Jump to content

Uchaguzi wa Wikimedia Foundation/2022/Tangazo/Kutangaza wagombea sita wa uchaguzi wa Baraza la Wadhamini wa 2022

From Meta, a Wikimedia project coordination wiki
Outdated translations are marked like this.

Kutangaza wagombea sita kwa uchaguzi wa Bodi ya Wadhamini wa 2022

Unaweza kupata ujumbe huu ukiwa umetafsiriwa katika lugha za ziada kwenye Meta-wiki.


Habarini nyote,

Mchakato wa upigaji kura wa Washirika umekamilika. Wawakilishi kutoka kila Shirika Mshirika walijifunza kuhusu watahiniwa kwa kusoma taarifa za watahiniwa, kupitia majibu ya watahiniwa kwa maswali, na kuzingatia ukadiriaji wa watahiniwa uliotolewa na Kamati ya Uchambuzi. Wagombea waliochaguliwa wa Bodi ya Wadhamini wa 2022 ni:

Unaweza kuona taarifa zaidi kuhusu Matokeo na Takwimu ya uchaguzi huu wa Bodi.

Tafadhali chukua muda kuwashukuru Wawakilishi wa Washirika na Wanachama wa Kamati ya Uchambuzi kwa kushiriki katika mchakato huu na kusaidia kukuza Bodi ya Wadhamini kwa uwezo na utofauti. Saa hizi za kazi ya kujitolea hutuunganisha katika uelewa na mtazamo. Asante kwa ushiriki wako.

Asante kwa wanajamii waliojiweka mstari wa mbele kama wagombea wa Baraza la Wadhamini. Kufikiria kujiunga na Baraza la Wadhamini si uamuzi mdogo. Muda na majitoleo ambayo watahiniwa wameonyesha hadi sasa inaonesha juu ya kujitolea kwao kwenye harakati hizi. Hongera kwa wagombea waliochaguliwa. Shukrani kubwa na moyo wa shukrani uwaendee wagombea ambao hawakuchaguliwa. Tafadhali endelea kushirikisha uongozi wako kwa Wikimedia.

Asante kwa wale waliofuatilia mchakato wa Washirika wa uchaguzi huu wa Bodi. Unaweza kukagua matokeo ya mchakato wa uteuzi wa Washirika.

Sehemu inayofuata ya mchakato wa uchaguzi wa Bodi ni kipindi cha upigaji kura cha jumuiya. Unaweza kutazama rekodi ya matukio ya uchaguzi wa Bodi hapa. Ili kujiandaa kwa kipindi cha upigaji kura wa jumuiya, kuna mambo kadhaa wanajamii wanaweza kujihusisha nayo kwa njia zifuatazo:

Wenu,

Mkakati wa Harakati na Utawala

Ujumbe huu ulitumwa kwa niaba ya Kikosi Kazi cha Uteuzi wa Bodi na Kamati ya Uchaguzi