Jump to content

Fundraising 2012/Translation/GorillaWarfare appeal

From Meta, a Wikimedia project coordination wiki
This page is a translated version of the page Fundraising 2012/Translation/GorillaWarfare appeal and the translation is 100% complete.

  • Tafadhali soma:
    Rufaa binafsi kutoka kwa
    mchangiaji mwenye hariri 18,000

Appeal

Kutoka kwa mchangiaji wa Wikipedia

Mimi ni mwanafunzi katika chuo kikuu. Vitabu vya kiada vya muhula mmoja vitanigharimu $500. Katika Wikipedia, huwa napata habari ya bure yenye dhamani ya ma elfu ya vitabu.

Ndiyo maana mimi sisomi tu Wikipedia, mimi husaidia kuijenga. Ni muhimu kwangu kufanya rasilimali hii kupatikana kwa kila mtu, bila malipo. Na wasomaji milioni 470 kwa mwezi, Wikipedia ni muhimu kwa watu wengi duniani kote.

Wikipedia ingeanguka na kuwa vipande vipande muda mrefu uliopita. Inaendeshwa na makubaliano, tofauti na jamii nyingine yeyote. Hakuna utawala halisi mkuu, hakuna bodi ya watendaji kuamua kila hariri na kila sera. Badala yake, jamii kubwa ya wahanga hufanya kazi kwa pamoja kuunda chanzo hiki cha maarifa, huru kutumia na huru bila ya matangazo.

Kwa kufanya kazi kwa njia hiyo, jamii yetu ya mamilioni ya wahariri inafanya kazi pamoja kujenga kamusi elezo katika lugha 283, zenye jumla ya pamoja ya makala zaidi ya milioni 20.

Sisi hufanya hivyo juu ya bajeti ndogo ikilinganishwa na tovuti nyingine za juu. Ili sisi kufanya kazi yetu, tunahitaji miundombinu imara: seva, Upana-bendi, programmers, na hata wanasheria kulinda uhuru wetu. Haya yote yanafadhiliwa na michango kutoka kwa wasomaji wa Wikipedia. Unaweza kufikiri dola chache tu ni kiasi kidogo sana, lakini ndizo hufanya kazi hii yote inawezekana.

Shukrani sana.