Jump to content

Mpango wa Mwaka wa Wikimedia Foundation/2023-2024/Ushirikiano

From Meta, a Wikimedia project coordination wiki
This page is a translated version of the page Wikimedia Foundation Annual Plan/2023-2024/Collaboration and the translation is 100% complete.

Kiambatisho cha Maoni

Kuanzia Aprili 18-Mei 19, 2023, Shirika la Wikimedia lilishirikisha na kujadili rasimu ya mpango wake wa kila mwaka na Wanawikimedia kote ulimwenguni na kote kwenye Wiki. Muhtasari wa rasimu ya mpango wa kila mwaka ilichapishwa katika zaidi ya chaneli za jumuiya 30+, ndani na nje ya wiki, katika lugha kadhaa.Shirika pia lilijiunga na mijadala ya jumuiya (vikao vitatu vya kimataifa na kikao cha ana kwa ana katika WikiConference India) ili kushirikisha katika mazungumzo ya pande mbili na wafanyakazi wa kujitolea na washirika kuhusu vipaumbele vyetu vya pamoja vya mwaka ujao wa fedha.

Hatimaye, Shirika liliandaa mijadala mitano ya mada: moja kuhusu mitindo ya nje na akili bandia na minne kuhusu maeneo ya kuzingatia ya kazi yetu ya Bidhaa na Teknolojia. Zaidi ya watu 690 (hadi ~38%[1] kutoka mwaka jana) walijiunga na mazungumzo ya moja kwa moja katika lugha 13 (takriban 217% kutoka lugha 6 mwaka jana) kuhusu mpango huo na zaidi ya watu 60 walijadili mpango huo kwenye wiki, hasa kwenye ukurasa wa majadiliano kuhusu kazi yetu ya Bidhaa na Teknolojia na ukurasa wa majadiliano kuhusu rasimu ya mpango kamili wa mwaka. Maoni ya kurasa kwenye wiki yaliongezeka kwa 203% - 34,604 mwaka huu dhidi ya 17,000 mwaka jana. Muhtasari wa mpango ulitafsiriwa katika lugha 30+ (zaidi ya 200% kutoka mwaka jana).

