalichagua wawakilishi wa kupiga kura kwa niaba ya Shirika Mshirika. Wawakilishi wa Washirika walipendekeza maswali ya kujibu kwa watahiniwa katikati ya Juni. Majibu haya kutoka kwa watahiniwa na maelezo yaliyotolewa na Kamati ya Uchambuzi yalitoa msaada kwa wawakilishi walipokuwa wakifanya uamuzi wao.

Tafadhali chukua muda kuwashukuru Wawakilishi wa Washirika na Wanachama wa Kamati ya Uchambuzi kwa kushiriki katika mchakato huu na kusaidia kukuza Bodi ya Wadhamini kwa uwezo na utofauti. Saa hizi za kazi ya kujitolea hutuunganisha katika uelewa na mtazamo. Asante kwa ushiriki wako.

Asante kwa wanajamii waliojitokeza kama wagombea wa Baraza la Wadhamini. Kufikiria kujiunga na Baraza la Wadhamini si uamuzi mdogo. Muda na majitoleo ambayo wagombea wameonyesha hadi sasa imeonesha juu ya kujitolea kwao kwenye harakati hizi. Hongera kwa wagombea waliochaguliwa. Shukrani kubwa na moyo wa shukrani kwa wale wagombea ambao hawakuchaguliwa. Tafadhali endelea kushirikisha uongozi wako kwa Wikimedia.

Wapiga kura wanaweza kufanya nini sasa?

Kagua matokeo ya mchakato wa uteuzi wa Washirika.

Soma zaidi hapa kuhusu hatua zinazofuata katika uchaguzi wa Baraza la Wadhamini wa 2022.

Wenu,

Mkakati wa Harakati na Utawala

Ujumbe huu ulitumwa kwa niaba ya Kikosi Kazi cha Uteuzi wa Bodi na Kamati ya Uchaguzi