Jump to content

Universal Code of Conduct/Enforcement guidelines/Voter information/sw

From Meta, a Wikimedia project coordination wiki
This page is a translated version of the page Universal Code of Conduct/Enforcement guidelines/Voter information and the translation is 92% complete.
Outdated translations are marked like this.
Universal Code of Conduct

Upigaji kura wa kuidhinisha rasmi Miongozo ya Utekelezaji Sheria Jumla za Kinidhamu (Universal Code of Conduct, UCoC) umepangwa kufanyika tarehe 7 Machi 2022 hadi 21 Machi 2022 kupitia SecurePoll. Wapigaji kura wote wanaostahiki miongoni mwa Jamii ya Wikimedia watakuwa na fursa ya kuungama au kupinga matumizi ya Miongozo ya Utekelezaji, na kutoa sababu. Uidhinishaji rasmi wa miongozo ya utekelezaji ni muhimu ili kuweka mbinu na michakato ya utekelezaji wa UCoC. Hapa chini kuna maelezo zaidi kuhusu maagizo ya kupiga kura na ustahiki wa mpigaji kura.

The vote is closed and the results have been published. The proposal is approved.

Pia tazama Maswali ya Kawaida kuhusu Upigaji Kura ili kupata maelezo kuhusu kupiga kura.

Mwito kwa wajitoleaji wa kufikia Wapigaji Kura

Ungependa kuimarisha idadi ya wapigaji kura katika jamii yako? Hauhitajiki kuwa na uzoefu katika uchaguzi au upigaji kura. Wajitoleaji wanaweza kusaidia kufahamisha jamii zao kuhusu upigaji kura ya uidhinishaji rasmi. Wajitoleaji wote kutoka kwenye Miradi yote ya Wikimedia wanakaribishwa! Saidia kuhakikisha kwamba sauti na maslahi ya jamii yako zinajumuishwa katika upigaji kura wa uidhinishaji rasmi (7 - 21 Machi 2022) kwa kuhusisha jamii yako! Unaweza kufanya hivi kwa kusajili kwenye Meta-wiki ili kupokea mapasho, kwa kutumia ukurasa wa mazungumzo ili kuona maswali kuhusu tafsiri, au unaweza kuwasiliana nasi kwenye ucocproject@wikimedia.org

Mchakato wa kupiga kura

Ikiwa unastahiki kupiga kura:

  1. Pitia Miongozo ya Utekelezaji ili kuona sera ya Sheria Jumla za Kinidhamu.
  2. Amua kuungama au kupinga matumizi ya Miongozo ya Utekelezaji. Ikiwa unapinga miongozo hii, andika mapendekezo yako ya mabadiliko kwenye Miongozo ili kujumuisha pamoja na kura yako.
  3. Jifunze jinsi ya kupiga kura yako ukitumia SecurePoll.
  4. Nenda kwenye ukurasa wa Upigaji Kura wa SecurePoll na ufuate maagizo.
  5. Kumbusha wanajamii wengine kupiga kura!

Ni nini kinachopigiwa kura?

Bodi ya Wadhamini ya Wikimedia Foundation wanaungama kura ya jamii kuhusu pendekezo la miongozo ya utekelezaji ya UCoC kufuatia uidhinishaji rasmi wa UCoC na Bodi yenyewe. Wadhamini pia wanatambua kuungama kura hiyo kwa barua ya pamoja ya Kamati za Usuluhishaji na utafiti wa maafisa wajitoleaji, wanachama washirika, na kamati ya kutengeneza rasimu.

Mojawapo ya mapendekezo makuu ya malengo ya kimkakati ya mwaka 2030 ilikuwa utengenezaji wa UCoC ili iwe msingi wa kote ulimwenguni wa tabia zinazoruhusiwa kwa mradi bila kuruhusu unyanyasaji.

Miongozo ya Utekelezaji Sheria Jumla za Kinidhamu

Miongozo hii ni ya utekelezaji Sheria Jumla za Kinidhamu. Hapo awali UCoC iliidhinishwa rasmi na Bodi ya Wadhamini, ingawa bado haijaidhinishwa na jamii. Inajumuisha hatua za uzuiliaji, ugunduaji, na uchunguzaji na hatua nyingine zinazochukuliwa ili kukabiliana na ukiukaji wa Sheria Jumla za Kinidhamu. Kimsingi, utekelezaji unashugulikiwa na, lakini sio tu, maafisa wateule kote kwenye miradi, matukio, na maeneo husika kwenye majukwaa ya wahusika wengine wa Wikimedia ya mtandaoni au nje ya mtandao. Itafanywa kwa mpangilio mzuri wa kimuda na kwa usawa katika mradi mzima wa Wikimedia.