Maoni kwa ujumla

 1. Kujikita kwenye Bidhaa na Teknolojia, na haswa, malengo ya warsha na matokeo muhimu, kuliunda fursa muhimu za maoni na ufafanuzi kati ya wafanyikazi na watu waliojitolea.
  Mwaka huu, mpango wa kila mwaka wa Shirika la Wikimedia uliweka mkazo mkubwa katika kazi yetu katika bidhaa na teknolojia, likileta umakini kwa ukubwa wa juhudi zetu katika maeneo haya kama sehemu ya kazi yetu ya jumla na vile vile lengo mahususi kwa mwaka huu ujao juu ya mahitaji ya wahariri imara. Ili kufikia hili, tulichapisha rasimu ya hatua ya awali "orodha" ya maeneo ya kazi kabla ya mpango wa mwaka, ikifuatiwa na rasimu Malengo na Matokeo Muhimu (OKRs) kwa mawazo zaidi na maoni ya jumuiya. Hii ilifuatiwa na mijadala kwenye wiki kati ya wafanyakazi na wahariri kuhusu lugha, lengo, vipimo, na mbinu ya jumla ya OKR zetu, pamoja na makundi lengwa ya watumiaji wanaohusika zaidi katika maeneo mbalimbali ya kazi yetu iliyopangwa. Watu 120 walishiriki katika mashauri haya.
  Katika majadiliano ya Bidhaa na Teknolojia (Lengo la 1: Kuboresha Maarifa kama Huduma), mada za mazungumzo zililenga zaidi kufafanua madhumuni ya matokeo muhimu mahususi (KRs), na pia kubainisha matokeo yasiyotarajiwa ya vipimo lengwa ikilinganishwa na vile yalivyokuwa yameandikwa hapo awali. Mada na maoni ya jumla ambayo Shirika lilipokea ni pamoja na:
  • Usaidizi wa kuzingatia mahitaji ya wahariri wenye uzoefu, hasa kushirikiana na wahariri wapya kwa njia chanya ambayo pia hupunguza mzigo wa kazi kwa ujumla.
  • Usaidizi wa kazi ya kuongeza hariri ambazo hazijarejeshwa, hasa kutoka kwa wahariri katika Kusini mwa Ulimwengu na wahariri wanaoshughulikia mada za jinsia na LGBTQ+
  • Istilahi kuhusu kuelezea "wahariri wenye haki zilizopanuliwa"/ambao wanaweza kufikia taarifa zisizo za umma ni ngumu. Tunakosa lugha ambayo imeshiriki maana na matumizi katika wiki kwa kundi hili pana la wachangiaji
  • Thamani ya kuunda zana zinazojulikana zaidi katika miradi ya Wikimedia
  • Umuhimu endelevu wa kuipa Toolforge kipaumbele
  • Haja ya uwazi zaidi wa vipimo na uchanganuzi
  • Matumaini na tahadhari kuhusiana na jukumu la akili ya bandia
  • Baadhi ya watu waliona kazi ya picha na sauti havipaswi kupuuzwa
  Mandhari haya mapana, pamoja na mapendekezo yaliyolengwa zaidi yatajumuishwa katika mbinu ya idara za Bidhaa na Teknolojia katika mwaka ujao wa fedha.
 2. Vipaumbele vilivyoainishwa vya Shirika vinaendana na vipaumbele katika harakati za Wikimedia.
  Maeneo haya ni pamoja na:
  • Kukuza kwa ufadhili wa jumla wa ruzuku, hata pale wakati maeneo mengine ya bajeti yanapunguzwa au kudumishwa
  • Kuendelea kwa uwekezaji katika maendeleo na majaribio ya kitovu cha kikanda na mada
  • Kuendelea kwa uwekezaji katika majukumu ya kikanda, ya wafanyakazi yanayoikabili jamii na kuwekeza muda wa wafanyakazi katika kujenga mahusiano ya muda mrefu ya jamii
  • Kufanya miradi ya Wikimedia kufikiwa zaidi, ikiwa ni pamoja na walemavu wa macho
  • Kuzingatia changamoto za kijamii na kiufundi zinazohusiana na udumishaji wa wahariri
  • Kushughulikia changamoto zinazohusiana na vizuizi vya IP na changamoto na habari potofu/upotoshaji ambao ni changamoto haswa kwa Wanawikimedia kutoka Kusini mwa Ulimwengu.
  Kwa mwaka ujao, ilipendekezwa kuwa Shirika litafute kwa uwazi zaidi maoni yaliyoelekezwa kwenye maeneo ya mpango wa mwaka ambayo yanahusiana na kazi au utaalamu wa vikundi tofauti vya harakati, na pia kutaja kinagaubaga mwingiliano na mipango na fursa zingine za Wikimedia kuhusu ushirikiano katika harakati zote. (Zaidi juu ya hili katika kipengele cha tano.)
 3. Umaalumu na uwazi wa rasimu ya mpango wa mwaka huu ulithaminiwa sana kama mfano wa Shirika "jipya".
  Tukiongelea kwa ujumla, urefu, sehemu za kuzingatia, na muundo wa rasimu ya mpango wa mwaka huu zilipokelewa vyema. Hasa, wafanyakazi wa kujitolea walionyesha kuthamini maelezo ya mpango wa kila mwaka, katika masuala ya shughuli zinazokusudiwa na Shirika kwa mwaka ujao na vile vile kuchapisha maelezo ya kina kuhusu shughuli za Shirika, mbinu za kulipa fidia, matarajio ya bajeti na mishahara ya watendaji wakuu. Jumuiya pia zilithamini upatanishi wa mpango huu kwa mchakato wa mkakati wa harakati na mapendekezo.
