Jump to content

Uchaguzi wa Shirika la Wikimedia kwa 2015/Mwito kwa wagombea

From Meta, a Wikimedia project coordination wiki
This page is a translated version of the page Wikimedia Foundation elections 2015/Call for candidates and the translation is 100% complete.
Info The election ended 31 Mei 2015. No more votes will be accepted.
The results were announced on 5 Juni 2015. Please consider submitting any feedback regarding the 2015 election on the election's post mortem page.

Tafadhali saidia kushawishi wagombea wapya kwa nafasi za kijamii kwa uchaguzi wa Baraza

Wapendwa Wana-Wikimedia,

Wakati miradi yetu ikiendelea kukua, Ni Muhimu tukatazama mbele ili kuendelea kujenga maarifa ya ulimwengu kwa muongo ujao. Mwezi uliopita, WMF iliwaalika wengi wa wasomaji wetu kushiriki mawazo yao katika ushauri wa mikakati. Baadhi ya majibu yaliyopokewa mara kwa mara yalikuwa maombi kwa uzingatiaji zaidi wa lugha na jamii, ikijumuisha tu wale hivi sasa wanaokuja mtandaoni. Katika harakati zetu za kufikia maarifa katika kila kona ya sayari yetu na katika kila akili inayopanuka, maombi haya yanageuza makini yetu na kuwa yakujumuisha zaidi sauti mbali mbali na zinazochipuka.

Kwa wakati huo huo, Bodi ya Wadhamini imekuwa ikijadiliana ujumuisho wa Bodi, na tunakubaliana kwamba tunahitaji uwakilishi mbali mbali wa jamii na miradi yetu katika uwanachama wetu. Hii inajumuisha kuleta wadhamini kutoka kwa jamii, lugha na miradi yetu wanaowakilisha jiografia na lugha kutoka kote duniani, ikijumuisha wale kufikia sasa hawajajumuishwa au kuwakilishwa vyema katika ujumuisho wa Bodi yetu.

Hii ndiyo sababu tunakuomba utusaidie kufikia jamii, katika Wikimedia na zaidi, kuleta wagombeaji bora wawezekanao ambao:

  • Wanatoka Afrika, Uhindi, Asia, au Mashariki ya Kati; au
  • Wana utaalamu na mojawapo ya miradi yetu midogo au miradi isiyo ya Wikipedia; au
  • Wana utaalamu wa undani katika teknolojia na bidhaa au fedha; na
  • Wana uzoefu wa usimamizi msingi (kufunza, usimamiaji watu, usimamiaji mradi, uzoefu katika bodi kubwa zaidi isiyo ya kifaida, haswa zile za mashirika ya kimataifa, n.k.)

Wagombeaji wote wawezekanao lazima waweze kuwasiliana na kujadiliana kwa Kiingereza, kwani hii ndiyo lugha tunayotumia katika majadiliano yetu yote ya bodi. Wadhamini wenye ufanisi pia wana msukumo wa misheni, ni wenye mikakati, wazingatiaji, wana uadilifu mkubwa, na ni wenye heshima na wanafikiri kuhusu jamii.

Bodi imejitolea uanuwai na usawa wa kijinsia. Tafadhali tusaidie kupata wagombeaji ambao wana mitazamo na sauti ambazo hazijawakilishwa vyema, lakini ambao ushiriki wao ni muhimu kwa siku zijazo za miradi yetu. Pia tunatia moyo wagombeaji kutoka kwa miradi na jamii zetu zote wanaozingatia kugombea Bodi kufanya vile pia, na watie moyo wapiga kura wote waliohitimu kushiriki kwa kuuliza maswali na kupiga kura. Tunahitaji ushiriki kamili wa jamii ya Wikimedia ili kuhakikisha kwamba Bodi ina nguvu na ina uanuwai iwezekanavyo kuenda mbele.

Ili kupata taarifa zaidi, kuuliza maswali, au kuteua wagombeaji tafadhali tembelea ukurasa wa mwanzo wa uchaguzi:

Asante kwa uungaji mkono wako,
Bodi ya Wadhamini ya Wikimedia Foundation

Tunatafuta memba 5 wapya na mchunguzi maalum kujiunga na Kamati ya Usambazaji Fedha

Jambo Wana-Wikimedia,

Kama unavyweza kuwa unajua, Kamati ya Usambazaji Fedha (FDC) ni kamati ya kujitolea inayofanya mapendekezo kwa Bodi ya Wadhamini kuhusu jinsi ya kutumia fedha ili kufanikisha malengo ya vuguvugu. Kila mwaka, FDC inakutana mara mbili ili kufanya shauri kwenye mapendekezo ya ruzuku ya mpango wa mwaka yaliyopendekezwa na mashirika ya Wikimedia. Imegawo kupitia mchakato shirikishi, wazi, wa pamoja wakufanya ruzuku, fedha hizi zinatumiwa na mashirika kupanua na kuimarisha ushiriki na kuwezesha uundaji na uhariri wa maudhui yenye ubora kwenye miradi ya Wikimedia.

Viti vitano kwenye kamati vimo wazi mwaka huu, na pia nafasi ya mchunguzi maalum. Kuhudumu katika kamati hii ni fursa ya kuimarisha ushiriki wa kao katika vuguvugu, kujenga uongozi na uzoefu wasko, na kufanya kazi karibu na wafanyikazi wenzako walio na nia ya kusaidia vuguvugu kufanikisha athari zaidi.

Majukumu ni makuu: utatarajiwa kuja kwa angalau mikutano miwili ya ana-kwa-ana kila mwaka inayodumu ka siku 4, kwa ziada ya kupitia zaidi ya mapendekezo 18 na nyaraka muhimu za usuli kila mwaka. Kwa memba wengi wa kamati, ushiriki katika mikutano hii pia inajumuisha usafiri mkubwa wa kimataifa. Kumbuka kwamba kamati itakutana San Francisco kwa kipindi cha siku nne kuanzia Novemba 15-21, kwa hivyo lazima upatikane wakati huu.

Tunatafuta kundi tofauti la watu wenye sifa zifuatazo:

  • Uzoefu katika kuelekeza au kutathmini mipango, ndani au nje ya vuguvugu la Wikimedia;
  • Utaalamu katika ruzuku (umepokea au umesimamia fedha za ruzuku au un auzoefu katika kutengeneza ruzuku);
  • Maarifa na uelewa wa, na uaminifu ndani ya vuguvugu la Wikimedia na kwenye miradi ya Wikimedia (yaanim uzoefu na miradi ya Wikimedia, mashirika ya Wikimedia, au vyeo vya uongozi kwenye tovuti);
  • Tuantafuta tofauti katika jinsia, geofrafia na lugha kwenye kamati, vile vile uzoefu na vyeo tofauti ndani ya vuguvugu la Wikimedia (k.m. wachangiaji maudhui, viongozi wa mpango, viongozi wamakundi ya watumizi, watendaji, member wa bodi)

Ili kupata taarifa zaidi kuhusu mahitajiko ya ustahiki, jinsi ya kuteua wagombeaji, au kuchapisha ujiteuaji wako mwenyewe tafadhali tembelea ukurasa wa mwanzo wa uchaguzi:

Tafadhali wasiliana nami na mswali yoyote.

Kwa Dhati,
Katy Love
Afisa Mkuu wa Mpango
Kamati ya Usambazaji Fedha