Jump to content

Mpango wa Mwaka wa Wikimedia Foundation/2023-2024

From Meta, a Wikimedia project coordination wiki
This page is a translated version of the page Wikimedia Foundation Annual Plan/2023-2024 and the translation is 100% complete.

Muhtasari

Shirika la Wikimedia Foundation limesalia katika kipindi cha mpito. Lilikaribisha uongozi mpya mwaka jana, ikiwa ni pamoja na Afisa Mtendaji Mkuu mpya na Afisa Mkuu wa Bidhaa na Teknolojia. Zaidi ya hayo, Shirika limeongoza mazungumzo na jamii zetu za kimataifa kuhusu masuala mbalimbali muhimu, kutoka hati ya siku zijazo inayofafanua majukumu na wajibu, hadi jinsi tunavyochangisha rasilimali za pamoja kupitia harambee ya bango. Mpango wa Mwaka wa mwaka huu unajaribu kutoa ufafanuzi zaidi kuhusu masuala ya kimkakati ya miaka mingi ambayo hayana marekebisho ya haraka, na chembechembe ya taarifa zaidi kuhusu jinsi Shirika linavyofanya kazi. Maoni kutoka kwa wadau wetu wengi yanakaribishwa na kuthaminiwa.


Soma hapa chini muhtasari wa Mpango wa Mwaka wa 2023-2024.

Tulipo leo

Mwaka jana,tuliamua kuelekeza nguvu zetu katika Wikimedia Foundation katika kubadilisha kwa kiasi kikubwa jinsi tulivyofanya kazi yetu. Hii ilijumuisha kupanga kazi yetu kikanda ili kukabiliana na mahitaji ya jamii duniani kote, kwa kufanya upya maadili yetu ndani ya Shirika ili kuboresha viwango vyetu vya ushirikiano. Hii inatuweka Katika nafasi nzuri zaidi kwa sasa zaidi kubadilisha kile tunachokifanya – hasa kama ulimwengu uliotuzunguka unabadilika kwa njia zisizotarajiwa zaidi na tunaangalia jinsi ya kuwa na matokeo zaidi ya pamoja katika malengo ya pamoja kuelekea mwelekeo wa kimkakati wa 2030.

Kwa mara nyingine tena, lazima kwanza tufikirie mabadiliko ya ulimwengu unaotuzunguka, unachokihitaji kutoka kwetu, na namna tunavyopaswa kukabiliana nao. Tunauwekea msingi mpango huu wa mwaka katika upangaji mkakati wa miaka mingi ili kuzingatia mabadiliko ya muda mrefu katika mapato, bidha na teknolojia za harakati za Wikimedia, na wajibu na majukumu.Mwenendo wa nje unaonesha kuwa majukwaa ya kijamii yanaendelea kuondoa injini za utafutaji za kitamaduni, na kwamba akili bandia inatishia mwingiliano zaidi kwa ulimwengu wa kidijitali. Kwa kuongezea, hali ya kisheria ambayo harakati zetu za kimataifa zinategemea inabadilika sana baada ya miongo kadhaa ya uthabiti. Kwa kujibu vitisho vinavyoendelea kama vile taarifa za upotoshaji na uongo, watunga sheria wanajaribu kudhibiti majukwaa ya mtandao kwa njia ambazo zinaweza kuhatarisha dhamira yetu. Vitisho hivi na kuongezeka kwa ubaguzi huunda sifa mpya hatarishi kwa miradi na kazi zetu. Hatimaye, kuendelea kukosekana kwa uhakika katika uchumi wa dunia kunaongeza kasi ya haja ya kutathmini mwelekeo wa vyanzo vyetu vya mapato, na kufanya uwekezaji sasa ambao unaweza kusaidia ukuaji wa rasilimali ili kufadhili kazi na malengo yetu ya Pamoja.

Mtazamo wetu kwa siku zijazo

Kwa mwaka wa pili mfululizo, Shirika la Wikimedia Foundation linasisitiza mpango wake wa kila mwaka katika mkakati wa harakati wa kuendeleza usawa. Nia yetu ni kuunganisha kazi ya Shirika kwa undani zaidi na Mapendekezo ya Mkakati wa Harakati ili kufanya Maendeleo ya kina zaidi kuelekea Mwelekeo wa Kimkakati wa 2030. Tunasalia kusukumwa kufanya hili kupitia mipango shirikishi na wengine katika harakati ambao pia wanatekeleza mapendekezo. Hili linatekelezwa zaidi Katika kuongeza umakini wetu wa kikanda ili usaidizi wa Shirika ukidhi mahitaji ya jamii tofauti katika maeneo yote duniani. Zaidi ya hayo, Mkataba wa Harakati ujao unatarajiwa kutoa ufafanuzi zaidi kuhusu wajibu, majukumu, ikiwezekana kupitia miundo mipya ya ushirikiano kama vile Vitovu na Baraza la Kimataifa. Tunakusudia kuendeleza ushirikiano wetu na mchakato wa mkataba ili kuendeleza usawa katika kufanya maamuzi kwa ajili ya harakati zetu.

Mbinu ya kupanga kila mwaka:

  • Kuchukua mtazamo wa nje. Kuanza na: nini kinachoendelea katika dunia inayotuzunguka. Kuangalia kwa nje. Kutambua Mitindo ya Nje muhimu inayoathiri kazi zetu.
  • Kulenga katika Bidhaa + Teknolojia. Kurejesha kati usaidizi kwa jamii na watu wanaojitoa kupitia wajibu wetu wa kipekee Katika kuwezesha bidhaa na teknolojia katika kiwango.
  • Mbinu ya kikanda. Kuendelea kuchukua mtazamo wa kikanda zaidi wa kusaidia jamii za kimataifa.