Miongozo ya Utekelezaji UCoC ina sehemu mbili:

  • Kazi za uzuiliaji
    • Kukuza ufahamu wa UCoC, kupendekeza mafunzo wa UCoC, miongoni mwa mengine.
  • Kazi za ukabilianaji
    • Kuweka mchakato wa kurekodi, Kusindika ukiukaji ulioripotiwa, Kutoa rasilimali kwa ukiukaji ulioripotiwa, Kuteua hatua za utekelezaji kwa ajili ya ukiukaji, etc.

Kwa nini unapaswa kupiga kura?

Uidhinishaji rasmi wa miongozo ya utekelezaji ni muhimu ili kufanikisha mbinu na michakato na hata za utekelezaji wa UCoC. Upigaji kura kuhusu Miongozo ya Utekelezaji umebuniwa ili kutathmini jinsi jamii inaungama UCoC na ili kukusanya maoni kama wapigaji kura wana wasiwasi kuhusu mapendekezo ya sasa. Ni muhimu kuhakikisha sauti yako inasikika kupitia kura yako na ikiwa unachagua "la", ni muhimu kubainisha ni sehemu gani ya miongozo ambayo unawasiwasi kuihusu, na kwa nini.

Muhimu zaidi, kupiga kura:

  • Kutahakikisha kwamba maoni yako kuhusu mradi wa Wikimedia yanawasilishwa katika kura za ulimwengu mzima.

Jinsi ya kupiga kura

A mockup of the SecurePoll ballot. Note especially that votewiki may suggest you are not logged in. Your vote will still count.

Tafadhali soma sehemu hii kabla ya kwenda kwenye SecurePoll ili kupata maelezo muhimu ili kurahisisha mchakato wako wa kupiga kura.

* Karatasi ya kura itawasilisha swali linalopigiwa kura, na kukupa machaguo mawili: “Ndiyo” na “La”
  • Sanduku la “Maoni” ni sehemu ua kuweka maoni kuhusu wasiwasi zozote ulizo nazo kuhusu miongozo iliyopendekezwa.
  • Kisha SecurePoll itakuarifu kwamba kura yako imerekodiwa.
  • Unaweza kupiga kura tena katika uchaguzi. Inafuta na kurekodi upya kura yako. Unaweza kufanya hivyo mara nyingi kadri utakavyo.

Matokeo ya kura yatabainishwa vipi?

Angalau kura zaidi ya 50% za watumiaji walioshiriki zitahitajika ili kuendelea kwenye uidhinishaji rasmi wa Bodi ya Wadhamini. Kwa sasa, mradi huu hauna mbinu moja ya kufuata ya kubaini mchakato wa kupiga kura uliofaulu/kutofaulu (baadhi ya mbinu hutumia mbinu ya kura nyingi kwa njia kubwa (⅔), huku mbinu nyingine zikitumia wingi wa kura tu (50% +1), ilhali mbinu nyingine zinaepuka kuhesabu idadi ya kura). Kwa mchakato huu, ili kuendanisha na kura nyingi za maoni katika mamlaka nyingi ulimwenguni, mbinu ya wingi wa kura tu itatumika.

Wapigaji kura wataulizwa ni vipengele gani vinahitaji kubadilishwa na kwa nini. Ikiwa kura zitaonyeshana kuwa "la" ndiyo mshindi, timu ya mradi wa UCoC wataondoa utambulisho wa waliotoa maoni na kuchapisha maoni ya waliopigia "la" kura, na kutayarisha ripoti iliyofupishwa. Wanachama wawili wa Kamati za Kutengeneza Rasimu za UCoC wataalikwa ili kutengeneza Kamati ya Uhakiki; kundi hili litapitia maboresho kwenye Miongozo kulingana na wasiwasi zilizoibuliwa katika mchakato wa kupiga kura. Sawa na mchakato huu, marekebisho yatachapishwa ili kuhakikiwa. na kupigiwa kura kwa mara ya pili.

Watu nje ya Wikimedia Foundation watahusika katika kufuatilia upigaji kura ili kuhakiki uhalali?