  Zoezi lingine muhimu katika mpango wa mwaka huu lilikuwa ni mbinu yake ya ushirikishwaji wa lugha nyingi. Muhtasari wa rasimu ya mpango ulitafsiriwa katika lugha 34, na Shirika lilijiunga na mijadala 6 ya moja kwa moja iliyoangazia ukalimani wa moja kwa moja, iliyochukua jumla ya lugha 10. Vikao hivi vya mtandaoni bilihudhuriwa na watu wengi, na takriban watu 510 walijiunga kushiriki katika lugha waliyochagua.
  Hatimaye, Shirika lilisikia kutoka kwa wafanyakazi wa kujitolea ambao walifurahi kuona kipindi cha mwezi mzima kilichotolewa kwa maoni ya jumuiya.
 4. Kulikuwa na majadiliano kuhusu maelezo mengi ndani ya mpango kuanzia mienendo ya nje na maelezo ya Shirika hadi malengo manne.
  Wanawikimedia walivutiwa na mada mbalimbali katika mpango wa kila mwaka wa Wakfu, na walishiriki maswali na mawazo mapya kuhusu mada mpya ambazo waliona ni muhimu kuzingatiwa katika mipango yetu ya mwaka ujao. Mada hizi zilijumuisha Uchina, muundo wa ufadhili wa Wakfu, mwelekeo wetu wa kaboni, zana za mikutano ya video, umuhimu wa ulinzi wa hakimiliki, zana za kupakia bechi za Commons, kujifunza kwa mashine, kuvutia watumiaji wapya, usawa wa maarifa, ushirikiano wa kiufundi, na mbinu yetu ya kieneo.
  Mabadiliko mengi katika mpango wa mwaka yalikuwa kurekebisha uchapaji na tahajia. Nakili hizi zinajumuisha mabadiliko ya Muhtasari (diff), Historia (diff), Mitindo ya Nje (diff), Malengo (diff) , Usalama na Ujumuisho (diff), Ufanisi (diff), na Maelezo ya Msingi (diff). Ukurasa wa Miundombinu umerahisishwa kidogo (diff) na sehemu kuhusu programu za kimaeneo na mada ilifafanuliwa kwenye ukurasa wa Usawa (diff). Mwishowe, baadhi ya maandishi yalipangwa upya kwenye ukurasa wa Fedha, na maudhui mapya yaliongezwa kuhusu programu za ruzuku (diff).
 5. Upangaji wa kila mwaka ni fursa ya kushiriki katika upangaji shirikishi na harakati, na kujifunza kuhusu vipaumbele kutoka mikoa na jumuiya mbalimbali.
  • Kikundi cha Wikimedistas Wayuu kilishirikisha kazi wanayofanya katika jamii na kushirikisha habari kwamba mnamo Februari 27, 2023, Wikipeetia süka wayuunaiki habari hatimaye ilizaliwa!
  • Jumuiya ya Kundi la Watumiaji wa Wikimedia Haiti ilishirikisha warsha zao za michango kuhusu miradi ya Wikimedia, ushiriki katika kampeni za kimataifa na matukio ya Wikimedia, na mwito wa michango katika Kikrioli cha Haiti.
  • Projeto Mais Teoria da História na Wiki ilishirikisha sehemu ya miradi ya 2022 na mbinu ya mada: Jinsia, Jinsia, Rangi na Epistemolojia za Kusini mwa Ulimwengu.
  • Wanawikimedia barani Afrika wananuia kufanyia kazi masuala yanayohusu habari potofu na habari zisizo sahihi, na hasa, kushirikiana na Shirika kwa kushirikiana na wadau husika na kuongeza ufahamu miongoni mwa wajitoleaji wa kanda. Pia walionyesha nia ya kuendeleza mazungumzo juu ya miundo ya Hebu na utawala wa harakati.
  • Jumuiya ya Asia ya Mashariki na Kusini-Mashariki na Pasifiki (ESEAP) inatarajia kukaribisha Wikimania 2023 kama njia ya kujenga jumuiya ya kikanda.
  • ESEAP pia inajitahidi kuunda kitovu cha eneo, kwa kuanza na kuunda kamati ya kuzindua kazi hii katika Wikimania, kuandaa mkutano wa ESEAP wa 2024, na kuimarisha mashindano ya kikanda kama vile Wiki Loves Earth na Wiki Loves Monuments.
  • Wikimedia Australia inahitimisha mwaka wa kwanza wa mpango mkakati wa miaka mitatu unaolenga usawa na ushirikishwaji, ushirikishwaji, na kujenga uwezo (kuanzisha ofisi, tathmini, kanuni za utawala). Pia watakuwa wakikuza kazi na ushirikiano ili kuongeza maudhui mbalimbali kwenye wiki.
  • Wikimedia Indonesia hivi karibuni itatoa mpango wa miaka mitano, na mwaka huu ujao utaangazia ushirishaji, ushirikiano, utafiti na kujenga uwezo.
  • Wikimedia Taiwan itaangazia ushirikiano wa GLAM, utetezi wa kisheria, na kufanya kazi na lugha ndogo za asili ili kuwasaidia katika kuzindua Wikimedia zao. Pia wanatekeleza mfumo wa usimamizi wa uhusiano wa mteja (CRM) na washirika wao.
  • Jumuiya ya WikiSource inapenda kuongezeka kwa usaidizi, hasa kwa ajili ya kutekeleza kampeni za Wiki Loves Manuscripts.