Mwaka huu, Shirika kwa mara nyingine linajikita kwenye mpango wake kuhusu Bidhaa & Teknojia, tukisisitiza jukumu letu la kipekee kama jukwaa la watu na jamii zinazoshirikiana kwa kiwango kikubwa. Sehemu kubwa ya juhudi hii, inayoitwa “Uzoefu wa Wiki,” inatambua kuwa watu wanaojitolea wako katika moyo wa mchakato wa Wanawikimedia wa kuleta maana na kuunda maarifa. Kwahiyo, mwaka huu, tunawapa kipaumbele wahariri mahiri (ikijumuisha wale walio na haki zaidi, kama vile wakabidhi, wasimamizi, wafanya doria, na wasimamizi wa kila aina, pia wakijulikana kama watendaji) badala ya wageni, ili kuhakikisha wana zana zinazofaa kwa kazi muhimu wanayofanya kila siku kupanua na kuboresha maudhui bora, na pia kudhibiti michakato ya jamii. Uendeshaji wa jukwaa kwa ufanisi pia unahitaji Shirika kushughulikia mahitaji makubwa ya miundombinu na data ambayo inaweza kuenea zaidi ya Uzoefu mahususi wa Wiki wa miradi. Kazi hii imefafanuliwa hapa chini kama “Ishara na Huduma za Data.” Na hatimaye, katika jamii iitwayo “Hadhira za Baadaye” ni lazima tuharakishe ubunifu unaoshirikisha hadhira mbalimbali kama wahariri na wachangiaji.

Marekebisho na Machaguo

Mtindo wa kifedha ambao harakati za Wikimedia zilitegemea kwa ukuaji wake mwingi wa kihistoria (uchangishaji fedha wa bango) unafikia kikomo. Mitiririko mipya ya ufadhili ili kukamilisha hili - ikijumuisha Biashara ya Wikimedia na Majaliwa ya Wikimedia - itachukua muda kuendeleza. Haiwezekani kufadhili viwango sawa vya ukuaji katika miaka michache ijayo kama tulivyoona Katika uchangishaji fedha wa bango katika muongo mmoja uliopita, hasa kutokana na mtazamo usio na uhakika wa uchumi wa kimataifa.

Katika kukabiliana na mielekeo hii, Shirika lilipunguza ukuaji mwaka jana ikilinganishwa na miaka mitatu iliyopita. Sasa tunapunguza bajeti ya ndani ikihusisha gharama zote mbili zisizo za watumishi na za watumishi ili kuhakikisha kuwa tuna mwelekeo endelevu zaidi wa gharama kwa miaka michache ijayo. Licha ya shinikizo hizi za bajeti, tutakuza ufadhili wa jumla kwa washirika wa harakati, ikiwa ni Pamoja na kupanua ruzuku ili: kuzingatia gharama za kimataifa za mfumuko wa bei, kusaidia wageni kwenye harakati, na kuongeza ufadhili wa mikutano kwa matukio ya harakati. Mpango huu unahusisha ufadhili zaidi katika maeneo yote huku ukiweka kipaumbele kwa ukuaji mkubwa katika maeneo yenye uwakilishi mdogo. Ili kuwezesha ukuaji huu kwa washirika na wageni, baadhi ya programu za ruzuku (kama vile fedha za Utafiti na Ushirikiano) zitahitaji kuwa ndogo zaidi. Zaidi ya hayo, tunapotathmini uwezo wa msingi wa Shirika, tunatambua kwamba kuna shughuli ambapo wengine katika harakati wanaweza kuwekwa mahali pazuri zaidi kuwa na matokeo ya maana na kuchunguza njia za kiuhalisia za kuelekea upande huo katika mwaka ujao.

Ili kuwa wazi na kuwajibika zaidi, mpango huu wa mwaka unajumuisha taarifa ya kina ya fedha, hasa kwenye muundo wa bajeti ya Shirika, na vile vile jinsi idara za Shirika zilivyopangwa, na miongozo ya kimataifa na kanuni za fidia.

Malengo

Wikimedia Foundation ina malengo makuu manne mnamo 2023−2024. Yamepangwa ili kufungamana na Mwelekeo wa Kimkakati wa harakati za Wikimedia na Mapendekezo ya Harakati za Mkakati, na kuendeleza kazi nyingi zilizoainishwa katika mpango wa mwaka jana. Hayo ni:

Katika dhamira hii pamoja

Katika sehemu zinazofuata, utapata maelezo mahususi zaidi juu ya kazi ya timu mbalimbali katika Shirika katika kuunga mkono malengo haya manne. Baada ya historia fupi ya kupanga katika Wikimedia Foundation, tunaangalia upande wa nje kile kinachobadilika karibu nasi – na kuuliza hii inamaanisha nini kwa Wikimedia na vipaumbele vya Shirika. Nini kingine tunahitaji kuzingatia? Je, kwa pamoja tunaelekea katika mwelekeo unaotuleta karibu na dira ya harakati ya 2030? Ulimwengu unahitaji nini kutoka kwetu sasa?

Katika kufanya upya thamani ya Wikimedia Foundation, wafanyakazi wetu wameidhinisha kanuni ya kuwa katika dhima hii pamoja. Tunatumai kuwa maudhui yanayofuata hapa chini yatakupa ufahamu wa kina wajjinnikazi inavyofanywa na Shirika inavyojaribu kutimiza ahadi hiyo kwa ajili yetu sote.