Matokeo ya kura yatafuatiliwa kuona kama kuna hatia zilizofanywa na Wafanyakazi wa Wikimedia walio na uzoefu katika michakato ya upigaji kura na uthibitishaji. Wafuatiliaji upigaji kura ni:

  • Sj - Mdhamini wa zamani, mhudumu wa zamani
  • User:Tks4Fish - Mhudumu wa sasa, Msimamizi wa Wikipedia ya Kireno, Mhakiki na Msimamizi
  • Matanya – current steward, admin on hewiki and Commons, member of the Small Wiki Monitoring Team
  • TheresNoTime – current steward, administrator, checkuser and oversighter on enwiki, admin on Meta

Ustahiki wa kupiga kura

Ustahiki wa kupiga kura unabainishwa na Bodi ya Wadhamini ya Wikimedia Foundation. Wachangiaji tote waliosajiliwa wa Wikimedia wanaotimiza mahitaji ya chini zaidi ya shughuli, wafanyakazi na wanakandarasi washirika na wa Wikimedia Foundation (walioajiriwa kabla ya tarehe 17 Januari 2022), na wadhamini wa sasa na wa zamani wa Wikimedia Foundation, watakuwa na fursa ya kupigia kura pendekezo la miongozo utekelezaji katika SecurePoll.

Wahariri

Unaweza kupiga kura kutoka kwa akaunti yoyote moja iliyosajiliwa unayomiliki kwenye tovuti ya Wikimedia. Unaweza tu kupiga kura mara moja, bila kujali ni akaunti ngapi unazomiliki. Ili kuhitimu, akaunti hii lazima:

  • isizuiliwe kutoka kwa zaidi ya mradi mmoja;
  • na isiwe roboti;
  • na iwe imefanya angalau maharirio 300 kabla ya tarehe 7 Februari 2022 katika tovuti zote za Wikimedia;
  • na iwe imefanya angalau maharirio 20 kati ya tarehe 7 Agosti 2021 na 7 Februari 2022.

Zana ya Ustahiki wa Akaunti inaweza kutumiwa ili kuthibitisha kwa haraka ustahiki msingi wa kupiga kura wa mhariri.

Watengenezaji

Watengenezaji wanahitimu kupiga kura ikiwa:

  • ni wasimamizi wa seva ya Wikimedia wenye ufikiaji wa Shell
  • au amefanya angalau mchango mmoja kwenye akiba zozote za Wikimedia repos kwenye Gerrit, kati ya tarehe 7 Agosti 2021 na 7 Februari 2022

Vigezo vya ziada:

  • au amefanya angalau mchango mmoja kwenye akiba yoyote katika nonwmf-extensions au nonwmf-skins, kati ya tarehe 7 Agosti 2021 na 7 Februari 2022
  • au amefanya angalau mchango mmoja kwenye akiba yoyote ya zana ya Wikimedia (kwa mfano magnustools) kati ya tarehe 7 Agosti 2021 na 7 Februari 2022
  • au amefanya angalau maharirio 300 kabla ya tarehe 7 Februari 2022 na amefanya angalau maharirio 20 kati ya tarehe 7 Agosti 2021 na 7 Februari 2022 kwenye translatewiki.net.
  • au wadumishaji/wachangiaji wa zana, roboti, programu za watumiaji, vifaa, na moduli zozote za Lua kwenye tovuti za Wikimedia.
  • au wamehusika pakubwa katika michakato ya kubuni na/au kuhakiki utengenezaji wa kiufundi unahusiana na Wikimedia.

Kumbuka: Ikiwa unatimiza vigezo vikuu, utaweza kupiga kura mara moja. Kwa ajili ya vikwazo vya kiufundi vya SecurePoll, watu wanaotimiza vigezo vya ziada huenda wasiweze kupiga kura moja kwa moja, isipokuwa iwe wanatimiza yoyote ya vigezo vingine. Ikiwa unafikiri kwamba unatimiza vigezo vya ziada, tafadhali tuma barua pepe kwa anwani ucocproject@wikimedia.org ukitoa sababu angalau siku nne kabla ya siku ya mwisho ya kupiga kura.

Wafanyikazi na wakandarasi wa Wikimedia Foundation

Wafanyikazi na wakandarasi wa sasa wa Wikimedia Foundation wanahitimu kupiga kura ikiwa wameajiriwa na Wikimedia Foundation kuanzia tarehe 17 Januari 2022.