Jumuiya na watu binafsi wa kujitolea pia walitoa mapendekezo kadhaa kuhusu jinsi Foundation inaweza kuimarisha ushirikiano na usaidizi mwaka huu:

 • Jumuiya za Amerika ya Kusini na Caribbean ziliomba ufafanuzi na uhakikisho kuhusu majukumu na njia husika za kufanya kazi pamoja kwa washirika na Wakfu wa Wikimedia katika kuchangisha pesa.
 • Kutumia video zaidi, infografikia, na taswira zingine pamoja na maandishi mafupi, ya muhtasari ili kufanya mawasiliano katika harakati za Wikimedian kufikiwa zaidi.
 • Umuhimu wa Shirika kuratibu na washirika mahalia kabla ya kusaini barua zozote za wazi
 • Haja ya msaada zaidi wa kimsingi kwa Wikimedian wanaoteswa na mamlaka kwa sababu ya kazi yao kwenye miradi

Takwimu

Nyenzo kwenye Wiki

Ukurasa Utazamaji wa kurasa
Kurasa kuu za rasimu ya mpango wa kila mwaka (jumla) 30,935
Ukurasa wa majadiliano wa Rasimu kuu ya Mpango wa Mwaka 1,652
Sasisho la Mpango wa Mwaka wa Maryana & Barua ya usikilizaji wa Selena 480 + 490
Kurasa zingine za kwenye wiki 1,047
JUMLA 34,604 (hadi 203% kutoka 17,000 mwaka jana)

Mijadala Mbashara

Tarehe Mjadala Washiriki (makadirio) Tafsiri
Februari Kamati ya Masuala ya Jamii, "Mazungumzo na Wadhamini" 60 ES
23 Machi Akili Bandia ndani ya Wikimedia 100 ES
26 Aprili Mpango wa Mwaka wa Kimataifa 88 FR, PT, ES
27 Aprili Uandaaji wa Mpango wa Mwaka 111 AR, FR, PL, RU, SW
27 Aprili Maboresho ya mtiririko wa kazi kwa kikundi cha "wasimamizi" (wasimamizi na kamati) 16 hakuna
28 Aprili Wikiconference India 180 HI, UR, PA
30 Aprili Uaandaaji wa Mpango wa Mwaka 70 ZH, JA, ID
3 Mei Maboresho ya mtiririko wa kazi kwa kikundi cha "wasimamizi" (Watumiaji wa kawaida) 12 hakuna
4 Mei Maboresho ya mtiririko wa kazi kwa kikundi cha "wasimamizi" (wazi) 17 hakuna
5 Mei Hadhira ijayo 16 hakuna
18 Mei Mkutano wa Kamati ya Masuala ya Jamii, "Mazungumzo na Wadhamini" 30 hakuna kilichoombwa

Utafsiri na Ukalimani

Hesabu za lugha ni pamoja na zile ambazo bado zinaendelea.

