Jump to content

Kutafuta Fedha 2012/Kutafsri/Utafiti wa Wafadhili

From Meta, a Wikimedia project coordination wiki
This page is a translated version of the page Fundraising 2012/Translation/Donor survey and the translation is 100% complete.


E-mail

Email subject

Ukaguzi wa wahisani wa Wakfu wa Wikimedia - tafadhali tusaidie na maoni yako

Email body

Mpendwa <jina>,

Unapata barua pepe hii kwa maana umechangia kwa Wakfu wa Wikimedia wakati wa harambe yetu ya kila mwaka. Usaidizi wako ni wa thamani sana. Ahsante sana.

Tungependa kupokea maoni kutoka kwako kutokana na uzoefu wako wa kuchangia. Maoni haya ni ya muhimu kwa ajili ya kutoa uzoefu bora kwako na wafadhili kutoka nchi yako , kwa hivyo tafadhali chukua muda wa kujibu maswali kadhaa juu ya mchango wetu.

Kutazama ukaguzi wa wafadhili, bonyeza hapa: <survey link>

Kama una maoni mengine yeyote ama ungependelea kutuma barua pepe, tafadhali tuma maoni yako kwa donorsurvey@wikimedia.org. Twashukuru usaidizi wako!

Asante, Timu ya Harambee ya Wikimedia


Ukaguzi wa Wafadhili

Wikipedia inahitaji maoni ya msaidizi kujifunza juu ya taarifa maalum kuhusu nchi husika na njia bora ya kujenga uzoefu wa wafadhili. Majibu yako ya maswali yaliyo hapa chini yatatusaidia kutoa uzoefu bora wa mchango kwa wafadhili wote wa ndani .Tafadhali chukua muda kupitia ukurasa wa mchango ambao utakusaidia kujibu maswali hapa chini.

1. Jambo la muhimu zaidi lililofanya uchangie ni nini?

 • Ninaunga mkono maarifa ya bure kwa wote.
 • Mwito ulikuwa wa dhati na adilifu
 • Mimi hutumia Wikipedia wakati wote na nilitaka kuchangia kwake.
 • Kuendeleza Wikipedia kuwa bila mabango ya matangazo.
 • Mengine (tafadhali fafanua)

2. Hisia yako ya mwito wa kibinafsi kutoka kwa mwanzilishi wa Wikipedia Jimmy Wales ulikuwa nini?

 • Ni ujumbe fanisi na nilishikamana nawo.
 • Ulikuwa umeandikwa kwa lugha nililoelewa
 • Lugha iliyotumiwa ilikuwa bila mpangilio na ngumu kuelewa.
 • Sehemu nyingine ya ujumbe ilikuwa ya kuchanganya
 • Sehemu kubwa ya ujumbe haikueleweka
 • ulikuwa ujumbe hafifu na siku patana nawo
 • Mengine (tafadhali fafanua)

3. Ungependelea kuchangia na sarafu gani?

 • Rand ya Afrika Kusini (ZAR)
 • CFA franc ya Africa Magharibi ()XOF
 • CFA franc ya Afrika ya Kati (XAF)
 • Shilingi ya Kenya (KES)
 • Euro (EUR)
 • Dola ya Marekani (USD)
 • Mengine (tafadhali fafanua)

4. Waweza fikiria kuchangia hata kama sarafu ya nchi yako haingekuwa hapa?

 • La, ningechangia tu na sarafu ya mtaa / nchi yangu
 • Ndio, ningechangia bado, hata na sarafu ya kigeni.
 • Ndio, lakini ningechangia tu na sarafu zifwatazo:

(tafadhali orodhesha zaidi ya moja ikibidi)

5. ungependelea njia gani ya kulipa?

 • Kadi la mikopo
 • Kadi ya Debiti
 • Kupitia benki
 • Kadi iliyolipiwa hapo mbeleni
 • Paypal
 • Inalipishwa kwa bili yako ya simu ya mkono
 • Mengine (tafadhali orodhesha zaidi ya moja ikibidi)

6. Je, ungechangia ijapokuwa njia ya kulipa unayopendelea (kadi ya mikopo, kupitia benki n.k.) haingekuwepo

 • La, ningechangi tu kama njia ninayo pendelea ya malipo ingekuwepo.
 • Ndio, ningechangia bado.
 • Mengine (tafadhali fafanua)

7. Je, kulingana na sarafu iliyokubalika, fedha ilioko katika mkono wa kulia uko sawa? [URLGOESHERE Bonyeza hapa] kutazama kiungo

 • Ndio, ni barabara
 • La, idadi hizo zinaonekana kuwa juu sana
 • La, idadi hizo zinaonekana kuwa chini sana
 • Kama la, ni idadi ipi ingekuwa sahihi zaidi

8. Tafadhali bonyeza kiungo ulichopewa, ambacho kitakuelekeza kwa anwani ya tovuti ya fomu yetu ya kuchangia. Je, yafanana na ulivyozoea kuandika anwani yako? [URLGOESHERE Bonyeza hapa] kutazama kiungo

 • Ndio, yafanana na jinsi ninanvyoandika anwani yangu
 • La, kulikuwa na uga uliyokosekana / kulikuwa na uga mengi sana
 • Kama la, tafadhali tujulishe ni nini ilikuwa na kosa au utupe mfano wa muundo sahihi wa anwani ya nchi yako

9. Kurasa zilikuwa na ujumla, viungo, na nyuga za habari zilikuwa rahisi kuelewa na katika lugha uliyojiskia vizuri kutumia?

 • Ndio, nilielewa kila kitu
 • La, uga mwingine/tafsiri/chaguo hazikuwa wazi au sahihi
 • kama la, tujulishe jinsi ya kuboresha

10. Nini ilikuwa hisia yako kwa ujumla ya ukurasa wa mchango?

 • Ilitumia istilahi za mitaa na chaguzi zilozotengenezwa mahsusi kwa ajili ya nchi yangu.
 • ilitumia istilahi na chaguzi za mtaa, lakini ilikuwa na vipengele kadhaa visivyokuwa sahihi.
 • Ilitumia istilahi na chaguzi za mtaa, lakini ilikuwa na vipengele vingi ambavyo havikuwa sahihi.
 • Ilionekana kana kwamba ilikuwa imetengenezwa kwa ajili ya nchi tofauti.
 • Nyingine (tafadhali taja)

11. Tafadhali tumia nafasi iliyopo hapa chini kuandika maelezo yoyote au maoni uliyo nayo kuhusu ukurasa wa misaada na ujumbe.

Asante kwa mara nyingine tena kwa ajili ya kusaidia Wikimedia, isiyo ya faida ambayo inasaidia Wikipedia.

Siri yako ni muhimu sana kwetu. Isipokuwa kwa mujibu wa sheria, sisi tutashiriki majibu yako na Wikimedia na makandarasi wake. Tunaweza, hata hivyo, hadharani kushiriki majibu bila majina na takwimu juu ya utafiti huo. Sisi kamwe hatutachapisha jina lako au anwani ya barua pepe, hata hivyo, tunaweza kutumia habari hii kuwasiliana na wewe kuhusu Wikimedia na shughuli zake. Wikimedia ni shirika duniani kote. Kwa kujibu maswali haya,, unaidhinisha uhamisho wa majibu yako kwa nchi ya Marekani na maeneo mengine kama inaweza kuwa muhimu. Unaweza kupata taarifa juu ya sera ya faragha Utafiti wa Monkey: URLGOESHERE