Wafanyikazi na wakandarasi wa washirika wa mradi wa Wikimedia

Sura ya sasa, shirika la kimuktadha, au wafanyikazi na wakandarasi wa kundi la watumiaji wa sasa wa Wikimedia Foundation wanahitimu kupiga kura ikiwa wameajiriwa na shirika lao kuanzia tarehe 17 Januari 2022.

Memba wa bodi ya Wikimedia Foundation

Memba wa sasa na wa awali wa Bodi ya Washamini wanastahiki kupiga kura.

Maswali ya Kawaida kuhusu Upigaji Kura

  1. Ninaweza kuthibitisha ustahiki wangu vipi?
    Wahariri wanaweza kutumia zana ya Ustahiki wa Akaunti ili kuthibitisha ustahiki katika uchaguzi wa sasa. Ukurasa wa maelezo ya akaunti unapatikana ili kujifunza mengi zaidi kuhusu idadi ya maharirio yako na historia yako ya michango.
  2. Mahitaji ya ustahiki yanabainishwa vipi?
    Bodi ya Wikimedia Foundation wanabainisha mahitaji ya ustahiki kabla ya uchaguzi kuanza. Haya ndiyo mahitaji sawa yanayotumiwa kwa chaguzi za Bodi ya Wadhamini.
  3. Mpigaji kura anayestahiki hawezi kupiga kura
    Unaweza kupokea ujumbe: "Samahani, haupo kwenye orodha iliyotayarishwa hapo awali ya watumiaji walioidhinishwa kupiga kura katika uchaguzi huu."
    Suluhu

    Hakikisha umeingia ndani ya akaunti.

    Hakikisha unapiga kura ukiwa kwenye Meta-wiki, unaweza kutumia kiungo hili elekezi ili kuenda kwenye ukurasa wa mwanzo wa kupiga kura.

    Ikiwa wewe ni mtengenezaji, mfanyakazi au memba wa Bodi ya Ushauri wa Wikimedia Foundation, Kamati ya Uchaguzi huenda wameshindwa kukulinganisha na jina mahsusi la mtumiaji. Unapaswa kuwasiliana na ucocproject@wikimedia.org ili kuongezwa kwenye orodha hii.

    Ikiwa bado unashindwa kupiga kura na unaamini unapaswa kuweza kupiga kura tafadhali acha ujumbe kwenye ukurasa wa mazungumzo wa uchaguzi au uwasiliane na Kamati ya Uchaguzi kwa anwani ucocproject@wikimedia.org .Jibu linapaswa kutumwa ndani ya saa 72.

  4. Ninashindwa kuingia ndani kwenye VoteWiki
    Hauhitajiki kuingia ndani kwenye VoteWiki ili kupiga kura. Ukiona karatasi ya kura, basi nikumaanisha SecurePoll imekutambua kwa mafanikio. Kwa sababu za kiusalama, ni akaunti chache zilizosajiliwa kwenye VoteWiki.
  5. Mtu yeyote anaweza chaguo langu nililopigia kura?
    Hapana, uchaguzi ni salama. Uchaguzi huu unatumia programu ya SecurePoll. Kura ni za siri. Hakuna mtu kutoka Kamati ya Uchaguzi, Bodi, wala mtu yeyote kwenye wafanyikazi wa Wikimedia Foundation anaweza kuona kura. Mwanatimu wa Imani na Usalama katika Wikimedia Foundation ana ufunguo wa usimbaji wa uchaguzi. Baada ya ufunguo hio kuamilishwa, uchaguzi unasimamishwa.
  6. Ni data zipi zinachukuliwa kuhusu wapigaji kura?

    Baadhi ya data inayoweza kutambuliwa kibinafsi kuhusu wapigaji kura inaweza kuonekana na watu wachache wateule wanaokagua na kuhesabu kura (Wafuatiliaji uidhinishaji rasmi watatangazwa punde).

Hii inajumuisha anwani ya IP na ajenti wa mtumiaji. Data hizi zinafutwa otomatiki siku 90 baada ya uchaguzi.

Hii inajumuisha anwani ya IP na ajenti wa mtumiaji. Data hizi zinafutwa otomatiki siku 90 baada ya uchaguzi.