 1. Some data incomplete

Ushirikishwaji

Wanawikimedia wana nafasi ya kushirikiana na Wikimedia Foundation kwenye wiki hadi tarehe 19 Mei na katika mijadala mbalimbali mubashara. Ushirikiano huu utaarifu maudhui ya mwisho ya mpango wa mwaka wa Wikimedia Foundation kwa mwaka wa fedha unaoanza tarehe 01 Julai 2023 hadi 30 Juni 2024.

Muhtasari wa slaidi za Mpango wa Mwaka. Lugha zingine: (ar, zh, fr, hi, pt, uk, id, es, ru, sw, ja)

Mazungumzo Mbashara

Mazungumzo haya yanatoa fursa kwa wanachama wa Harakati za Wikimedia kushirikisha mipango na nia zao za mwaka ujao na Shirika na wao kwa wao, na pia kujifunza zaidi na kutoa mapendekezo kuhusu mpango wa kila mwaka wa Shirika.

Wanajamii wanakaribishwa kuhudhuria vikao vya mtandaoni vya moja kwa moja vinavyowafaa. Ikiwa ungependa kuhudhuria kiako na tafsiri haipatikani katika lugha unayopendelea, tafadhali tuma barua pepe kwenda movementcomms(_AT_)wikimedia.org na tutakupangia.

 1. Machi 23 saa 18:00 UTC kikao cha wazi kuhusu Akili Bandia ndani ya Wikimedia. (kimemalizika)'
 2. Aprili 26 kutoka : Mazungumzo na Shirika la Wikimedia. Ufafanuzi utapatikana katika Kiingereza, Kifaransa, Kireno na Kihispania.Kiungo cha Mkutano Ongeza kwenye Kalenda (kimeshafanyika, rekodi)
 3. Aprili 27 kutoka : Mazungumzo na Shirika la Wikimedia. Ufafanuzi utapatikana katika Kiarabu, Kifaransa, Kipolandi, Kirusi na Kiswahili. Kiungo cha Mkutano (kimeshafanyika, rekodi)
 4. Aprili 28: Mazungumzo ya kibinafsi na Shirika la Wikimedia kwa ushirikiano na WikiConference India. Rekodi ya video ya tukio hili na madokezo yatashirikiwa hapa yanapopatikana. (Yameshafanyika)'
 5. Aprili 30 kutoka : Mazungumzo na Shirik la Wikimedia. Ufafanuzi utapatikana katika Kichina cha Mandarin, Kijapani na Kiindonesia. Kiungo cha Mkutano Ongeza kwenye Kalenda. (yamefanyika, rekodi)

Mazungumzo ya kikundi cha Focus Group

Pamoja na mazungumzo ya jumla hapo juu, idara ya Bidhaa na Teknolojia ya WMF inaandaa baadhi ya mazungumzo ya kikundi kidogo. Haya kila moja yamejikita katika kujadili sehemu mahususi ya rasimu ya hati ya "malengo na matokeo muhimu" na kundi la watu ambao wanaweza kuathiriwa na OKR hiyo. Hizi ni pamoja na:

Kumbuka, mazungumzo haya hayakukusudiwa kuwa ya kina katika utangazaji wao. Washiriki wakiidhinisha, madokezo na/au rekodi ya mikutano itatolewa. Maoni kutoka kwa mtu yeyote kuhusu OKR zozote bado yanakaribishwa kwenye sehemu husika ya ukurasa wa mazungumzo wa rasimu.

Kwenye-Wiki

Toleo la muhtasari wa mpango wa mwaka litachapishwa ndani ya nchi katika lugha nyingi kwenye Wikipedia mbalimbali. Toleo kamili litakaloambatana na tafsiri litapatikana kwenye tovuti hii ya Meta-Wiki. Unaweza kushirikiana nasi kwenye kurasa zote za mazungumzo ya ndani na hapa kwenye ukurasa wa mazungumzo wa Meta-Wiki hadi 19 Mei. Tutaongeza viungo hapa ambapo maudhui yatakuwa yamechapishwa kadri yanavyopatikana.

Idara ya Bidhaa & Teknolojia pia imechapisha rasimu ya "malengo na matokeo muhimu", na inatafuta maoni kuhusu ukurasa huo wa mazungumzo katika kipindi chote cha Aprili na Mei.