  1. Data hizi zitatumika vipi?
    Takwimu kuhusu uchaguzi huu zitafupishwa kwenye matokeo ya kurasa za uchaguzi kuhusu ripoti kuu na za baada ya uchambuzi za uchaguzi. Hakuna maelezo yanayoweza kutambuliwa kibinafsi zitakazochapishwa. Maelezo haya yanayoweza kutambuliwa kibinafsi yanaweza kutumika kubaini idadi ya wapigaji kura binafsi na jinsi kura zilivyotapakaa kote ulimwenguni.
  2. Ninapopiga kura, sioni arifa yoyote kwamba kura imepokewa, na ujumbe otomatiki unatokea na kusema kwamba ninahitajika kuwa nimeingia ndani ili kupiga kura. Ni nini kinaendelea?

    Hauhitajiki kuingia ndani kwenye VoteWiki ili kupiga kura. Hitilafu hii sana sana ni suala la kashe. Tuwie radhi kwa ajili ya tatiso hili: tafadhali jaribu kupiga kura tena kwenye m:Special:SecurePoll/vote/391.
    Hii inapaswa kukuletea ujumbe unaosema "Upigaji kura huu utafanywa kwenye tovuti kuu. Tafadhali bofya kitufe kilicho hapo chini ili kuhamishwa." Kubofya kitufe hiki kutakupeleka kwenye seva ya kupiga kura na kukuwezesha kupiga kura.

    Pia kumbuka kwamba uko huru kuchagua au kubadilisha chaguo lako unalopigia kura mara nyingi kadri utakavyo. Ni kura moja pekee itakayohifadhiwa kwa kila mtumiaji, na kwa urahisi mfumo utabadilisha kura yako ya zamani na kura yako mpya, na kufuta kura zozote za hapo awali.

    Wakati mchakato wako wa kupiga kura umekamilika, ujumbe wa mapokezi unaonyeshwa kwenye skrini, ambao unaweza kuhifadhi kama ushahidi kwamba umepiga kura.

  3. Mfumo wa kupiga kura umelindwa vipi dhidi ya watumiaji wanaowasilisha kura maradufu?
    Ni kura moja pekee itahifadhiwa kwenye mfumo kwa kila mtumiaji. Uko huru kuchagua au kubadilisha chaguo lako unalopigia kura mara nyingi kadri utakavyo. Kwa urahisi mfumo utabadilisha kura yako ya zamani na kura yako mpya, na kufuta kura zozote za hapo awali.
  4. Wafanyakazi wanalazimishwa au kuhamasishwa kupigia kura chaguo fulani?
    Hapana, wafanyakazi wa Wikimedia Foundation na wale wa washirika hawahamasishwi kupigia kura chaguo fulani. Tunahamasisha kila mtu binafsi kupiga kura kwa njia huru. Ili miongozo ya utekelezaji Sheria za Kinidhamu iwe fanisi, tunahitaji michango ya kweli ili kutusaidia kugundua kama kuna maeneo yanayohitaji kuboreshwa.
  5. Timu ya Imani na Usalama ni ya haki kuhusiana ana matokeo ya kura?
    Kitengo cha Imani na Usalama kina sehemu tatu: Sera, Maelezo Potoshi, na Operesheni. Timu inayowezesha UCoC ni timu ya Sera. Timu ya Sera haihusiki katika uchunguzi wa tabia za watumiaji. Ingawa haiaminiki kwamba timu ya Operesheni inaweza kuwa isiyo ya haki, utengenishaji huu wa majukumu uliwekwa haswa ili kuepuka hali zisizo za haki kutokea. Timu ya Sera haikadiriwi na kana kwamba hati hii iliyotengenezwa kwa ushirikiano inapitishwa kwa mara ya kwanza au marekebisho zaidi yanahitajika. Timu hii inakadiriwa na kana kwamba inashirikiana vyema na jamii. Hii inamaanisha kutengeneza mkabala wa ushirikiano wa kutekeleza UCoC ambayo inahudumia jamii. Lengo letu ni kutimiza jukumu hilo vyema kadri iwezekanavyo.
  6. Maswali mengine ambayo hayajatajwa hapa
    Kwa hitilafu za kiufundi au mfuto wa kupiga kura, tafadhali tuma barua pepe kwa anwani ucocproject@wikimedia.org. Tafadhali bainisha jina la mtumiaji ambalo unajaribu kutumia ili kupiga kura na mradi ambao unajaribu kupigia kura. Mwanatimu wa mradi atajibu barua pepe yako punde iwezekanavyo.